Tafuta

2022.06.27 Padre Christopher Odia aliyeuawa nchini Nigeria 2022.06.27 Padre Christopher Odia aliyeuawa nchini Nigeria 

Nigeria:mapadre wawili katoliki wameuawa

Mamia ya Wanigeria ni waathirika wa kutekwa nyara na magaidi na wote bila kuadhibiwa."Ikiwa kuna amani nchini,wale walio na kazi ya kutangaza Injili,kama sisi,wana nafasi ya kufanya hivyo.Lakini hakuna amani na usalama,kama inavyotokea sasa,kazi yetu ni ngumu,imezuiwa na ukweli kwamba hatuwezi kuzunguka kwa uhuru".Ni maneno askofu mkuu wa Kaduna na kwamba hiyo ni hali mbaya wanayoishi leo nchini Nigeria.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mbele ya msururu wa umwagaji damu unaoikumba nchi ya Bara la Afrika  na hasa Kanisa Katoliki nchini Nigeria Padre Patrick Alumuku, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Kijamii wa Jimbo Kuu la Abuja na Mkurugenzi wa Televisheni ya Taifa ya Kikatoliki ya Nigeria amesema: “Kama mapadre, haturudi nyuma, hatuogopi: tumejitayarisha kuwa mashahidi, kwa sababu ni kwa damu ya kifo cha imani ndipo Kanisa la Nigeria litakua”. Makasisi wengine wawili waliuawa mwishoni wa Juma lililopita katika jimbo la kusini la Edo na katika jimbo la kaskazini la kati la Kaduna, juma chache baada ya mauaji ya Mtakatifu  Francis wa  Xavier huko Owo, katika jimbo la kusini magharibi mwa Ondo.

Padre Stephano Ojapa ,MSP na Padre Oliver Okpara
Padre Stephano Ojapa ,MSP na Padre Oliver Okpara

Habari ya kipee iliyoinua kidogo roho za waamini ni  kuhusu Padre Stephen Ojapa na Padre Oliver Okpara, makasisi waliotekwa nyara siku ya Jumamosi katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa nchi. Na katika  jimbo la Edo, Padre Christopher Odia, 41, aliyetekwa nyara katika Kanisa la Mtakatifu  Michaeli, Ikabigbo, Uzairue, alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya kuadhimisha misa. Kasisi huyo aliuawa baadaye na washambuliaji wake, kwa taarifa kutoka kwa Kanisa la eneo hilo ilieleza. Jumamosi 25 Juni Padre Vitus Borogo, padre wa Jimbo kuu la Kaduna, badala yake aliuawa katika Shamba la Magereza, kando ya Barabara ya Kaduna-Kachia, baada ya kuvamiwa na magaidi, alisema  Padre Alumuku, kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari na vyanzo vya habari, na Dhirika la Kipapa la Makanisa Hitaji.

Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Matthew Man-Oso Ndagoso, askofu mkuu wa Kaduna, amebainisha juu ya  watu wengi wengi wa Kanisa  waliouawa katika nchi hiyo ya Kiafrika kwamba: “ni jukumu la serikali kumlinda kila Mnigeria. Ni jambo baya sana. Kanisa limehuzunishwa, lakini si hilo tu: Wanaigeria wote wanahuzunishwa na kile kinachotokea. Watu hawajisikii salama majumbani mwao, barabarani, na mahali popote wanapokuwa”. Aidha Askofu Mkuu wa Kaduna alisisitiza kwamba “Mamia ya Wanigeria ni waathrika wa wateka nyara na magaidi na wote bila kuadhibiwa. Ikiwa kuna amani nchini, wale walio na kazi ya kutangaza Injili, kama sisi, wana nafasi ya kufanya hivyo; ambapo hakuna amani na usalama, kama inavyotokea sasa, kazi yetu ni ngumu, imezuiwa na ukweli kwamba hatuwezi kuzunguka kwa uhuru: hiini hali mbaya tunayoishi leo nchini Nigeria”.

Kwa mujibu wa maelezo ya Mkuu wa  mawasiliano ya kijamii ya Jimbo kuu la Abuja alisema Kasisi huyo,  mwenye umri wa miaka 50, alikuwepo akiwa na watu wawili, kaka yake na mvulana mwingine, ambao wakati huo walitekwa nyara na watu wenye silaha. Padre Alumuku alimfahamu Padre Vitus, alikuwa mwanafunzi wake wakati alipokuwa mkuu wa seminari ya Mtakatifu Yakobo, jimbo la Makurdi, huko  Benue. “Alikuwa mvulana mzuri ba mwema sana. Nilikutana naye hivi majuzi, miezi michache iliyopita huko Kaduna. Kama kasisi wa Chuo Kikuu cha Jimbo la Kaduna, aliwaongoza wanafunzi Wakatoliki wa Chuo Kikuu hicho kwa imani, kuwa ishara chanya katika jamii ya mahali hapo”.

Eneo la Kaduna ni moja wapo ya wachungaji walioathirika zaidi na wachungaji wa Kifulani, alifafanua Padre huyo, akimaanisha kabila la kuhamahama la Afrika Magharibi, lililoenea kutoka Mauritania hadi Cameroon, mara nyingi katika mapambano ya umwagaji damu na watu wanaokaa katika kilimo, kwa muktadha wa jumla wa ukosefu wa usalama unaotokana na ghasia za athari mbalimbali za itikadi kali za Kiislamu za Boko Haram. Padre Alumuku amezungumzia mtafaruku wa kijihadi nchini, katika hali ambayo Kanisa Katoliki ni  walengwa kwa urahisi kwa imani yao ya Kikristo. Kwa mujibu wake alisema “ sisi hatupigani na mtu yeyote, na hatuna silaha. Kuhubiri upendo katika hali hizi ni vigumu, lakini pia ilikuwa vigumu wakati wa Yesu. Tuna matumaini kwamba ghasia hizi zote zitakwisha, wakati tunatarajia uchaguzi wa urais wa 2023”.

Askofu Mkuu Mathew Ndagoso wa Kaduna nchini Nigeria
Askofu Mkuu Mathew Ndagoso wa Kaduna nchini Nigeria

Kwa niaba ya Signis Nigeria, hali halisi ya ndani ya Chama katoliki cha Mawasiliano Duniani, ambacho Padre Alumuku ni rais wa Abuja, ametoa ushuri kwa  vyombo vya usalama katika ngazi ya shirikisho na serikali kuongeza juhudi zao za kuwafikisha wauaji mbele ya sheria na  wakati huo huo kuzidisha dhamira ya kulinda maisha ya raia wote.

27 June 2022, 15:31