Kard. Zuppi aongoza mazishi ya Kitaifa ya Bwana Sassoli
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.
Ijumaa tarehe 14 Januari 2022, saa sita kamili imefanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa la Mtakatifu Maria wa Malaika, Roma kwa ajili ya Bwana David Sassoli aliyekuwa Rais wa Bunge la Ulaya na ambaye aliyeaga dunia siku ya Jumanne tarehe 11 akiwa na umri wa miaka 65. Zaidi ya kuwapo Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella, katika Mazishi Kitaifa, Waziri Mkuu Mario Draghi, mawaziri na viongozi wa vyama mbali mbali, wageni wengine 300, miongoni mwao kutoka ngazi ya Bunge la Ulaya kama vile Bi Ursula von der Leyen na Michel, na umati mkubwa ulioshiriki kwa nje kutokana na dharura ya kiafya inayoendelea kuwa tishio. Hata hivyo Mjane mke wa Sassoli na watoto wake walitiwa moyo na familia zao, marafiki zake ambao ni kutoka sekta ya kisiasa na ya waandishi wa habari, kwani Bwana David kabla ya kwenda ngazi ya Juu alikuwa mwandishi maarufu wa habari katika Televisheni ya Taifa la Italia(RAI).
kifo ni kazaliwa kwa upya huko mbinguni na kuwa na maisha mapya
Aliyeongoza Ibada ya Misa alikuwa ni Kardinali Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Bologna Italia, na ambaye akiwa kijana alisoma shule moja ya Virigilio Roma na Marehemu Sassoli, na mara nyingi waliweza kukutana katika mikutano mbali mbalo, ikiwa ni pamoja mkutano wa hivi karibuni wa G20 wa kidini uliofanyika mjini Bologna. Kardinali Zupi katika mahubiri yake amegusia wasifu wa Bwana Sassoli na hasa jinis alivyo weza kuishi ugonjwa wake kwa ujasiri na unyenyevu akiwa anafanya kazi. Alikuwa ni mwanaume kwa ajili ya wote na alikuwa mtu wa umoja. Amenukuu, amesisitiza kuwa ukristo sio wazo bali ni mtu na kwamba maana kifo ni kazaliwa kwa upya huko mbinguni na kuwa na maisha mapya”
Salamu za rambirambi za maaskofu wa Ulaya
Katika salamu mbali mbali za rambi rambi, maaskofu wa Ulaya wanaadika kuwa: “Rais Mteule wa Bunge la Ulaya, mnamo 2019, alisisitizia hitaji la sera karibu na raia na mahitaji yao, hasa kwa vijana, kukuza maadili ya Ulaya na umakini maalum kwa ajili ya walio wadogo, ndivyo aliandika Askofu Mkuu Gintaras Grušas wa Vilnius na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya CCEE. katika ujumbe wa salamu za rambi rambi. Kwa mujibu wake: “Maaskofu wa Ulaya wanakumbuka undani wake mkuu wa kisiasa na kitaasisi na kujitolea kwake, kama mwamini, kwa mazungumzo na huduma kwa manufaa ya wote. Rais wa Baraza la Maaskofu Ulaya Comece, Kadinali Jean-Claude Hollerich, ameelezea huzuni kubwa kwa ajili ya kifo cha David Sassoli, rais wa Bunge la Ulaya. “Nimehuzunishwa sana kusikia habari kwani alikuwa mtu wa maadili na mazungumzo, mwenye hisia kubwa ya wajibu, ambaye alifanya kazi kwa manufaa ya wote kama mwandishi wa habari na kama kiongozi wa Umoja wa Ulaya ili kuboresha taasisi za kidemokrasia na kuwaleta karibu na wananchi wa Ulaya.
Ujumbe wa Maaskofu wa Italia
Katika kujitolea kwake kitaaluma kama mwandishi wa habari na baadaye kama mtu wa taasisi, amekuwa akifanya kazi kwa ajili ya jamii inayounga mkono zaidi na kuzingatia mahitaji ya vijana na walio wadogo. Hiki ni kifungu kutoka katika ujumbe wa rambirambi wa Baraza la Maaskofu Italia CEI, uliotiwa saini na Kardinali Gualtiero Bassetti Rais wa Baraza hilo. Kwa mujibu wa ujmbe huo “alisistiza kwamba waamini na walei wote wanaweza kwa pamoja kujenga upya nyumba ya pamoja ili kuendelea kupambana dhidi ya miungu, kubomoa kuta, kujenga madaraja, kutoa umuhimu kwa ubinadamu mpya, kama alivyosisitiza katika hotuba yake huko Bari, wakati wa tukio la mkutano Baraza la Maaskofu Italia uliokuwa unaongzwa na kauli mbiu “ 'mpaka wa amani wa Mediterranean' mnamo 2020 ".