Tafuta

5.jpg

Pakistan:Kanisa kusadia makatekista ambao ni injini ya utume!

Kanisa linafanya jitihada kubwa iwezekanavyo kuwasaidia makatekista 112 katika utoaji wa huduma kwenye majimbo.Zaidi jimbo limetoa shukrani kusaidia makatekista wazee,waliostaafu na wajane makatekista waliostaafu.Ni maelezo ya Askofu Indrias Rehmat wa Faisalabad nchini Pakistan.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Makatekista wanajikita katika utume muhimu sana wa uinjilishaji wa Kanisa. Katika majimbo, makatekista wengi wanatembea kwa umbali mrefu sana ili kuona jumuiya ndogo ndogo.  Utume wao kwa hakika ni msingi kwa ajili ya kuhitafadhi na kufundisha imani katoliki kwa waamini katika majimbo na ili kuwafanya wahisi ukaribu sana wa Kanisa. Na Kanisa linafanya jitihada kubwa iwezekanavyo ili kuwasaidia makatekista 112 katika utoaji wa huduma kwenye majimbo. Zaidi jimbo limetoa shukrani kusaidia makatekista wazee, waliostaafu na wajane makatekista waliostaafu.

Usaidizi kwa makatekista wazee na wajane

Haya ni maelezo kutoka kwa Askofu Indrias Rehmat, anayeongoza jimbo katoliki la Faisalabad, huko Punjab nchini Pakstan. Kwa mujibu wa Askofu huyo amebainisha kwamba wanatoa mchango wa fedha kuwasaidia kununua vyakula hata kwa ajili ya mradi wao wa viwanja ulioanzishwa kwa makatekista 30 wazee na wastaafu na familia zao kuweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku. Askofu Rehmat amethibitisha jinsi alivyohisi hitaji la nguvu kwa ajili ya kuonesha pongezi makatekista wao ambao mara baada ya Papa Francisko kuchapisha Barua yake binafsi ya Kitume 'Antiquuum Ministerium' ambayo ilikuwa na utambuzi na kuanzisha rasmi huduma ya Makatekista. Askofu huyo pia anamshukuru sana Papa Francisko kwa utambuzi huo, kwani wao wanaona kwa karibu sana changamotoa ambazo wanapitia na kukabiliana nazo wakati wa kutenda huduma yao hiyo ya kila siku. Kwa namna ya pekee katika kipindi cha Janga la Uviko -19 makatekista wanaishi kipindi kigumu sana. Vile vile tangu mwaka jana Kanisa Katoliki lilizindua huduma hai kwa ajili ya makatekista 112 kuweza kuwa na huduma ya matibabu na kugharimia manunuzi ya dawa, ikiwa wanaugua au kupata matatizo ya kiafya kutokana na UVIKO.

Shukrani kwa uaminifu na ukarimu wao

“Makatekista wetu wanapokea, kwa ajili ya kazi yao ya wakati wote katika huduma ya Kanisa, mshahara mdogo zaidi: tunatambua na kuthamini huduma yao ya kitume, inayofanywa kwa bidii na kujitolea, katikati ya changamoto nyingi. Kwa sababu hiyo, Kanisa la Faisalabad limeanza mpango wa kutumia viwanja 30 vinavyokusudiwa kwa ajili ya makazi, kwa makatekista hasa wazee au wastaafu ili kuwapa mahali pa kuishi. Askofu anaongeza: “Tunawashukuru pia waamini wetu Wakristo kwa ukarimu wao na msaada wao kwa kazi ya kimisionari ya Makatekista wetu; Ninawaomba mapadre, watawa na waamini kuunga mkono kazi yao kuu, kuwaenzi na kuwasaidia kwa kazi muhimu ya kichungaji na kimisionari”.

Makatekista wanatoa muda mwingi wa kichungaji 

Akizungumzia kuhusu huduma waliyopewa Makatekista, Askofu amebainisha kwamba Changamoto katika huduma ya Makatekista zinaongezeka siku baada ya siku.  Kuna ukuaji kwa kazi wa Wachungaji na Jumuiya za madhehebu mengine ambayo yanatengeneza makanisa mengine madogo na huduma yao; Kuna fursa mbaya za imani, ambazo zipo kupitia Intenet na mitandao ya kijamii. Na zaidi kuna ongezeko la kushuka ambalo daima linakuwa gumu kukabaliana na gharama za mahitaji msingi za familia. Mara nyingi makatekista wanalazimika kufanya kazi mara mbili ili waweze kuishi, wakati huo wa kutoa muda wao kuweza kutoa huduma ya kichungaji ya kifamilia, na kuweza kutosheleza mahitaji ya kiroho kwa waamini.

Mwaka 2022 ni mwaka wa makatekista jimbo la Faisalabad Pakistan

Kwa kuhitimisha Askofu amesema katika kipindi cha maandalizi ya Sinodi 2021-2023, wanatarajia kutangaza mwaka 2022 kuwa mwaka wa Makatekista katika Jimbo la Faisalabad, kwa kuanza na tafakari kuu ya Hati ya Papa Francisko ya Antiquum Minsterium. Kwa kuthamanisha huduma hiyo ya kitume na thamani ya utume wa uinjilishaji. Kwa makatekista, hao Askofu anatoa shukrani kubwa kwa kile ambacho wanafanya kwa kusafiri kwa uvumilivu na ili  waamini wapate kusimika mizizi na kukua katika imani, matumaini na upendo.

08 December 2021, 12:56