Tafuta

Watu nchini Myanmar wanaoteseka waweze kuhakikishiwa usaidizi wa kibinadamu na ulinzi wa maisha ya binadamu. Watu nchini Myanmar wanaoteseka waweze kuhakikishiwa usaidizi wa kibinadamu na ulinzi wa maisha ya binadamu. 

Myanmar:Wito wa maaskofu ili watu wahakikishiwe msaada wa kibinadamu

Tunaomba sana heshima ya maisha,heshima ya utakatifu wa mahali patakatifu katika maeneo ya ibada,uadilifu wa hospitali na shule.Wale wote wanaojaribu kusaidia watu lazima walindwe.Haya ni maelezo yaliyomo kwenye hati ya mwisho wa mkutano wa Baraza la Maaskofu nchini Myanmar uliofanyika kuanzia tarehe 11-14 Januari 2022 huko Yangon.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu Katoliki nchini Myanmar, wako katika sehemu ya haki, amani, mapatano na kuomba nguvu kwa watu wote ambao wanahusishwa kurahisha hupatikanaji wa msaada wa kibinadamu msingi. Tunaomba sana heshima ya maisha, heshima ya utakatifu wa mahali patakatifu katika maeneo ya ibada, uadilifu wa hospitali na shule. Wale wote wanaojaribu kusaidia watu lazima walindwe”. Huu ndio wito uliomo katika tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Myanmar, lililotiwa saini na Maaskofu wote wa nchi hiyo na kutolewa huko Yangon, baada ya nchi hiyo kukumbwa na ongezeko la hatari la ghasia na mashambulizi ya silaha katika wiki za hivi karibuni.

Makanisa ya Kikatoliki ya eneo hilo na mashirika ya kibinadamu kama vile Unicef ​​​​yalitoa tahadhari katika siku za hivi karibuni za kuongezeka kwa vurugu na milipuko ya mabomu, hasa katika baadhi ya maeneo ya nchi. Baraza la Maaskofu Katoliki Myanmar kwa maana hiyo limesikitishwa sana na hali ya sasa nchini humo na linaonesha wasiwasi wake juu ya ongezeko la kutisha la hatari kwa maisha na usalama wa watu wasio na hatia hasa watoto waliokimbia makazi yao ndani ya nchi, watoto, wanawake, wazee na wagonjwa katika maeneo yenye migogoro, bila kujali rangi na imani. Hawani maelfu wanakimbia, mamilioni wanakufa kwa njaa.

Maaskofu -waliokusanyika huko Yangon kuanzia tarehe 11 hadi 14 Januari 2022 kwa ajili ya Mkutano Mkuu walitoa shukrani zao kwa mapadre wote na watawa waliojitolea kusindikiza na kuwasaidia wale wanaokimbia kutoka katika hali hatari. Katika Kanisa kuu la jiji la Loikaw, kwa mfano, jimbo hilo linatoa ukarimu na ukaribisho kwa takriban watu 200 waliokimbia makazi yao, wengi wao wakiwa wanawake, watoto, wazee na wagonjwa. Taifa hilo litaponywa kwa ishara hizo, maaskofu waliandika katika ujumbe huo na kuongeza kuwa: “Kama chombo kilichoanzishwa kwa misingi ya imani, Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Myanmar linaamini kwa uthabiti kwamba ‘lo lote linawezekana kwa Mungu’.

Maskofu aihdha wanahisimiza sana majimbo yao yote Katoliki kuendeleza amani ya nchi yao  kwa juhudi zote zinazowezekana, hasa kwa njia ya maombi. Kwa ksindikizwa nao kichungaji, wataweza kuleta faraja katika uhitaji. Huduma yao wanasema itamfikia kila mtu katika nchi hiyo bila kujali rangi au dini ”. Tangu Mosi Februari 2021, ambayo ilikuwa ni siku ya mapinduzi nchini humo, zaidi ya watu 1,400 wameuawa, wengine kutiwa mabaroi na watoto wasiopungua 50, na zaidi ya watu 10,000 wamekamatwa. Miongoni mwao pia mapadre wakatoliki na wachungaji wa wa Makanisa ya kiinjili.

17 January 2022, 15:51