Tafuta

2023.02.08 Kanisa Kuu la Iskenderun lilianguka kutokana na tetemeko. 2023.02.08 Kanisa Kuu la Iskenderun lilianguka kutokana na tetemeko. 

Kanisa la Ulaya linawaombea wahanga wa tetemeko la ardhi huko Uturuki na Siria

Kutoka katika mkutano Kanisa la Bara la Ulaya wa awamu ya kibara huko Praga,washiriki wameonesha ukaribu kwa wakazi wa maeneo ya Kusini mwa Uturuki na Kaskazini mwa Siria waliokumbwa na Tetemeko usiku wa tarehe 6 Februari.Ni jeraha kubwa ambalo nchini Siria linaongeza la vita kwa miaka 12 sasa.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Kutoka jiji la Praga ambako mkutano awamu ya Pili ya kibara kuhusu mchakato wa  Sinodi uunaendelea ulioanza tarehe 5 Februari, Makanisa barani Ulaya kutoka na janga wameonesha ukaribu wao na wakazi wa maeneo ya kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Siria walioathiriwa sana na tetemeko la ardhi lilitokea usiku wa tarehe 6 Februari iliyopita. Hadi sasa idadi kubwa ya vifo inazidi kuongezeka pamoja na idadi inayokusudiwa kuongezeka zaidi na  uharibifu, mateso ya watu wengi ambayo yameathiri sana na kugusa roho zao.  Washiriki wa Mkutano huo wamebainisha kwamba “hili ni jeraha kubwa, ambalo nchini Siria linaongezwa na lile la vita vinavyoendelea katika eneo hilo kwa miaka 12 sasa”.

Kanisa Kuu la Iskenderun limeanguka
Kanisa Kuu la Iskenderun limeanguka

Katika taarifa yao, wamebainisha kwamba “Tuko karibu na jumuiya Vikarieti ya  Iskenderun, ambapo iliona kanisa lake kuu likiharibiwa, lakini kwa bahati nzuri bila kulipa gharama katika maisha ya binadamu. Mawazo yetu yanaenda kwa Vicariati ya Anatolia, ambayo inakabiliwa na hali ngumu ya uharibifu. Kwa hiyo hebu tutazame Aleppo, mji ambao uliuawa kishahidi kwa vita huko Siria na ambao sasa unapitia mauaji haya zaidi ya kishahidi”.

Mtoto akijaribu kutafuta chochote ambacho kimebaki katika nyuma yao baada ya tetemeko
Mtoto akijaribu kutafuta chochote ambacho kimebaki katika nyuma yao baada ya tetemeko

Washiriki wa mkutano wa kibara huko Praga katika tamko lao aidha amebainisha kwamba “.Zaidi ya yote, mawazo na shukrani zetu zinakwenda kwa wale ambao kwa sasa wanaleta juhudi za usaidizi, katika hali ngumu sana, na joto la msimu wa baridi. Caritas yetu imejitolea kushughulikia dharura, kutibu majeruhi, kuwafariji waliopoteza wanafamilia, kutafuta paa kwa wale ambao hawana tena. Makanisa mahalia tayari yanatoa kila aina ya usaidizi na makaribisho, na ni mfano mzuri ambao tunautazama kwa kustaajabisha. Kwa hisia, Makanisa yaliyoko Ulaya hukusanyiji na ukaribu na watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi, wakifanya kwa upya maomo yao  na kutangaza kama sasa kila msaada unaowezekana kushughulikia dharura”.

Kardinali Mario Zenari wa Aleppo kati ya waliorundika kutokana na tetemeko huko Siria.
Kardinali Mario Zenari wa Aleppo kati ya waliorundika kutokana na tetemeko huko Siria.
08 February 2023, 11:58