Tafuta

2023.03.04 Misa takatifu wakati wa Sinodi barani Afrika. 2023.03.04 Misa takatifu wakati wa Sinodi barani Afrika. 

Askofu Gherbreghiorghis:Kanisa Afrika linahitaji uongofu wa dhati!

Kanisa Barani Afrika linahitaji wongofu wa dhati ili kuwa wazi katika majadiliano katika kujenga jamii pamoja yenye isharaza za haki,upatanisho na amani,alisema hayo Askofu wa Jimbo la Emdeber, Ethiopia wakati wa Ibada ya Misa,Jumamosi tarehe 4 Machi 2023 huko Addis Ababa katika awamu ya kibara inayoendelea hadi 6 Machi.

Na Sr. Sheila Pires, - Addis Sababa na Angella Rwezaula;-Vatican.

Katika tafakari yake kwa  washiriki wa Mkutano Sinodi ya kibara huko Addis Sababa katika liturujia  iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kuzaliwa kwa Bwana Jumamosi asubuhi, tarehe 4 Machi 2023, Askofu Musié Gherbreghiorghis wa Jimbo la Emdeber nchini Ethiopia  alielezea hatua ya bara ya Sinodi kama wakati wa neema na kama uzoefu wenye matunda kwa ajili ya Kanisa Barani Afrika. “Afrika nzima inawakilishwa katika mkusanyiko huo.  Kwa sababu tunazungumza lugha tofauti. Tuna asili tofauti za kiutamaduni. Tuna ibada tofauti na bado sisi  ni washiriki wa Kanisa Katoliki lilelile”.

Sinodi ya kibara huko Addis Ababa 1-6 Machi 2023
Sinodi ya kibara huko Addis Ababa 1-6 Machi 2023

Kwa mujibu wa Askofu Musié, mkusanyiko huo ni fursa ya "kushiriki kwa uhuru furaha na mahangaiko yetu ya bara la Afrika. "Jamii ya Kiafrika ni jamii iliyochangamka, yenye maadili tajiri ya kiutamaduni ambayo yanahitaji kuzingatiwa kikamilifu..." Kwa kuongeza amesema "Maadili haya hayapaswi kupunguzwa na udikteta wa demokrasia au utandawazi kwa sababu maadili haya yana mengi ya kufundisha ulimwengu mzima." Askofu Musié katika mahubiri hayo alisisitiza, “kwa sababu migogoro mingi barani Afrika ni miongoni mwa Wakristo, Mchakato wa kisinodi unaalika Kanisa kuwa wazi kwa majadiliano, ili kujenga pamoja jamii inayotambulika kwa haki, upatanisho na amani.”

Sinodi barani Afrika huko Addis Ababa 1-6  Machi kwa uwakilishi wa vitengo vyote
Sinodi barani Afrika huko Addis Ababa 1-6 Machi kwa uwakilishi wa vitengo vyote

Hatua ya kibara ya Sinodi ya Kanisa Barani Afrika inamalizika

Kwa hiyo kuanza tarehe Mosi -6 wajumbe kutoka Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika na Madagascar (SECAM) wamekuwa wakitafakari kutoka katika mazingira ya ndani ya Afrika juu ya Waraka wa Kitendea kazi kwa Hatua ya Bara (DCS). Wakiongozwa na Roho Mtakatifu, Makardinali, Maaskofu, watawa wa kike na kiume na walei walibainisha vipaumbele vinane vya Sinodi ya hatua ya Bara juu ya hati ya Sinodi.

Misa wakati wa mkutano wa kibara huko Addis Ababa, Ethiopia
Misa wakati wa mkutano wa kibara huko Addis Ababa, Ethiopia

Kwa hiyo vipaumbele hivyo: vipaumbele vyenyewe ni  1-Ushiriki wa Kanisa, familia ya Mungu katika kutatua migogoro, vita dhidi ya unyonyaji wa rasilimali katika Afrika na kukuza utawala bora, haki na amani.

2. Sauti na maadili ya Kiafrika yazingatiwe wakati wa kufafanua mafundisho ya Kanisa: maadili ya familia, Ubuntu (mshikamano), Ujamaa (maisha ya kijumuiya), Indaba (mazungumzo ya heshima), ukarimu na uwajibikaji pamoja.

3. Dhana ya Sinodi lazima ihusiane na dhana ya kitamaduni na upyaji wa kiliturujia ili kujibu matamanio, ushiriki, na ukuaji wa jumla wa waamini wa Kiafrika.

4. Sinodi inapaswa kuhusisha usaidizi katika ngazi zote za maisha ya Kanisa ili kukuza ushirikishwaji, ushiriki, na ushirika wa washiriki wote hasa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

5. Sinodi ina maana ya mabadiliko katika mtindo wa maisha wa Kanisa na hivyo hitaji la kuundwa kwa roho mpya ya Kanisa la Sinodi ili kuasisi mtindo wa sinodi kama kielelezo cha kichungaji cha maisha na utendaji wa Kanisa.

6. Sinodi inahitaji kujikita katika tunu za Kanisa la Familia ya Mungu: heshima ya maisha, utu wa binadamu katika kategoria zote na heshima kwa uumbaji.

7.Haki ya hali ya hewa na utunzaji wa ardhi unahitaji kuendelezwa na kuishi

8. Uchungaji wa familia unaozingatia ndoa na changamoto zake katika Afrika ya sasa, hasa mitala, talaka na kuolewa tena, uzazi wa pekee.

TAARIFA ZA SINODI AFRIKA 4 MACHI 2023
04 March 2023, 18:10