Tafuta

#SistersProject

‘In-Visibles’ni filamu ya historia kuonesha wanawake wasioonekana

Filamu hiyo ya dakika 30 itaoneshwa kwa mara ya kwanza wakati wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani utakaofanyika mjini Roma tarehe 13 Mei 2023.Imetengenezwa Afrika,ambayo inaelezea mateso ya wanawake wengi katika bara na kuzaliwa kwa upya maisha mapya shukrani kwa msaada wa wanawake,walei na watawa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Je, Eya Hegnon (fundi wa ushonaji), Agnes Sokpo (mtaalamu wa akili), Benedicta Sokpo (mwanasaikolojia), Christine Munetu (mpishi wa maandazi), Rebecca Ama Agboli (mpishi wa maandazi), Mamatou Akpo Sotondji (mfanyabiashara), Dorcas Fleur Kpodo (mwanzilishi wa kituo cha watoto yatima) na Noeline Ezan Akossiwa (mwanafunzi wa kusuka nywele ),pamoja na wanawake wengine wengi barani Afrika wana kitu gani kinachowaunganisha barani Afrika? Uzoefu wa kuachwa, wa vurugu, wa upweke, wa ukosefu wa ajira.  Kama wasingekuwa  Watawa wa Maria Mama wa Kanisa na watawa wa mashirika mengine, wanawake hawa bado wangeachwa, peke yao na bila kazi. Ni wanawake wasioonekana ambao  kinyume chake filamu yenye kueleza mambo halisi yenye kichwa  “In-Visibles” ya dakika 30 inataka kuwaonesha.

Mpango wa WUWCO(UMOFC) kuhusiana na filamu ya kweli barani Afrika
Mpango wa WUWCO(UMOFC) kuhusiana na filamu ya kweli barani Afrika

‘In-Visibles’ itaweza kuonekana kwa mara ya kwanza mnamo Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 asubuhi, wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Wakatoliki Duniani (Umofc) unaoendelea mjini Roma. Katika mahojiano na Vatican News, Bi  Maria Lia Zervino, rais wa UMOC na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake Duniani (OMD), anathibitisha kwamba ‘In-Visibles’ inataka kutimiza utume wa uwakilishi  ambao ni kuwapa mwonekano wanawake wasioonekana na wanaoonekana. kwa sababu wamezama kwenye bahari hiyo ambayo Papa anaiita 'utandawazi wa kutojali'. Na pia kutoa kujulikana kwa kazi za watawa . UMofC iliamua kwamba njia bora ya kuongeza ufahamu wa mateso ya wanawake barani Afrika kutokana na unyanyasaji wa kijinsia ilikuwa ni kutengeneza filamu papo kwa . “Na sanaa ndiyo njia rahisi zaidi ambayo tunaweza kujifunua kwa ukweli mwingine, kuwa na ufahamu wa kile kinachotokea, juu ya hali, uzoefu na wanawake ambao wameteseka, lakini ambao, shukrani kwa msaada wa watawa, pamoja , wakiwemo wanawake walei, sasa wameweza kugundua tena maana ya maisha yao na kuunda familia iliyounganishwa katika jamii na kusonga mbele” alieleza Bi Zervino.

Lia Beltrami
Lia Beltrami

Lia Beltrami, Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirika la Maono Aurora Vision, ameteuliwa na OMD kwa utengenezaji wa maandishi. “Ilipopendekezwa kwangu, mara moja nilipenda wazo hilo kwa sababu ni ahadi ya maisha. Baada ya kutambua eneo kati ya Togo na Ghana tulianza kufanya kazi pamoja, na wanawake, kwa sababu wanawake barani Afrika  katika kesi hiyo wanapata mateso makubwa ambayo ni ya kawaida katika maeneo yote”  aliiambia Vatican News. Lia alimchagua Sr  Eleonora Agassa, wa Shirila la Watawa wa Mpaji kuwa kama mkurugenzi msaidizi wa utengenezaji wa filamu. Kwa hiyo  “ Nilipenda wazo la kufanya kazi na mtawa ... aina tofauti ya mtawa kuliko mfano uliozoea," alisema, akimaanisha ukweli kwamba Sr  Eleonora ni mwanaanthropolojia na amesomea leseni katika mawasiliano. “Historia nzuri sana nyuma yake ni kwamba mamake Sr. Eleonora yuko katika kundi la Umofc la Togo, ameelezea Lia Beltrami tena. Na Sr Eleonora, kwa hivyo, kama mtawa  tayari yumo  ndani ya wazo hilo, ambapo Umoja wa wanawake wa Kikatoliki hufanya kazi pamoja na watawa kwa faida ya wanawake,  yaani ya wanawake wote wa jamii.

Filamu ya dk 30 itaoneshwa tarehe 13 katika Mkutano  mjini Vatican wa Umoja wa wanawake Katoliki Ulimwenguni
Filamu ya dk 30 itaoneshwa tarehe 13 katika Mkutano mjini Vatican wa Umoja wa wanawake Katoliki Ulimwenguni

Utaalam wa Sr  Eleonora ulikuwa wa msingi kwa utengenezaji wa filamu hiyo, Lia alidokeza. “Usahihi wake na azimio lake lilikuwa la msingi. Lakini pia usikivu wake katika kubainisha historia za kusimulia: kwa sababu mara moja alipanga mikutano yote” pamoja na makutaniko mbalimbali ya watawa na hivyo kupunguza kundi la wanawake la kuzingatia. “Tukio hili lilikuwa zuri, kwangu lilikuwa aina ya uanafunzi, Sr Eleonora alisema kwa Vatican News.  Kwa hiyo “In-Visibles ni kama Pasaka, kwa sababu inasimulia juu ya kushuka kwa mateso makubwa zaidi ambayo wanawake wa Kiafrika walivumilia na kisha kuzaliwa tena, ufufuko wao. Na karibu nao katika ufufuko kuna sura ya wanawake waliowekwa wakfu.” “Ningesema kwamba filamu hiyo haioneshi mateso yote ya wanawake wa Kiafrika, hapana. Hii ni tone tu. Ni kama x-ray na labda sio tu ya wanawake wa Kiafrika, lakini ya wanawake wote ulimwenguni.” Sr Eleonora alieleza zaidi kwamba kipengele kimoja cha mateso wanayobeba wanawake wa Kiafrika ndani yao ni hisia mbaya sana wanapokosa ujasiri wa kuwafungulia wengine, basi "maisha yanakuwa ... yanakuwa kaburi ambalo wanawake wanaishi".

Wanaoonekana kusaidia wasioonekana

"Ningesema tena kwamba kazi ya watu waliowekwa wakfu ndiyo hiyo, msaada huu unaotolewa sio kukidhi hitaji la kitambo, bali kumfanya mtu kuwa huru, ili aweze kujikimu kimaisha. Ndiyo maana natoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema kusaidia mipango ya umoja na jumuiya za kitawa zinazofanya kazi katika eneo hilo la kuwapa uhuru wanawake na familia.” Maria Lia Zervino pia alishiriki katika utengenezaji wa filamu.  Kwa upande wake alisema “Kwangu mimi, kibinafsi, ilikuwa tukio la kusisimua sana.” Tayari alikuwa amesoma tafiti 10,000 ambazo WCO ilikuwa imepokea kutoka kwa wanawake wa Kiafrika katika zaidi ya nchi 30, na alikuwa amesikiliza mamia ya wanawake katika mikutano ya vikundi vidogo. Kila kitu alichosikia na kusoma “kikawa mwili na damu, kikawa halisi”. “Tumegusa kwa mikono yetu, tumeona kwa macho na kuhisi mioyoni mwetu na hatujaelewa tu kwa akili zetu, tumehakikisha kuwa sauti ya wanawake hao inakuwa yetu” alisisitiza. Hapa: kwa sababu hii, shukrani kwa msaada wa mshirika wetu, Hilton Foundation, imewezesha kutoa 'In-Visibles': tunataka kuunda mtandao kati ya mashirika ya kitawa na  mashirika ya kiraia ili kuzindua kampeni ya kimataifa ya kutokomeza vurugu hatua kwa hatua dhidi ya wanawake barani Afrika”.

11 May 2023, 17:12