Tafuta

Afrika ya Kati ina utajiri mkubwa wa madini mengi  kama  dhahabu, almasi chuma, manganese, shaba, au tuseme ni ardhi adimu yenye madini ya kutengeneza vifaa vya kidigitali Afrika ya Kati ina utajiri mkubwa wa madini mengi kama dhahabu, almasi chuma, manganese, shaba, au tuseme ni ardhi adimu yenye madini ya kutengeneza vifaa vya kidigitali 

Afrika ya Kati:Unyonyaji mbaya wa rasilimali za nchi unaharibu mazingira

Katika ujumbe uliochapishwa wakati wa kuhitimisha mkutano wa mwanzoni mwa mwaka wa Maaskofu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,wanalaani vitendo vya unyonyaji mbaya wa rasimali za nchi na kwamba unaharibu mazingira.Aidha kuna mgogoro wa kimaadili ambao unawagusa watoto wananyonywa na watu wazima wasio wema.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Unyonyaji mbaya na uharibifu wa mifumo yao ya kiekolojia unaopesha sana kwa mujibu wa Maaskofu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ulioandikwa katika ujumbe uliochapishwa wakati wa kuhitimisha mkutano wao wa kwanza wa Maaskofu kwa mwaka huu. Maaskofu katika ujumbe huo wanasisitiza kuwa maliasili za nchi yao zinaporwa na wageni kwa ushirikiano wa baadhi ya wakazi. Kwa maana hiyo wanawaomba kwa moyo wote uwazi kuhusu mikataba kati ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na washirika na nchi za kigeni.

Ufisadi, utajiri usio halali uzembe na ukosefu wa maadili

Unyonyaji mbaya  wa mali asili za Afrika ya Kati unaongezewa hata na mgogoro wa thamani za kimaadili, ambao ni  ubaya mwingine unaosumbua Nchi kama walivyokumbusha katika ujumbe. Ufisadi, utajiri usio halali, ukatili wa uendeshaji, uzembe na ukosefu wa maadili ya kitaaluma katika baadhi ya huduma za serikali, matumizi mabaya ya mamlaka na ukosefu wa haki, zote ni dalili zinazoonesha mgogoro wa maadili. Huo ni mgogoro wa kimaadili ambao kwa Maaskofu wanasisitiza kuwa unawagusa watoto ambao wananyonywa na watu wazima wasio wema, kuliko wale wenye nguvu katika kimo chao.

Utumiaji wa fursa za ujinga kuwanyonya watoto

Kwa upande wa mtazamo wa kijamii, maaskofu wanabainisha kwamba watu hao wanatumia fursa ya ujinga wa watoto na kuwanyonya kwa madhumuni ya ngono, hivyo kuweka rehani ujana wao na maisha yao ya baadaye.  Kwa mtazamo huo, mwezi Septemba Umoja wa Mataifa uliamuru kuondoka kwa karibu wanajeshi 450 huko Gabon kama kikosi cha kulinda amani katika Jamhuuri ya Afrika ya Kati, baada ya kushukiwa kuwa na unyonyaji wa kijinsia na manyanyaso ya kingono ambapo serikali ya Libreville ilifungua uchunguzi dhidi yao. Mbali na dhahabu, almasi na mbao, rasilimali zinazotumiwa, Afrika ya Kati ina utajiri mkubwa sana wa madini mengi kama: cassiterite, chuma, manganese, shaba, au kinachojulikana kama ardhi adimu, yenye vitu muhimu sana kwa ajili ya uchumi wa ‘digitali’ na ile ya ‘kijani’.

20 January 2022, 13:58