Tafuta

2023.02.14 Ufunguzi wa Mkutano wa Sinodi kibara kwa Makanisa ya Mashariki ya Kati,,12-18 Februari 2023. 2023.02.14 Ufunguzi wa Mkutano wa Sinodi kibara kwa Makanisa ya Mashariki ya Kati,,12-18 Februari 2023. 

Lebanon: mkutano wa Sinodi kwa makanisa ya katoliki ya Mashariki ya kati Feb.12-18

Katika eneo ambalo utamaduni wa sinodi ni wa zamani,wajumbe wa hatua ya kibara ya sinodi wanakutana huko Bethania-Harissa kuanzia 12 hadi 18 Februari.Historia ya watu wanaokabiliana na mipaka ya uhuru,ufisadi,ukosefu wa utulivu wa kisiasa na kijamii,inafungamana na shauku ya amani na umoja.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baada ya sala ya kuwaombea wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea Siria na Uturuki, Padre Khalid Alwan, katibu mkuu wa Baraza la Mababa wa Kanisa Katoliki Mashariki na mratibu mkuu wa Baraza la Sinodi ilifungua rasmi nchini Lebanon , katika hoteli ya Bethania-Harissa, kazi ya Baraza la Mabara kwa ajili ya Mashariki ya Kati, kwa kukumbuka kile walichokiita ramani ya barabara ya sinodi: barua ya mwaka 1992 ambayo Mababa wa Kanisa Katoliki la Mashariki walizungumza juu ya uwepo wa Wakristo katika Mashariki ya kati, kama ushuhuda na ujumbe, unaofumbatwa katika urithi wa Waarabu katika huduma ya mwanadamu bila ubaguzi au ubaguzi. Hayo tunayapata kutoka kwa wawakilishi wa Vatican News, Antonella Palermo na  Jean-Pierre Yammine waliko huko Bethania-Harissa,Lebanon katika Mkutano huo kuanzia tarehe 12 hadi 18 Februari 2023.

Mkutano wa mchakato wa Sinodi kwa upande wa Makanisa katoliki ya Mashariki ya Kati
Mkutano wa mchakato wa Sinodi kwa upande wa Makanisa katoliki ya Mashariki ya Kati

Uwepo wa Kikristo unategemea roho ya kiekumene

Kwa mujibu wa maelezo hayo, wamebainisha kwamba kuna uwepo wa Kikristo, unaotegemea roho ya kiekumene na mazungumzo ya kidini kwa ushirikiano wa pamoja. Katika siku hizo, Makanisa saba ya Kikatoliki yanakutana: ambao ni Wakopti, Wasiria, Wamaroni, Wamelkiti, Wakaldayo, Waarmenia na Walatino, ambao wametoka Nchi Takatifu, Yordani, Lebanon, Siria, Misri, Iraq na Armenia, ili kusikiliza kile ambacho Roho anasema kwa Makanisa  na kusali na kutafakari pamoja juu ya mahangaiko ya kawaida na kushiriki matarajio ya wakati ujao kwa tumaini lisilokatisha tamaa. “Mambo mengi yanatuunganisha, tunaunganishwa na hali ya nchi zetu, ambapo sote mara nyingi tunakosa uhuru wa imani, uhuru wa kujieleza, uhuru wa wanawake na watoto. Sote tunatafuta kulingana na nguvu zetu,  kupambana na rushwa katika siasa na uchumi.” Alisema.

Mkutano wa awamu ya kibara unaendelea kwa upande wa Makanisa ya Mashariki ya Kati
Mkutano wa awamu ya kibara unaendelea kwa upande wa Makanisa ya Mashariki ya Kati

Kutekeleza uraia inaowajibika

“Sote tunataka kutekeleza uwazi katika taasisi zetu za kidini na kijamii, na tunataka kutekeleza uraia unaowajibika na kupigana dhidi ya umaskini na ujinga. Sisi sote tunakabiliwa na uhamiaji wa watoto wetu, ambao upeo wa maisha ya heshima umepungua, na hivyo kupunguza maisha yetu. Hata hivyo, sisi watoto wa Kanisa, si tu kwamba tumeunganishwa na mahangaiko na shida za maisha, bali pia tunaunganishwa kwa ubatizo mmoja, imani moja, upendo mmoja na tumaini moja”. Padre Alwan alisisitiza utofauti wa semi za kiliturujia za Makanisa ya Mashariki lakini pia asili ya upeo wao wa kiroho na kitaalimungu, nguvu ya ushuhuda wao kwa karne nyingi, na mara nyingi hadi kifo cha kishahidi. Alizungumza juu ya utofauti katika Kanisa kama kipengele ambacho kimekuwa chanzo cha utajiri katika kiwango cha ulimwengu wote.Kwa bahati mbaya alielezea - ​​imegeuka kuwa mgawanyiko kutokana na dhambi za wanadamu na umbali wao kutoka kwa Roho wa Kristo. Hata hivyo, kile kinachotuunganisha ni muhimu zaidi kuliko kile kinachotutenganisha, na haituzuii kukutana na kushirikiana.

Viongozi wa makanisa Katoliki ya Mashariki ya Kati wanaendelea na mkutano hadi 18 Februari
Viongozi wa makanisa Katoliki ya Mashariki ya Kati wanaendelea na mkutano hadi 18 Februari

Wito, ushuhuda na majaliwa ni kitu kimoja

“Wito ni mmoja , ushuhuda ni mmoja na  majaliwa ni mamoja. Kwa hiyo Padre Khalid alisisitiza kuwa  “tunaitwa kufanya kazi pamoja, kwa njia na njia mbalimbali, ili kuunganisha mizizi ya waumini waliokabidhiwa kwetu, katika roho ya udugu na upendo, katika nyanja mbalimbali ambazo wema wa pamoja wa Wakristo wote unatusukuma.” Katika Mashariki, ama sisi ni Wakristo pamoja au si sisi, alieleza kwa kubainisha kwamba, ikiwa mahusiano kati ya Makanisa ya Mashariki hayajawa mazuri sikuzote kwa sababu nyingi za ndani na nje, basi wakati umefika wa kumtakasa Mkristo zile  kumbukumbu kutoka katika amana hasi za zamani. 

Mkutano wa kibara wa sinodi kwa makanisa ya Mashariki ya Kati unaendelea
Mkutano wa kibara wa sinodi kwa makanisa ya Mashariki ya Kati unaendelea

Kardinali Hollerich:Kutembea pamoja' ni dhana rahisi katika maneno,si katikamatendo

Kwa upande wa Kardinali Jean-Claude Hollerich, mratibu wa Mkutano Mkuu wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu, alisema jinsi alivyo na  heshima kubwa kuwepo Mashariki ya Kati, ambako sinodi ina utamaduni wa muda mrefu . “Ni shauku yangu kuiona na kujifunza kutoka kwao, aliongeza, akisisitiza pia jinsi ya  'kutembea pamoja' ni dhana ambayo ni rahisi kuiweka katika maneno, lakini si rahisi kuitekeleza. Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu wa Sinodi ya Maaskofu, alirudia tena, kama alivyokuwa amekwisha fanya katika Mkutano wa Ulaya huko Praga, na kwamba mazoezi ya Sinodi kamwe hayawaweki maaskofu na watu wa Mungu katika ushindani, bali huwaweka katika uhusiano wa kudumu, kuruhusu wote wawili kufanya kazi yao. “Kanisa la Sinodi ni Kanisa la kusikiliza”, alisema, akibainisha kwamba hilo haliwezi na halipaswi kupunguzwa kuwa maneno ya faragha. Ni uhakika wake  kwamba kupitia njia hiyo itawezekana kufanya maendeleo pia katika uekumene wa mazungumzo.

Mkutano wa awamu ya kibara unaendelea katika makanisa ya Mashariki ya Kati
Mkutano wa awamu ya kibara unaendelea katika makanisa ya Mashariki ya Kati

Kardinali Boutros: Kuwa Kanisa la Sinodi ni kumsikiliza Roho

Kardinali Mar Bechara Boutros Al-Rahi katika mahojiano na Vatican alikumbuka maandishi elekezi ya kazi hadi sasa, kwamba  Hati ya awamu ya bara, ambayo ni matokeo ya awamu ya kwanza ya mashauriano katika ngazi ya ndani. Patriaki wa Maroniti aliendelea kuonesha mada kuu mbili  za mchakato wa safari ya sinodi ambazo zinabainisha  ni kwa jinsi gani  safari hiyo ina kuwa ya pamoja ambayo inaruhusu Kanisa kutangaza Injili kulingana na ujumbe ambao umetolewa kwake, unaotekelezwa leo, ndani na kimataifa? Na baadaye ni hatua gani zaidi ambazo Roho Mtakatifu anahimiza kuchukua ili kukua kama Kanisa la sinodi? Kwa hiyo alisema  Si jambo tupu la kielimu, bali ni suala la kuhamasishwa na sala, na kwa kusikilizana, kufafanua vipaumbele ambavyo vitasomwa katika mkutano mkuu ujao.

14 February 2023, 16:40