Tafuta

2022.03.25. Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Tanzania 2022.03.25. Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Tanzania 

Tanzania,Askofu Mkuu Nyaisonga:Maria daima ni msaada dhidi ya mabalaa

Migogoro mingi inatokana na kukosa kufuata mapenzi ya Mungu.Ndiyo maana wanafikia ukatili na unyama ambao unakuta chanzo kikubwa kinatokana na mtu mmoja au watu kadhaa waliochonganisha na kusababisha mateso kwa wanadamu.Amesema hayo Askofu Mkuu Nyaisongo wa Mbeya,wakati wa misa ya siku kuu ya Kupashwa Habari Maria sambamba na kuziweka wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria,Ukraine na Urusi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 25 Machi 2022 ambapo Mama Kanisa alikuwa anaadhimisha siku kuu ya Kupashwa Habari Mama Bikira Maria kuwa Mama wa Mungu, ilikuwa pia ni siku Maalum ambayo Papa Francisko alipendelea na kutoa mwaliko kwa watu wote wa Mungu na wenye mapenzi mema ulimwenguni kuungana naye katika kusali kwa ajili ya Amani, wakati wa kiziweka wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria nchi ya Ukraine na Urussi. Kwa hakika siku hiyo kuanzia madhabahu madogo hadi makubwa, makanisa madogo, hadi makubwa, kwa kuongozwa na maaskofu wao, waliweza kufanya tendo hilo hilo katika ibada ya misa Takatifu. Baba Mtakatifu Francisko alifanya tendo la kuweka wakfu, mara baada ya sakrementi ya kitubio, kuungama yeye na kuungamisha baadhi ya waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican. Na huko Fatima, nchini Ureno, Papa aliwakilishwa na Kardinali Konrad Krajewski, Msimamizi wa Sadaka ya Kitume Vatican katika madhabahu hiyo maarufu duniani kwa maombezi ya Bikira Maria.

Misa ya Siku Kuu  ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria
Misa ya Siku Kuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria

Katika Jimbo kuu katoliki la Mbeya, Tanzania, Askofu Mkuu Gervas J. Nyaisonga ambaye pia ni rais wa Baraza la Maaskofu nchini Tanzania (TEC) akiwa katika hitimisho la Kongamano la Mapadre wazee wa Jimbo Kuu katoliki la Mbeya, aliadhimisha Misa Takatifu, ambapo katika mahubiri yake na kuhusu tendo la kuweka wakfu alisema: “Kwa namna ya pekee leo hii tunafurahi na Kanisa zima katika kusherehekea fumbo kubwa la Bikira Maria Kupashwa Habari ya kumzaa  Bwane wetu Yesu Kristo”. Akiendelea alisema, wanapotafakari juu ya wito wao kama kuhani, kuna mafumbo ambayo wanaweza kuwagusa wao katika upadre wao, yanayohusiana na siku kuu hiyo. Akikumbuka somo la siku hiyo alisema awali ya yote “Wayahudi waliambiwa watake ishara, lakini walisita, hawakujua ishara gani hiyo na ina lengo gani.  Lakini ishara yenyewe ilikuwa wazi: kwamba atazaliwa mtoto Emanueli, Mungu mtu, ambaye atakuwa ishara wazi ya Mungu anayetaka kukaa katikati ya watu wake”. Askofu Mkuu Nyaisonga akitaka kufafanua zaidi alikumbusha maneno ya Mtakatifu Leo Mkuu kwamba analeza vizuri kuhusu fumbo hilo la Mtu kweli na Mungu Kweli: “Huyu Mtu ukweli wa utu wake alizaliwa na mwili ambao ni (original) yaani ‘asili”.

“Haya yote yalifanyika ili kwamba, kama ilivyokuwa wakati wa wokovu wetu, mpatanishi mmoja wa pekee kati ya Mungu na wanadamu, mwanadamu Kristo Yesu, ambaye aliepushwa na kifo kwa upande mmoja, alitiishwa kwa upande mwingine. Kweli, fungamani na kamilifu ilikuwa asili ambayo Mungu alizaliwa, lakini wakati huo huo ni kweli na kamilifu alikuwa asili ya kimungu ambamo anakaa bila kubadilika. Ndani yake kuna umungu wake wote na ubinadamu wetu wote. Kwa asili yetu tunamaanisha ile iliyoumbwa na Mungu hapo mwanzo na kuchukuliwa, ili aweze kukomboa kutokana na Neno. Kwa upande mwingine, hakukuwa na dalili katika Mwokozi wa uovu ule ambao mdanganyifu aliuleta ulimwenguni na ambao ulikubaliwa na mtu aliyerubuniwa. Hakika alitaka kuchukua udhaifu wetu, lakini si kushiriki dhambi zetu. Alijitwalia hadhi ya mtumwa, lakini bila kuchafuliwa na dhambi. Alipunguza ubinadamu, lakini hakupunguza umungu. Kuangamizwa kwake kulifanya aonekane asiyeonekana na mwenye kufa, muumba na bwana wa vitu vyote. Lakini hiyo yote ilikuwa afadhali kujishusha chini kwa huruma kuelekea taabu yetu kuliko kupoteza uwezo wake na utawala. Alikuwa muumbaji wa mwanadamu katika hali ya umungu na mwanadamu katika hali ya mtumwa. Huyu alikuwa ni Mwokozi yule yule”. (Barua ya Mtakatifu Leo Mkuu Papa kwa Flaviano, 3-4; Pl. 54,763-767, ‘Fumbo la upatanisho wetu’).

Askofu Mkuu Nyaisonga alisema, kwa maana hiyo sio mwili ule uliojeruhiwa na dhambi ya Adamu na Eva.  Mwili wa Yesu kwa hiyo haukuwa na doa kama vile mabaya yatokanayo na ibilisi aliyoingiza katika asili ya mwanadamu. Askofu Mkuu alisisitiza kwamba ndiyo maana tendo la uwilisho wa Kristo, tendo la kutangazwa hali ya mwanadamu, hakika mwanadamu huyo anapaswa kujivunia hilo.  Akiwageukia Mapadre wazee ambao wamefanya uzoefu wa muda mrefu wa kikuhani katika utume wao, amesema wanaguswa sana hasa kwa kushiriki katika kudhihirisha ishara ambayo ina hadi halisi ya ishara bila kusita sita kuiomba.

Misa ya Siku Kuu  ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria
Misa ya Siku Kuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria

Katika huduma yao ya kikuhani, wao wanafanya Mungu awe katikati ya watu wao, wanapokea jukumu, la kumjengea Mungu nyumba. Kwa maana hiyo ni kufanya mwendelezo ule wa ufalme wa milele wa Kristo kwa sababu ni Kristo mwingine. Padre mwingine, “Alter Christus”,  “another Christ”, kwa kuwa wao wanaendeleza uwepo wake Kristo , wanashiriki kiti cha kifalme, kile cha milele hapa duniani na wanakuwa ishra iliyo wazi ya ufalme unaodumu kati kati ya watu. Kwa njia hiyo wao moja kwa moja wanashiriki kujenga nyumba ya Milele ya Mungu, alibanisha Askofu Mkuu Nyaisonga. Na hiyo ndiyo fursa kubwa waliyo nayo, nafasi kubwa ambayo imetokana na kusudio la Mungu na kudhihirishwa wazi wazi na mwitikio wa Bikira Maria na kuendeleza nafasi yao kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

Askofu Mkuu  Nyaisonga alisema lakini  jambo kubwa ni lile la kukubali mapenzi  ya Mungu na ndiyo siri ilipo. Alitoa mfano rahisi kuhusu mapenzi hayo hasa kwa kutenda kwa niaba ya… kwa jina la …  kwa mfano viongozi wa raia wanapowakilisha rais, kwamba hata katika salamu zao, lazima waseme wametumwa “kwa niaba ya rais,  wanatoa salamu kwa niaba ya raisi…. Na sio kwa jina lao, maana inaweza kuwa kitu kingine, na wanaweza kukosa nafasi hiyo. Kutokana na hilo pia ndiyo na zaidi nahusu makuhani wanapotenda kila kitu kwa jina la Bwana, (Baba, Mwana na Roho Mtakatifu….) na si kwa jina lao na ndiyo wanaweza kutimiza mapenzi ya Mungu.

Misa ya Siku Kuu  ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria
Misa ya Siku Kuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria

Hatimaye akizungumzia juu ya mgogoro alithibitisha kwamba umetokana na kukosekana kufuata mapenzi ya Mungu na ndiyo maana wanafikia ukatili na unyama ambao unakuta kuna chanzo kikubwa ambacho kimetokana na  mtu mmoja au watu kadhaa ambao wamechonganisha na baadaye kusababisha mateso kwa wanadamu. Wangetambua Mungu alivyo mweka wakfu binadamu, hakuna ambaye angethbutu  kufanya ubaya kama huo. Kukosa kushika amri ya mapendo ya Mungu inasababisha kuona hali halisi ilivyo mbaya. Sala ya Rosari imekuwa msaada mkubwa na kumlilia Bikira Maria ambaye kwa karne nyingi aliingilia kati kwa  vita vingi na mabalaa mengi ulimwenguni. Kwa maana hiyo alisisitizia makuhani hao kuomba na  kumlilia  Bikira Maria na kumwambia Mungu lakini wakiwa kwanza na utayari wa kupokea mapenzi yake.

Misa ya Siku Kuu ya Kupashwa Habari Bikira Maria na kuweka Wakfu kwa Moyo Safi wa Bikira Maria
26 March 2022, 11:06