Tafuta

Injili inasema kwamba «hatimaye yule mfuasi mwingine, aliyetangulia kufika kaburini, naye akaingia ndani. Aliona na kuamini” (Yn 20:8). Injili inasema kwamba «hatimaye yule mfuasi mwingine, aliyetangulia kufika kaburini, naye akaingia ndani. Aliona na kuamini” (Yn 20:8).  

Pasaka ya Bwana: Kuona, Kuamini, Kutangaza na Kushuhudia Injili

Mtakatifu Petro alipofika aliinga moja kwa moja kaburini na baadaye yule aliyetangulia kufika naye akaingia kushuhudia. Injili inasema kwamba «hatimaye yule mfuasi mwingine, aliyetangulia kufika kaburini, naye akaingia ndani. Aliona na kuamini” (Yn 20:8) Waamini wanaitwa na kutumwa kutangaza na kushuhudia imani yao kwa Kristo Yesu aliyeteswa, akafa na kufufuka kwa wafu.

Na Padre Efrem Msigala, OSA, - Roma.

Karibu mpendwa msikilizaji na msomaji wa Radio Vatican na Msomaji wa Vatican News katika tafakari ya Masomo ya Dominika ya Pasaka, Ufufuko wa Bwana wetu Yesu Kristo. Hebu tufikirie kwa muda athari ambayo jambo kama hilo lingetokea katika nyakati zetu, ikiwa tungejua kwamba rafiki au jamaa yetu, kutoka jiji letu au mji au kijiji chetu na hata katika jumuiya yetu baada ya siku tatu za kuzikwa, ghafla aonekane hai, amebomoa kaburi katoka. Na kuonekana kwa familia yake na marafiki, kwa wale walioomboleza au wanaoomboleza kuondoka kwake na ambao wanajua kweli kwamba amekufa, ambao walimzika. Wengine wangekufa kwa hofu, wengine wangezimia wakiamini wanaona mzimu, wengine wangelia kwa hisia na kupigwa na butwaa. Bila shaka, zingekuwa habari kuu ambazo zingechukua kurasa za mbele za magazeti na habari za televisheni ingekuwa ndiyo habari yenye kuvuta hisia za watu. Kutoka nchi nyingi wangefika mahali hapo kuhojiana naye na kuripoti habari hiyo kuu. Mitandao ya kijamii ingejazwa na picha za pamoja za tukio hilo la ajabu na hata kufanya “selfi”. Ilikuweka kumbukumbu ya kudumu. Ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote wangekusanyika karibu naye ili kumgusa na kuzungumza naye, kumuuliza maswali na kukidhi udadisi wao ni vyema na haki kabisa.

Wanafunzi wake wakaona, wakaamini, wakatangaza na kushuhudia Injili.
Wanafunzi wake wakaona, wakaamini, wakatangaza na kushuhudia Injili.

Hisia hizo ndizo ziliwajaza Wakristo wa kwanza na zinapaswa kutujaza sasa, kwa sababu ni habari kuu inayotuweka na imani na matumaini kwamba sisi pia tutafufuka pamoja na Kristo. Na ni kwamba kama Kristo hangefufuka hakuna ambaye angeweza kufufuka tena; kifo kingekuwa mmiliki kamili wa hatima ya watu wote. Kama Kristo hangefufuka kusingekuwa na wakati ujao kwa yeyote. Kifo kingekuwa mwisho na mwisho. Mauti imeshindwa kwa ufufuo wa Kristo. Kwa sababu Kristo alikufa, lakini hakubaki kaburini: alivunja mzunguko wake mbaya na kufungua hatima nyingine kwa wanadamu. Ikiwa tunakosa imani katika Ufufuo wa Kristo, kila kitu kinasimamaIkiwa Kristo hangefufuka, matunda ya kuhubiri yangekuwa bure, wakati ungepotea bure. Lakini alifufuka, na ndiyo sababu tupo na furaha, tukiwa na tumaini! Na ndio maana Ukristo bado unasimama. Na ndiyo maana Kanisa letu Takatifu, Katoliki na la Mitume baada ya miaka zaidi ya 2000, linaendelea kusonga mbele, likiwa na imani thabiti kwamba siku moja sote tutafufuka tena pamoja na Kristo. Ndiyo maana pia Mtakatifu Paulo katika somo la pili la leo anatuambia: “Ikiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu (1Kor.15:20).

Mpendwa msikilizaji: Wainjili wote wanne wanatuambia kwamba kaburi tupu au li wazi, la Yesu liligunduliwa kwanza na wanawake. Mwinjili (Mt. 28:1-2) anasema “Maria Magdalena na yule Maria mwingine walienda kaburini asubuhi na mapema siku ya kwanza ya Juma, wakakuta kaburi li wazi...”(Mk.16:1-4baada ya sabato kuisha Maria Magdalena, Maria mama wa Yakobo na Salome walienda asubuhi mapema... walipofika kaburini wakakuta jiwe limetolewa na kaburi li wazi” (Lk. 24:) “wanawake walienda asubuhi na mapema kaburini siku ya kwanza ya Juma, wakakuta jiwe limetolewa kwenye kaburi, walipoingia hawakuona kitu. Yn.20:1 “Siku ya kwanza ya Juma Maria Magdalena alienda asubuhi na mapema akakuta kaburi liko wazi...” Katika jamii ya Kiyahudi ya karne ya kwanza wanawake hawakuweza kuwa mashahidi wa kisheria. Hivyo ilikuwa vigumu kuaminika kwa kila walichosema cha kisheria. Mwinjili Yohane, mwanamke pekee aliyeenda kaburini asubuhi na mapema ni Mariamu Magdala. Huyu akakuta kaburi lipo tupu. Lakini pia Injili ya Yohane sehemu ya mwanzo katika tukio la Maria Magdalena kuona kaburi wazi, haielezi kuonekana kwa malaika kwenye kaburi. Badala yake, inasemekana kwamba Maria aliona kwamba jiwe lililokuwa limeziba kaburi lilikuwa limeondolewa, naye alikimbia kuwaambia Simoni Petro na mwanafunzi mwingine aliyependwa na Yesu yaani Yohane akasema: “wamemwondoa Bwana kaburini hatujui walikomweka(Yn 20:1-2). Kauli yake kwao inawaambia. Anafikiri kwamba mwili wa Yesu umetolewa, labda umeibiwa. Hafikiri kwamba Yesu amefufuka kutoka kwa wafu.

Ufufuko wa Kristo Yesu ni kiini cha imani ya Kanisa.
Ufufuko wa Kristo Yesu ni kiini cha imani ya Kanisa.

Wale wafuasi wawili Petro na Mwanafunzi mwingine aliyependwa na Bwana yaani Yohane, walipoambiwa kuwa kaburi lipo wazi na hawajui Bwana yuko wapi walifunga safari na kwenda kwa mwendo kasi na aliyetangulia kufika ni yule Mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda alikuwa kijana na baadaye akafika Petro. Petro alipofika aliinga moja kwa moja kaburini  na baadaye yule aliyetangulia kufika naye akaingia kushuhudia. Injili yasema kwamba «hatimaye yule mfuasi mwingine, aliyetangulia kufika kaburini, naye akaingia ndani. Aliona na kuamini” (Yn 20:8). Kupitia imani yake anatambua kwamba utupu na vitambaa vya kitani vilivyolala chini na leso iliyokunjwa mahali pake, vyote hivyo ilikuwa ishara kwamba Mungu alikuwa hapo, ishara za maisha mapya. Na kwamba hajaibiwa bali amefufuka. Injili inasema pia: "Mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda" (Yn 20:2) aliongozwa na upendo aliopokea kutoka kwa Kristo. "Kuona na kuamini" hata hivyo, kwamba hata baada ya kuona kaburi tupu na vitambaa vya kuzikia, wanafunzi bado hawakuelewa kuhusu Ufufuo. Katika aya zinazofuata Maria Magdalena anakutana na Yesu lakini hatambui mapema kuwa ni Yesu kwani alifikiri ni mtunza bustani, ila baada ya mazunguzo anatambua kuwa ni Yesu (Yn.20:11-18).

Ndipo baadaye anatambua na baada ya hapo alienda kuwajulisha habari hiyo njema kwa wanafunzi wake. Hivyo wanawake wameshiriki kwa namna ya pekee kutangaza habari njema yaa Ufufuko wa Yesu Kristo. Hivyo basi imani yetu ya Pasaka inategemea ushuhuda wao kwa kaburi wazi, ushuhuda wa Maria Magdalena kukutana na Yesu, ushuhuda wa Mitume kukutana naye baada ya ufufuko na kula mbele yao (Yn.21:12-13). Ushuhuda wa wale wafuasi wa Emmau (Lk.24:13-35), na uhusiano wao endelevu na Yesu katika kuonekana kwake kwa nafasi mbalimbali kwa mfano “Alipowatokea wanafunzi na milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi (Yn.20:19-29). Tuishi Pasaka hii kwa furaha tele. Kristo amefufuka: basi tusherehekee kwa furaha na upendo. Mauti, dhambi na huzuni, leo vimeshindwa na Yesu Kristo… na amefungua milango ya maisha mapya, maisha halisi, maisha tunayopaswa kuyaishi kwa neema ya Roho Mtakatifu. Ishara kuu ambayo Injili inatupa leo ni kwamba kaburi la Yesu ni tupu. Hatupaswi kuangalia tena kati ya wafu kwa maana Yeye aliye hai amefufuka. Na wanafunzi wake, ambao baadaye watamwona amefufuka, yaani, walimwona akiwa hai katika kukutana naye kwa nafasi tofauti. Basi maisha yake yatuhuishe na tufanye upya neema ya Ubatizo tuliopokea. Tuwe mitume na wanafunzi wake. Tuongozwe na upendo na tutangaze kwa furaha yetu yote kumwamini Kristo. Tuwe mashahidi wenye matumaini ya Ufufuo wake.

Pasaka kuona na kuamini

 

16 April 2022, 10:10