Tafuta

Maaskofu nchini Equador wanasema lazima kutetea uhai wa maisha bila kutoa mimba na hivyo wanapinga muswada wa sheria. Maaskofu nchini Equador wanasema lazima kutetea uhai wa maisha bila kutoa mimba na hivyo wanapinga muswada wa sheria.  (©Natalya Lys - stock.adobe.com)

Equador:Maaskofu wapinga muswada wa utoaji mimba katika kesi ya ubakaji au ulemavu

Kutoa mimba sio haki bali ni uhalifu. Hivyo ndivyo Rais wa Baraza la Maaskofu wa Equador wanawaandikia Tume ya Haki ya Bunge ili kupitia kwa upya mswada unaoruhusu utoaji mimba katika kesi la ubakaji,mimba za utotoni au wanawake wenye ulemavu,ili maisha yalindwe na pingamizi lihakikishwe la dhamiri ya madaktari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika barua ya Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Equador amewaalika wajumbe wa Bunge la nchi hiyo, kuhusu muswada wa sheria unaotoa dhamana ya utoaji wa mimba kwa hiari kwa wasichana, vijana na wanawake pale inapotokea ukatili wa kijinsia. Katika barua hiyo inasema: “Mswada wa sasa unalenga pekee katika utoaji mimba kama njia pekee mbadala kwa wanawake waathirika wa ubakaji na unapunguza binadamu aliyetungwa mimba kuwa bidhaa rahisi isiyo na haki.” Katika waraka huo, Maaskofu hao wanaeleza kuwa Mahakama ya Katiba iliitaka Ofisi ya Mchunguzi wa Haki za Binadamu na Bunge la Kitaifa kuweka masharti na matakwa ili kuwepo na uwiano wa kutosha kati ya ulinzi wa maisha tangu kutungwa kwake na haki za kikatiba ya mahitaji ya wanawake waathirika wa ubakaji. Hata hivyo, Ijumaa iliyopita tarehe 14 Januari 2022, Tume ya Haki ya Bunge iliendelea na mjadala kuhusu muswada huo ili kubaini, hasa, ikiwa utoaji mimba, katika kesi ya unyanyasaji wa kijinsia, unaweza kutumika ndani ya kipindi cha juu cha wiki 28 za ujauzito (miezi saba) katika kesi ya watu wazima na bila mipaka ya muda na katika mimba za utotoni na wanawake wenye ulemavu.

Hakuna sheria ya kimataifa au ya kitaifa inayotambua utoaji mimba kuwa ni haki

Kwa upande wa Baraza la Maaskofu, muswada huo umeegemezwa katika dhana mbili zisizo na msingi: “kutoa mimba ni haki” na kwamba “maisha ya mwanadamu hayaanzii na kutungwa”. Na kwa maana hiyo maaskofu wamekumbusha kwamba “atiba ya Equador inalinda maisha tangu kutungwa kwake” na kwamba “utoaji mimba si sehemu ya haki za kujamiiana na uzazi na upangaji uzazi”, na kwamba “hakuna sheria ya kimataifa au ya kitaifa inayotambua utoaji mimba kuwa ni haki”, maaskofu wamesisitiza.

Maisha ya Mwanadamu yanaanzia tangu kutungwa kwake hadi mwisho

Baraza la Maaskofu wa Equador limekazia kusema  kwamba “maisha ya mwanadamu huanza na kutungwa kwa mimba, hadi mwisho wake na kama sayansi ya matibabu inavyoonesha, na ni ya kibinafsi, kiholela na kinyume na matokeo yoyote ya kiufundi na kisayansi ili kuonesha umri wa ujauzito ambao inawezekana kutoa mimba. Baada ya kutungwa kwa mimba, upasuaji wowote, wa kimatibabu au wa kemikali, unamaliza muhtasari na kiholela kwa maisha ya mwanadamu”. Na kwa hivyo, Maaskofu wanaona, pia wakizingatia hatari kwa ajili ya afya na maisha ya mama, utoaji mimba haupaswi kutumika kama sababu ya kuua mwanadamu, hata kama katika kesi ya ubakaji hakuna vikwazo vya kisheria vinavyowekwa wahusika wa kutoa mimba”.

Ubakaji ni uhalifu lazima wawajibishwe bila kuwaachia waende zao

Kwa mujibu wa Baraza la Maaskofu, zaidi ya hayo, ubakaji, kama inavyothibitishwa na kanuni ya adhabu, na ni uhalifu lakini haulaumiwi na kuchunguzwa kwa kina, ambapo hukuza hali ya kutokujali na kuhimiza kurudiwa na waalimu hao. Kutokana na hivyo maaskofu wanatoa lawama kwamba kwamba badala ya kuanza uchunguzi na kuchukua hatua za ulinzi kwa ajili ya waathirika, wanabaki bila malalamiko, na  hakuna haki, mbakaji huenda zake bila kuadhibiwa na mwanamke anabaki bila mtetezi.

Madaktari wanafurahia haki ya kibinadamu na ya kikatiba na kukataa kwa sababu ya dhamiri

Hatimaye, Maaskofu wa Equador wanawakumbusha washiriki wa mkutano huo kwamba madaktari wanafurahia haki ya kibinadamu na ya kikatiba ambayo ni kukataa kwa sababu ya dhamiri, na kwa hiyo wafanyakazi wa matibabu hawapaswi kulazimishwa kutoa mimba dhidi ya imani yao wenyewe ya matibabu, maadili na adili chini ya tishio la vikwazo kama vile faini au kifungo. Maaskofu wa Ecuador wanahitimisha barua hiyo kwa wito wa kuwa na busara na nia njema  kwa wajumbe wa Bunge la Kitaifa, ili katika muswada huo kuwe na usawa wa kutosha kati ya ulinzi wa maisha tangu kutungwa kwa  mimba na haki za kikatiba za wanawake waathirika wa mimba wa ubakaji ”, kama ilivyoelezwa na Mahakama ya Katiba.

19 January 2022, 10:24