Tafuta

2023.02.10 Mkutano wa Kibara huko Ulaya umehitimishwa kwa rasimu: mojawapo ya mapendekezo ni kurudia tukio kama hilo kila baada ya miaka 10 kwa maaskofu na Walei. 2023.02.10 Mkutano wa Kibara huko Ulaya umehitimishwa kwa rasimu: mojawapo ya mapendekezo ni kurudia tukio kama hilo kila baada ya miaka 10 kwa maaskofu na Walei. 

Sinodi:kupenda Kanisa la Ulaya na tunu mbili za utamaduni wa kilatino na mashariki

Wawakilishi 200 kutoka Nchi 45 za Ulaya wamekubali rasimu ya hati ya mwisho iliyoandikwa kwa kufuata maelekezo yaliyoibuka katika makabiliano.Kuna baadhi ya vipaumbele vinavyo hitaji jitihada katika mchakato unaoendelea kufanyiwa uzoefu kwa hatua zake.Pendekezo ni kurudia tukio hilo kila baada ya miaka 10 kwa kujumuisha maaskofu na walei.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Katika hitimisho la siku nne za kusikiliza na kujadiliana kwa kina kuanzia na Hati ya Kitendea Kazi ya awamu ya kibara katika umbu la Makanisa ambayo yamekuwa na wawakilishi wa Kanisa katika Mkutano wa  Sinodi ya awamu ya kibara, Ulaya, kuanzia tarehe 5 hadi 10 Februari 2023 ni upeo wa kutembea pamoja katika Kanisa. Kwa hiyo kwa kuhitimisha Mkutano huo umekubali rasimu ya ufupisho wa kazi ambayo hadi sasa imefanyika, katika utambuzi wa uzoefu wa kina wa kiroho, kwa njia ya mtindo wa kisinodi. Mkutano huo ulifanyika huko Praga katika Jamhuri ya nchi ya Czech ukiwa sambamba na ule wa  Australia katika visiwa vya Suva-Fiji(5-10 Februari 2023).

Kazi yenye shauku ambayo haikukosa mvutano na maswali

Zilikuwa ni siku za kina sana ambapo washiriki walijikita  kwa kina kua na  uelewa lakini bila kukosa mivutano na maswali ambayo kwa dhati Makanisa ya Ulaya yanapaswa yanakabiliana nayo. Hata hivyo kwa mujibu wao, mkutano huo umekuwa ni kazi ambayo wameifafanua kama tajiri na shauku, hata kama kiukweli shida na matatizo hayakukosekana lakini ambayo yaliruhusu kuwa na mtazamo wa macho ya  Kanisa ambalo ni Ulaya yenye  tunu zake mbili msingi za utamaduni  unaoundwa na kilatino na wa mashariki. Hii ina maana ya kwamba Barani Ulaya imeundwa na Makanisa katoliki ya liturujia za kilatino na pia liturujia za mashariki mwa Ulaya ambamo ni mchakanyiko wa makanisa mbali mbali yakiwemo ya lirurujia za kiorthodox, kigiriki, kiarmenia na mengine.

Kanisa linahisi uchungu na majeraha kuhusu nyanyaso

Katika rasimu hiyo inabainisha kwamba, kwa namna ya pekee mkutano huo ulihisi uchungu wa majeraha ambayo yanaikumba historia ya hivi karibuni, kuanzia na ile inayotesa Kanisa kwa sababu ya nyanyaso  za kijinsia zilizo jipenyeza kutoka kwa baadhi ya watu wanahudumia Kanisa hilo au kuwa na wajibu wa Kanisa, vile vile kuibuka kwa vurugu mbaya za vita vya uchokozi ambavyo vinamwaga damu huko Ukraine, na hatimaye janga la mwisho la tetemeko la ardhi kwa nchi za Uturuki na Siria.

Kuhusu majeraha yaliyojipenyeza, Kanisa linahitaji kuomba msamaha

Hati hiyo vile vile inabaninisha kwamba: “Kanisa letu ni zuri ambalo linabeba aina aina nyingi za uzuri huo ambao pia ni utajiri wetu. Na baada ya kuanzisha katika moyo wa Ulaya, aliyeshiriki anahisi kulipenda tena zaidi kwa kina licha ya majeraha yake, ambamo kuna haja ya kuomba msamaha ili kwezesha kufikia upatanisho, uponyaji wa kumbukumbu na mapkaribisho ya watu waliojeruhiwa. Mahali ambapo ni kupenda kwa kina Kanisa, lakini sio mtindo rahisi wa kihisia tu."

Inawezekana kukutana na kulipenda Kanisa katika aina zake zote

Hatua ya  Sinodi kwa hiyo imetambua kwamba "inawezekana kukutana, kusikilizana na mazungumzo kuanzia na tofauti na zaidi ya vikwazo vingi, kuta na vikwazo ambavyo historia yetu inaweka katika njia yetu." Walitambua haja ya kusaidiana katika kuheshimiana, kuimarishwa kwa imani katika Bwana na kwa uwezo wa Roho wake. Ahadi waliyofanya ni ile ya kuendelea kutembea katika mtindo wa sinodi, na kwamba si suala la kuwa na mbinu tu, lakini kuwa na  mtindo wa maisha ya Kanisa, wa utambuzi wa jumuiya na utambuzi wa alama za nyakati. Kwa hiyo imetafsiriwa katika shauku ya Mkutano wa  Bara kwamba isibakie kama uzoefu wa aina ya pekee tu, lakini iwe kwa hakika uteuzi wa mara kwa mara, kwa kuzingatia kupitishwa kwa jumla kwa mbinu ya sinodi ambayo inaeneza miundo na taratibu zao zote katika ngazi zote. Hivyo kwa pendekezo la kurudia mchakato kama huo kila baada ya miaka 10 wakijumuisha maaskofu na walei.

Sinodi ya kuwapatia  hadhi waamini wote wa Kanisa

Kuwasindikiza watu waliojeruhiwa, vipaumbele kwa vijana na wanawake, ufunguzi wa uwazi wa kujifunza kutoka kwa watu waliotengwa ni baadhi ya maeneo tu ambayo wao wameahidi kuyafanyia kazi kwa usahihi kwa kupitisha mtindo huo katika mtazamo wa kimisionari na sio kupuuza uekumene, majadiliano ya kidini, kwa  kubaki kupooza na woga, lakini  kwa kuchotoa nguvu ili kuendelea katika mchakato wa safari. Kujenga umoja katika utofauti, kuepuka majaribu ya umoja na kuwa wazi kwa kukubalika kama ushuhuda wa upendo usio na masharti wa Baba kwa watoto wake. Kwa hiyo wamesisitiza kuwa ndiyo mivutano miwili ya kuishi ili hema la Kanisa liweze kusimama. Kujenga Kanisa la Sinodi zaidi ni njia ya kutoa umuhimu kwa usawa katika hadhi ya washiriki wote wa Kanisa, walisisitiza.

Baadhi ya vipaumbele kwenye mtindo wa sinodi

Katika hati hiyo, hata hivyo baadhi ya vipaumbele vimeorodheshwa vya kuimarisha utendaji wa kitaalimungu  na maana ya sinodi. Lazima wagundue tena kitu ambacho ni cha zamani na ni cha asili ya Kanisa, na ni kipya kila wakati na wachukue hatua za kwanza mara moja. Baadaye kuna maana ya Kanisa linalohudumia kikamilifu, kushughulikia, kama upeo wa kuingiza tafakari juu ya karama na huduma (iliyo rasimi na isiyo rasimi)na juu ya mahusiano kati yao. Zaidi ya hayo, mtindo huo lazima uchunguzwe kwa ajili ya utekelezaji wa mamlaka ya sinodi, yaani, huduma ya usindikizaji wa jumuiya na ulinzi wa umoja, lakini vigezo vya utambuzi wa mchakato wa sinodi pia  lazima vinahitaji kufafanuliwa ni katika ngazi gani, kuanzia mahalia hadi kufikia maamuzi ya ulimwengu.

Wanawake, liturujia, malezi, utume, lugha, maskini

Na tena katika hati yao wamebainisha kwamba, lazima kuchukua maamuzi thabiti na ya ujasiri juu ya nafasi ya wanawake ndani ya Kanisa na juu ya ushiriki wao mkubwa katika ngazi zote, ikijumuisha katika kufanya maamuzi na kuchukua maamuzi hayo. Vile vile kwa kuzingatia mivutano inayozunguka Liturujia, ili kuelewa kimtazamo Ekaristi kama chanzo cha ushirika; kutunza malezi katika sinodi ya Watu wote wa Mungu, kwa kuzingatia hasa kupambanua alama za nyakati kwa mtazamo wa kutekeleza wa utume wa pamoja; kuvumbua hali hai ya utume, kushinda nyufa kati ya imani na tamaduni ili kwa mara nyingine tena kuleta Injili katika akili za watu,  wakati huo huo kwa kutafuta lugha inayoweza kueleza mapokeo na kusasisha, lakini zaidi ya yote kutembea pamoja na watu badala ya kuzungumzai juu yao au kwao.  Kwa njia hiyo hati hiyo ni yenye utajiri mkubwa ambayo hatimaye  inabainisha kwamba: “Roho anatutaka tusikilize kilio cha maskini na dunia katika Ulaya yetu hii, hasa kilio cha kukata tamaa cha wahanga wa vita wanaoomba amani ya haki”.

11 February 2023, 11:55