Tanzania,Ask.Kilaini:Jumuiya ndogondogo ni msingi wa Kanisa kufanya kazi pamoja!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Hivi karibuni idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican ilifanya mahojiano maalum na Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Tanzania, katika fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kupata daraja la ukuhani mnamo mwaka 1972. Mjubilei huyo katika maelezo yake alijikita kufafanua juu ya shughuli za kichungaji kwa jimbo lake kwa ujumla kuanzia mapadre, wamisionari wachache walioko kwenye jimbo hilo na walei lakini pia hata kufafanua changamoto za uchungaji huo na hakusahau suala la utunzaji wa wazee. Katika mahojiano hayo Askofu Kilaini alionesha na kusema kuwa na furaha kuwa nasi ili kuweza kubadilishana juu ya masuala ya kichungaji, mambo ya Mungu na mambo ambayo yanawasaidia watu kuishi vema hapa duniani katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametuelekeza namna ya kuishi ili tuweze kufika kwake mbinguni.
Askofu Kilaini akianza kudadavua shughuli za kichungaji kwa kifupi ambazo wanahamasisha na wanakusudia kuzifanyia kazi wakati huu, alisema kwamba: Jimbo la Bukoba ukilinganisha na majimbo mengine ni kongwe, kwa sababu lilianza mnamo mwaka 1892, kwa namna hiyo ndipo ulianza uinjilishaji na hivyo kwa hakika watu wamekwisha hamasika kiasi cha kutosha. Katika jimbo la Bukoba asilimia ya wakatoliki ni zaidi ya 65 na wanakariba laki saba na kazi imekuwa ni nyingi na kubwa, lakini ni nzuri na katika wakristo hawa tunahamasisha kwa bahti nzuri tunatenda kazi zaidi na mapadre 150 wa jimbo na wamisonari mapadre wachache ambao ni kama saba hivi. Ingawa mapadre wengine tumewatuma nje, kwani wako katika mabaraza ya maaskofu, wako seminari mbali mbali za Taifa, wanafundisha, wengine hata nje ya nchi, lakini wengi bado wako ndani ya nchi na wote wanajitahidi katika kufanya kazi ya kuendeleza neno la Bwana.
Baba Askofu Kilaini alijikitia kutoa ufufanuzi pia kuhusu shughuli hiyo kwa wakristo hata wapya na kusema kwamba: Kazi kubwa tunayofanya hasa ni ya kuimarisha ukristo tulio nao. Ni kweli kabisa tunapaswa kupata na wale wapya, lakini wapya sio wengi, kwa sababu wengi ni wakatoliki na kama si wakatoliki, ni waprotestanti, na hasa waprotestanti waliopo hapa ni Waluteri ambao wanaweza kuwa kama asiliia 14-15 hivi na Waislamu ni wachache sana, hivyo tunachofanya sasa ni wale wakristo tulio nao, wakatoliki kuwahamasisha wabaki wakristo imara, ambao wanaendeleza dini yao kuanzia kwenye familia mpaka kwenye miundo mbinu mikubwa ya taifa, hasa ya jimbo zima. Na kwa kuanzia na familia ni sawa lakini hasa kitengo kikubwa tunachokisaidia ili kusaidia kwenda chini, kusaidia kwenda juu imekuwa ni Jumuiya Ndogo ndogo. Jumuiya Ndogo ndogo za Kikristo zimekuwa msingi tangi ilipopitishwa na AMECEA mnamo mwaka 1976, ikapitishwa rasmi kama kipaumbele cha uinjilishaji na Baraza la Maaskofu Tanzania mnamo 1977, hivyo ikawa kipaumbele cha Tanzania nzima. Lakini kwa namna ya pekee kama ilivyo mahali pengine hapa hapa Bukoba. Na hiyo ni kwamba kukiwa na Jumuiya Ndogo ndogo zilizo imara zinasaidia kuimarisha familia kiasi kwamba zamani walikuwapo ukoo. Familia ikipata matatizo inaingia kwenye ukoo wanasuluhisha. Sasa ukoo bado upo vijijini lakini sio imara kiasi hicho. Hivyo zinataka Jumuiya ndogo dogo sasa ziwe ndiyo ukoo mpya wa Kikristo, kiasi kwamba hata familia ikipata matatizo iweze kupata mahali pa kukimbilia, katika Jumuiya ndogo ndogo.
Jumuiya Ndogo ndogo kwa maana hiyo, sio tu kaketi na kusali na kuondoka, hapana, Jumuiya ndogo ndogo ziweze kuwa katika maisha ya kikristo yaani Jumuiya ndogo ndogo ni katika kuinjilisha, kuingiza maisha ya kikiristo katika maisha ya kila siku ya Binadamu na maisha ya kila siku ya binadamu anayeishi kule kijijini mwake, kitongoji, mtaa kama yuko mjini. Maisha haya yatawezekana kama anayeishi na wale watu ambao wanamjua, na yeye anawajua , anakula nao kila siku, watoto wake wanacheza na watoto wao na yeye anakwenda na kufanya shughuli mbali mbali za kijamii pamoja na watu hao. Na wanapozifanya, wanazifanya wakifikiria vile vile juu ya imani yao. Na ndiyo sababu tunasisitiza sana juu ya jumuiya Ndogo Ndogo na maisha juu ya Jumuiya Ndogo ndogo. Askofu Kilaini kwa kusisitizia zaidi juu ya Jumuiya ndogo ndogo alibainisha kuwa sio kwamba hatuzungumzii juu ya familia, juu ya watoto, juu ya vijana, lakini wote tunaongea nao, tunawasisitiza, kuanzia juu ya jumuiya ndogo ndogo kama Kanisa Msingi ambalo unaweza kuliunganisha kufanya kazi pamoja. Ni kweli familia ndio ina nia msingi lakini ni familia hiyo ya watu wa ndani. Na ndiyo maana tunaanzia katika jumuiya ndogo ndogo kabla ya kikango na kwenye parokia. Hiyo kiukweli mapadre wote wanasisitiza juu ya hilo, kwa sababu Jumuiya Ndogo ndogo inatusaidia kupata watoto wa kubatizwa katika vijiji, ndio inatusaidia kuona ni akina nani hawajafunga ndoa, lakini wanaishi pamoja ili kuweza kuwaelekeza waweze kufunga ndoa na ili padre anapokwenda wanamwelekeza ni wapi pa kutembelea familia, na jinsi ilivyo, wanakupatia kile kitu cha familia hiyo, hata unapokwenda unajua familia ile ikoje, imefikia wapi,na inasaidiwa hadi kiasi gani, na wewe inaweza kusaidiajie, hata wale wanaokuja kupata sakramenti nyingine, kama vile kumunio ya kwanza, kipaimara, wanajaza fomu na zinapitia katika Jumuiya Ndogo ndogo ili Jumuiya Ndogo Ndogo iweze kuwa hai na kazi ya kufanya na ndiyo kazi kubwa tunayofanya katika ngazi za msingi.
Uhamasishaji, kuongezeka kwa watu na upanuzi wa majengo ya Kanisa
Askofu Kilaini alielezea pia juu ya uhamasishaji, kuongezeka kwa watu na kupanua majengo mbali mbali kwamba: baada ya hapo katika ngazi ya juu, sehemu nyingi bado kuna ujenzi kwa sababu watu wanaongezeka na tunataka kupeleka imani, na ibada karibu na watu, hivyo watu wanajitahidi kujenga na kukata maparokia. Kutokana na kwamba tuna maparokia 44, lakini tunataka yaongezeke zaidi sana ili mtu aweze kwenda kwa urahisi kusali na hivyo ataweza kusali mara nyingi zaidi kuliko anavyosali sasa. Tukipata mapadre zaidi vile vile waweze kutengeneza sio tu vigango ili viweze kuwa parokia. Kwa maana hiyo kuna ujenzi mwingi sana unaofanyika katika sehemu mbali mbali, watu wanapata ardhi, wanaanza kujenga na unapojenga kitu kinachokuja kwa sasa sasa kwani, zamani wakati wamisionari, hata sisi mwanzoni tulikuwa tukipata misaada nyingi kutoka nje, maana tulikuwa tukiandika barua Roma, unapata ela, unaandika barua Ujerumani unapata ela na kweli bado wanatusaidia, lakini misaada imepungua sana na ni vema na haki kuwa hivyo. Kwa sababu na sisi baada ya miaka hiyo tujifunge kibwebwe na huo ndio uelewa wa watu ili waweze kulitegemeza Kanisa lao.
Waamini wanapaswa kuwajibika katika Kanisa lao
Askofu Kilaini amefafanua kwamba ili kuweza kufanya hivyo wanapaswa kuwa wamiliki wa Kanisa lao. Yaani ni kujua kwamba Kanisa hili ni la kwao. Kwa sababu kama hawajuhi kuwa Kanisa hilo ni la kwao wataliona Kanisa kama la padre na katekista na kumbe hapana! bali ni la kwao. Baada ya hapo ndipo zinaundwa Almashauri za Walei, kiasi kwamba wakristo kuanzia Jumuiya Ndogo ndogo wanachagua viongozi wao, nao pia wanachagua viongozi wa ngazi kubwa ambayo tunaita Jumuiya mama na Jumuiya mama zinakwenda kwenye kigango, kigango kinakwenda kwenye parokia ili kusudi mipango ifanyikayo iwe ni mipango yao, kama mnaamua parokia au mapadre wanakuwapo wasipange maana ya maendelea katika parokia bila kuhusisha hawa Almashauri ya Walei na wakiwahusisha wanapeleka habari kwa watu. Hata paroko akiondoka akaja mwingine wanachukuwa kilichoamliwa moja, mbili na tatu. Na hiyo inasaidia kuleta kujitegemeza kwa kuwa wanafanya kitu ambacho wanakielewa , wananasaidia kuamua na kusaidia kufanya mipango na kutoa ripoti katika kile kinachofanyika kama vile ripoti za fedha na kila kitu. Inasaidia kidogo ili watu wajue ukweli na kwamba mapadre ni watumishi, sio watu wa kutoa maagizo ya fanya hili na lile katika Kanisa.
Kila mmoja ajue wajibu wake
Mapadre wanajua mambo ya dini mfano Teolojia na hapo kwa mfano waamini hawawezi kuwambia kwamba waoe wake wengi na padre akakubali, hapana! Lakini mambo ya maendeleo tujenge Kanisa tujenge kigango, tuanzishe banki za Kanisa, na je nyumba ya mapadre tuisaidieje, tuiendelezeje, hata mapadre watakula nini, na wasaidie kujua mapadre wataishijie, petroli itapatikana wapi. Hii iwasaidie sana kwa watu kushika hatumu ya maendeleo ya Parokia zao. Askofu Milaini alitibitishwa kwamba hata hivyo hiyo imefanuka na ido maana katika jimbo limeweka mwongozi wa fedha kusudi fedha za parokia ziweze kueleekwa zinazoingia na kutoka zinakwendaje na kuwa na mpangilio, fedha za Jumapili ziandikwe n asio Paroki tu ajue zimefika fedha kiasi gani kwa kutoa mkono wa kuume na wa kushoto bila kujua.