Tafuta

Mgogoro nchini Ethiopia unaendelea. Mgogoro nchini Ethiopia unaendelea. 

Ethiopia:Watawa 7 waachiwa huru baada ya kushikiliwa tangu Novemba 2021

Watawa 7 wa kabila la Kitigrina wa mashirika mawili tofauti ambao walikuwa mikononi mwa vyombo vya dola,labda katika muktadha wa operesheni za kuchanganua watu waliokuwa karibu na waasi wa Tigray wameachiwa huru.

Sr. Angella Rwezaula -Vatican.

Vyombo vya madola, nchini Ethiopia vimewaachia huru watawa 6 wa Shirika la Mabinti wa Upendo, la Mtakatifu Vincent wa Pauli walioshikiliwa huko Addis Abeba mnamo tarehe 30 Novemba 2021. Kwa mujibu wa shirika la habari za kimisonari Fides, linabainisha kuwa hawa ni Sr Letemaryam Sibhat, Sr Tiblets Teum, Sr Abeba Tesfay, Sr Zaid Moss, sr Abeba Hagos na sr Abeba Fitwi, lakini pia Jumamosi 15 Janauri mchana aliwekwa huru hata Sr. Abrehet Teserma, wa Shirika la Mtakatifu Ursula huko Gandino, ambaye alirudi kwenye jumuiya yake ya kitawa iliyoko Shola na kwamba watawa wote wako salama na afya tele.

Watawa wote kike na kiume wa kabila la kitigrina walikuwa wanashukiwa

Pamoja watawa hao kurudi kwenye jumuiya zao, lakini hakuna taarifa zozote kuhusu mashemasi wawili na watawa engine wa Kobo ambao wako katika hali ya kifungo pamoja na maelfu ya waethiopia wenye asili ya kitigrina ambao wamefungwa katika maeneo yasiyoeleweke vizuri. Watawa hao wa kike walikuwa wameondolewa kwenye nyumba zao wakati wa operesheni ya polisi, ambapo walikamatwa watawa wote wa kabila la kitigrigna kwa sababu ya  kushukiwa kuwa walikuwa wanashirikiana na waasi wa Tigrey (TPL) katika nchi.

Watawa Wasalesiani 17 na walei walichukuliwa tarehe 5 Novemba 2021

Mnamo tarehe 5 Novemba 2021, huko Addis Abeba, katika kituo cha mafunzo cha Wasalesiani, eneo la Gottera, walikamatwa watu 17. Kikosi cha wanajeshi wa serikali, walivamia jengo la shule na kuwaondoa watawa na walei huku wakawapakia kwenye lori na kuwapeleka mahali pasipojulikana. Lakini baada ya kuulizwa kuhusiana na masuala ya fedha ya shule wote waliachiliwa huru tarehe 13 Novemba 2021

18 January 2022, 15:38