Tafuta

Mlipuko wa Vokano chini ya Bahari katika kisiwa kikubwa cha TONGA na kusababisha uharibifu mkubwa wa visiwa vyote vya pembezoni. Mlipuko wa Vokano chini ya Bahari katika kisiwa kikubwa cha TONGA na kusababisha uharibifu mkubwa wa visiwa vyote vya pembezoni. 

Caritas Italia iko karibu na watu wa visiwa vya Tonga

Caritas ya Italia inaonesha ukaribu kwa Caritas Tonga na kuwasiliana na mtandao wa kimataifa ambao huko tayari kupeleka msaada kwa ajili ya wale wote ambao wamekumbwa na dharura hii ya mlipuko wa Volkano katika Kisiwa kikubwa cha Tonga chenye safu ya visiwa vidogo vidogo ambavyo vimeguswa.Papa Francisko amewakumbuka na kuwaombea kwa Mungu ili wapate faraja katika mateso.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mlipuko wa volkano huko Tonga umeleta wasi wasi mkubwa kwa kuachia madhara na uharibifu kwasababu ya  Visiwa kufunikwa na majivu, nyumba kadhaa zikaharibiwa na takribani watu watatu kufariki na wenginae bado hawajapatikana kulingana na taarifa zilizotolea. Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali ya Tonga kwa vyombo vya habari siku ya Jumanne, tarehe 18 Januari 2022 watu watatu waliofariki ni raia wa Uingereza mmoja na wawili wa Tonga. Hata hivyo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, liliripoti kuwa watu wengi bado hawajulikani walipo, huku takriban watu 90 wakielekea katika maeneo salama katika vituo vya uokoaji katika kisiwa cha Eua, na wengine wengi kukimbilia katika makazi ya marafiki na familia.

Papa amewaombea watu waliojaribiwa na Volkano ili wapate faraja katika mateso

Jumatano tarehe 19 Januari 2022, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Katekesi yake, yak ila Juma mawazo yake yamewaendelea watu wa Visiwa hivi ambao wamepata mkasa huo kutokana na Volkano iliyolipuka chini ya bahari na kusababisha madhara makubwa. Papa amesema yuko pamoja nao kiroho watu wote waliojaribiwa na kumwomba Mungu awape faraja katika mateso yao.

Majivu na vumbi kuchafua hali ya hewa na maji

Kisiwa cha Tongatapu kimefunikwa na vumbi na majivu ya volkano karibu sentimita mbili, jambo linaloibua wasiwasi wa hewa chafuzi, maji na uchafuzi wa chakula, kwani  karibu nyumba 100 zimeharibiwa na 50 zimeharibiwa kabisa. Vile vile hata nyumba za kisiwa cha Mango ambapo zimebaki nyumba mbili tu katika kisiwa cha Fonoifua. Uharibifu  huo ni mkubwa sana pia katika kisiwa cha Nomuka, kwa wastani  hali hiyo ni sehemu ya mlolongo wa visiwa vidogovidogo  kwani hata  ambapo visiwa 41 kati ya 104 vinavyoonekana vimeharibiwa, na karibu vyote vimefunikwa na majivu, kulingana na picha zilizoonekana kwenye sateliti,  ingawa kituo kinabainisha kuwa tathmini hii inabakia kuthibitishwa na timu zilizo katika maeneo. Kuna habari njema, hata hivyo kwamba vituo vyote vya afya katika kisiwa kikuu vinafanya kazi kikamilifu, na shughuli za kusafisha tayari zimeanza.

Caritas mahalia na na Caritas New Zealand wako tayari katika kambi

Caritas Tonga inajaribu kwa kila njia kujibu mahitaji ya watu waliokumbwa katika eneo hilo  na msaada mkubwa unaweza kutegemewa  na timu ya watu wa kujitolea. Mahitaji ya lazima kwa sasa ni maji ya kunywa kwa maana yaliyopo yamechafuliwa na majivu. Serikali mahalia imetangaza hali ya hatari na kuandaa usambazaji wa maji katika kisiwa cha Ha'apai (kilicho karibu zaidi na volkano). Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara alisema kuwa: “Misaada ilisambazwa ambayo, shukrani kwa Caritas Tonga na Caritas New Zealand, tayari walikuwa wamehifadhi katika baadhi ya maeneo. Misaada hiyo ni pamoja na vifaa vya kusafisha maji, makopo, vifaa vya kufanyia usafi, ndoo na mabomba.

Uharibifu umekumba karibu visiwa vyote vya pembezoni

Na kutokana na masasisho machache ambayo yamefika, Caritas Australia inasisitiza kuwa uharibifu umekumba zaidi ya yote visiwa vya pembezoni. Pia kuna hitaji la dharura la maji safi na makazi, hasa kwa jamii za pwani ambazo nyumba zao zilikumbwa na tsunami. Barabara na madaraja pia yaliharibiwa. Mawasiliano yamekatizwa na mawasiliano na nje yanawezekana tu kupitia simu ya setilaiti.

Caritas Italia kuonesha ukaribu na mshikamano wa Caritas Tonga

Kutokana na hilo pia  Caritas Italia imeonesha ukaribu na mshikamano kwa Caritas Tonga na kuwasiliana na mtandao wa kimataifa ambao huko tayari kupeleka msaada kwa ajili ya wale wote ambao wamekumbwa na dharura hii ya Volkano katika Kisiwa cha Tonga. Kwa mawasiliano zaidi : www.caritas.it

Ndege mbili za tua Tonga kupeleka msaada

Ndege mbili za kwanza zimeondoka kutoka Sydney kwa ajili ya kupeleka msaada na kutua huko Tonga, siku tano baada ya mlipuko wa Vokano chini ya bahari na Tsunami iliyofuatia baada ya vulkano majini. Kwa mujibu wa maelezo ya Umoja wa Mataifa,(UN) uharibifu umewakumba watu 84,000 kwa maana ya kusema asilimia 80% ya wakazi mahalia. Sekta ya Kilimo imepata jaribio kubwa kutokana na usalama wa vyakula.

19 January 2022, 14:43