Tafuta

1638214420283.jpg

Ujumbe wa CEI kwa Siku ya Mazungumzo kati ya Wakatoliki na Wayahudi

Baraza la Maaskofu Italia wamechapisha Ujumbe wa 33 wa Siku ya tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakatoliki na Wayahudi ambayo itafanyika tarehe 17 Januari 2022 kwa kuongozwa na kauli mbiu:“Nitatimiza ahadi yangu njema” (Yer 29, 10).Katika ujumbe wanaonesha hofu kutokana na matukio yanayojitokeza ya kiubaguzi.Wakristo na wayahudi wote wasaidiane kukabiliana na changamoto.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Tarehe 17 Januari  2021 ni Siku ya tafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakatoliki na Wayahudi, ambapo kwa wakristo ni fursa muhimu ili kutunza heshima, mazungumzo na fursa ya kujua vema utamaduni wa wayahudi. Ndivyo ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) wameandika kwa ajili ya Siku ya 33 ya kutafakari na maendeleo ya mazungumzo kati ya wakatoliki na wayahudi. Ujumbe huo inaongozwa na kauli mbiu:“Nitatimiza ahadi yangu (Yer 29,10). Kwa bahati mbaya katika ujumbe huo unabainisha kwamba kwa kipindi wanaona matukio mbali mbali yanayotaka kufuta kumbu kumbu na vile vile kuona chuki dhidi ya Wayahudi. Siku hiyo ina maana kubwa kwani ni fura ya kusisitiza mahusiano yanayofungamana na Kanisa na Israeli ili kutazama jumuiya za wayahudi wa sasa kwa uhakika kwamba Mungu anaendelea kutenda katika watu wa Agano la kizamani na kufanya kuzaliwa upya thamani za hekima ambayo inatokana na kukutana na Neno la Mungu. (EG 249).

Mazungumzo kuhusu amri kumi na vitabu vitano

Ujumbe wa Maaskofu nchini Italia unasema kwamba miaka ya mwisho, mada zinazohusu mazungumzo zimejikita kutazama amri 10 na Meghilloth, ( yaani vitabu vitano muhimu vinavyosomwa kwa lengo la liturujia ya wakati fulani wa siku  kuu kwa upande wa Wayahudi), sasa kwa mwanga wa janga la uviko, na matokeo yake, wamependelea kujitikia kutafakari safari ya Kinabii. Somo la Nabii Yeremia ndilo linapendekezwa ambaye anaonekana kufanana zaidi katika kipindi kigumu ambacho kila mmoja anapitia. Kwa kauli mbiu ya ujumbe huo ni maneno ya waraka wa nabii Yeremia alioupeleka toka Yerusalemu, kwa  waliobaki wakuu waliochukuliwa mateka (Yer 29,1-23). Katika barua yake, Yeremia anawageukia watu waliokuwa wanaishi kama mateka na kwa maana hiyo Israeli inajikuta katikati ya wapagani, wakiwa mbali sana na nchi ya ahadi, bila hekalu, na kwamba ni katika hali hiyo,wanapata maana ya wito wao.  Hayo yalikuwa ni kuendelea kwa nchi hiyo, kusimika mizizi, kusaidia amani na kuhamasisha matarajio kwa wote kuanza na mambo msingi na rahisi ya maisha (kazi, uhusiano, nyumba, familia…).

Huo ndio wito anaowakabidhi Mungu watu wake

Huo ndiyo wito wa Mungu anaowakabidhi walio wake. Katika maelekezo ya namna ya kuishi wakati wa kuchukuliwa mateka, ulikuwa umefungamana na ahadi ya wakati ujao. kwa maana hiyo anayechagua kuhisi kila kitu na kubaki ameshikilia ya wakati uliopita wenye sifa, yuko hatari ya kujipoteza hata mwenyewe, wakati yule anayekuwa na uwezekano wa kuacha kila aina ya uongo wa uhakika ataweza kuona siku zake, wanabainisha maaaskofu katika ujumbe wao. Hata hivyo kwa kutazama janga hili wamesema "Haisaidii kujidanganya kufanya kwa haraka ili kufikia jinsi ilivyokuwa mwanzo". Na hhii inaonesha kwamba wakati ule "Jumuiya iliyokuwa mateka ilikuwa na vishawishi viwili: kupoteza kila tumaini na kujenga jumuiya iliyofungwa". Katika janga kama waamini, maaskofu wanabainisha kuwa wameona vishawishi sana na vile vya  kupoteza tumaini na jumuiya kuendelea kujifungia binafsi kwa kutaka kujitosheleza wenyewe kama ilivyokuwa zama za Nabii Yeremia.

Vishawishi vya ubaguzi vya kiutamaduni na kidini

Vishawishi hivyo vinavyojionesha mbele ya hali halisi ya matukio ya ubaguzi wa kiutamaduni wa kidini au ya ukristo inao hatarisha kupoteza hata tumaini na kuunda jumuiya ambazo zinajifunga zenyewe zaidi. Nabii Yeremea kwa maana hiyo anatoa mwaliko wa kuwa chanya ndani ya uhalisia na kusimika mizizi ili kukaa ndani ya upyaisho. Changamoto ya kidini ipo mahali ambapo inatakiwa kuwa chanya kwa kuwa na uweza wa kufanya kazi ili kujenga jamii na ambayo inatoa matumaini mapya. Wakristo na kama ilivyo kwa Wayahudi wote wanaweza kusaidiana kukabiliana na changamoto hiyo, ili ahadi ibaki kidete katika historia, wanasisitiza Maaskofu. Bwana anafanya kazi ili kuanzisha upya. Yeye ni mwaminifu na hawezi kamwe kuacha watu wake. Kila mgogoro ni fursa njema, kipindi muafaka kisichopotezwa kupanda mbegu ya tumaini. Wakimbizi wanatoa jitihada kuirejesha nchi, wanafanya kazi, wanawekeza nguvu kwa ajili ya nchi hadi kufikia kusali kwa Bwana kwa ajili ya ustawi wa Nchi wanazokaribishwa.

Mgeni ni rasilimani kwa ajili ya nchi anayoingia

Katika ujumbe huo wa maaskofu wa siku ya tafakari kuhusu Wayahudi, unabainisha kuwa hii inakumbusha kuwa yule anayetoka nje kwa maana hiyo mgeni ni rasilimali kwa ajili ya nchi na kwamba mgeni ni baraka na kukarimu kama kitovu cha utamaduni wa kiyahudi na kikristo unaweza kuwa mtindo ambao leo hii kama waamini wanafanya katika historia na kuisha kijamii. Barua ya Yeremia kwa maana hiyo ni maandishi ambayo yanapaswa kusomwa kwa sauti kuu mbili katika siku hiyo ili kuweza usaidia kugusa uzoefu wa imani katika kipindi hiki cha mabadiliko ya enzi. Mada a ujenzi  mpya wa matumaini, wa mazungumzo  na hali halisi, unakumbusha juu ya kukubiliana na mwingine hata mgeni, kwamba inawezakana kupata muafaka sana kulingani na namna ya kuishi katika nchi. Hii ni fursa kwa hakika ya kukabiliana na mazungumzo. Kwa wakristo wote wakatoliki wanaweza kufundisha ukweli wa mtindo wa sinodi. Kwa kuhitimisha ujumbe wao, Maaskofu wa Italia anawageukia Jumuiya ya Wayahudi wa Italia wakiwashukuru kwa kile wanachowakilisha kwao na kuwaomba wahisi ushiriki huo wa mchakato ambao kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema, kwamba inawezakana kusaidiana kwa pamoja ili kushirikishana utajiri wa Neno na kama ilivyo hata kushirikishana imani  adilifu na wasiwasi wa pamoja kwa ajili ya haki na maendeleo ya watu (EG 249).

06 December 2021, 14:46