Tafuta

2022.08.17 Miaka 50  tangu kupewa upadre Askofu M.Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo katoliki la Bukoba Tanzania 2022.08.17 Miaka 50 tangu kupewa upadre Askofu M.Kilaini, Askofu Msaidizi wa Jimbo katoliki la Bukoba Tanzania 

Ask.Kilaini:Wazee ni tunu msingi tuwahudumie na kuwatunza!

Wazee wajiandalie uzee wao,wakati huo huo na watoto wao wawasaidie ipasavyo na kuwajali kwa kukumbuka tunu msingi ambayo waliipokea kutoka kwa wazazi wao.Ni ushauri kutoka kwa Askofu Kilaini,Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba Tanzania,wakati wa mahojiano maalum na Vatican News,akiwa katika fursa ya Jubilei ya miaka 50 tangu kupewa daraja la ukuhani.

Na Angella Rwezaula –Vatican.

Askofu Methodius Kilaini, Askofu Msadizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Tanzania akizungumza katika mahojiano maalumu na Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican, hivi karibuni aligusia masuala mengi ya kichungaji kuanza na utume wa makuhani , wamsionari, watawa na waamini wale. Katika mazungumzo marefu alizingumzia juu ya vyama vya kitume kama vile Wawata, TYCS, Utoto Mtakatifu na vile vile UWAKA katika jimbo lake jinis vinavyotenda utume wake mafanikio na changamoto. Katika sehemu hii Baba Askofu anajikita na  suala la wazee katika kuenzi wito wa Baba Mtakatifu Francisko na ambaye hasa sasa Katekesi zake ni mwendelezo wa mada hiyo ya uzee. Kwa upande wake  Askofu Kilaini alisema kuwa karibu kila Jumapili anatoa tafakari moja inayorushwa na moja kwa moja na Radio Maria Tanzania.

Wazee wanahitaji kuhudumiwa  katika uzee wao
Wazee wanahitaji kuhudumiwa katika uzee wao

Baba Askofu Kilaini kwa njia hiyo  amekiri ni kwa jinsi gani  alipoianzisha alipata watu wengi sana kuhusiana na mada hiyo na walio wengi sana walijibu suala hili. Baba Mtakatifu Francisko alizungumzia na anaendelea kuzungumzia juu ya wazee katika Katekesi zake na jinsi  ya kuwatunza kwa maana hiyo Askofu Kilaini alisisitiza kwamba hata wazee wapasaw kujitayarisha kupokea uzee wao. Hiki ni kitu kizuri na katika jamii  za kiafrika hadi leo hii wazee wengi bado wanatunzwa. Hata hivyo Askofu alisema kwamba tofauti na watoto ambao labda hawana uwezo, lakini kwa ujumla wenye uwezo wawatunza wazee wao. Hata wale ambao wanakwenda mjini, wazazi wao wakiugua, wanapelekwa ili kuwatunza huko japokuwa kuna utofauti kwa sababu  wazee wengi hawapendi kwenda mijini, kwa kuwa maisha yao yote waliishi kijijini na masuala ya kubaki ndani na mtu wa kazi wakati watoto wao wako kazini inawapelekea kuhisi upweke tofauti na ambavyo angekuwa  kujijini. Kwa njia hiyo Askofu Kilaini amehamasisha watoto waweze kuwatunza wazazi wao nyumbani kwao, kwa kuwafikishia mahitaji na hata huduma za kiafya ili wabaki katika mazingira waliyozoea bila kuwaondoa mahali pao.

Wazee wanahitaji kuhudumiwa  katika uzee wao
Wazee wanahitaji kuhudumiwa katika uzee wao

Askofu Kilaini akiendelea na hoja hiyo ya uzeee aliwaomba hata na wazee kujua jinsi ya kujitayarisha kwa ajili ya uzee. “Zamani alisema walikuwa wanazaa watoto wengi wakifikiri ndio watapata wa kuwatunza lakini wazee wakumbuke kuwa sio kila mara watoto wanaweza kufanya hivyo. Kwa maana hiyo wazeee kwa kile kidogo wanachokipata wakitunze kwa ajili ya uzee wao”, alisisitiza Askofu Kilaini. Wazee nao Baba Askofu alisema  wapokee hali yao ya kuzeeka, maana alimema kwamba mara nyingi wazee hawataki kukubaliana na uzee na wanataka kubaki kama vijana kwa kufanya kile ambacho walizoea wakiwa bado na nguvu zao,  utakuta wanatoa masharti, wanatukana watoto, bila kujua kwamba wamezeeka na sasa wanahitaji msaada wa kutunzwa na sio kutoa masharti.

Wazee wanahitaji kuhudumiwa  katika uzee wao
Wazee wanahitaji kuhudumiwa katika uzee wao

Askofu Kilaini vile vile hakukosa kutoa ushauri kwa watoto ambao wana tabia ya kupenda urithi badala ya kiandalia maisha yao ya baadaye  kwamba: “Kila mtoto aliyepata elimu imsaidie kujitengemea na ili kumwachia mzee mali yake. Badala ya kusubiri urithi wa baba utafilizika. Kila mtoto atengeneze vyake, na vile vya baba kumwachia abaki navyo hadi anakufa  vizuri na wewe umsaide tena”, alisisitiza Askofu. Kwa kuhitimisha mahojiano hayo  na Vatican News, Kiongozi huyo wa Jimbo La Bukoba Tanzania, alitoa ushauri  kwa wote  hasa kwa makuhani vijana akiwa katika mwaka wake wa 50 tangu apewe daraja la ukuhani mnamo  1972 kwamba “ Ukimpenda mwenyezi Mungu ukajitoa kiukweli hata mara moja hatakuacha nyuma. La muhimu ni kuwepo kila mahai pa kazi yoyote unayoifanya na  iwekwe mikononi mwa Mungu na utaweza kufakiwa”. Askofu Kilaini akiwa anaadhimisha njubilei hiyo kwa shangwe kuu alisema kwamba pamoja na mambo mengi mazuri na mema aliyopata, lakini hata changamoto hasikukosekana zakiafya na kila hali, lakini zote hizo kwa kuziweka kwa mwenyezi Mungu ni ushindi. Na ndiyo  lilikuwa jambo la mwisho alilopenda kumweleza kila mmoja hasa mapadre vijana kwamba: “ Kujitoa kabisa bila kutegemea chochote na popote pale atakapowekwa padre achimbe na atapata dhahabu”.

Askofu Kilaini azungumzia juu ya wazee na kushauri watoto wao kuwatunza

 

18 August 2022, 10:03