Tafuta

Eucaristia calici ostie comunioneAEM.jpg

Maaskofu Marekani wakubaliana hati juu ya Sakramenti ya Ekaristi

Kwa kura 222 za ndiyo,8 hapana wa ushauri wa kukataza kupewa komunyo kwa watu mashuhuri wa umma wanaotetea misimamo ambayo haiendani na mafundisho ya maadili ya Kanisa,ndiyo umesikika kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu Marekani uliofanyika huko Baltimore,kwa kutoa hati kuhusu“huduma ya Ekaristi katika maisha ya Kanisa.Watu wa umma wanakumbushwa kuendana na nafasi zao na imani na maadili ya Kanisa.

Na Sr. Angella Rwezaula- Vatican.

Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano na siku mbili za mjadala mkali, maaskofu wa Marekani waliidhinisha hati iliyokuwa ikisubiriwa kuhusu upatanisho wa Ekaristi. Maandishi hayo yalipendekezwa baada ya uchaguzi wa 2020 na baadhi ya maaskofu wa Marekani ambao waliona haja ya kuchukua msimamo ulio wazi kuhusiana na Rais Mkatoliki anayepinga mafundisho ya Kanisa. Suala la mrejesho ulikuwa ni kukubalika kwa uhalali wa kutoa mimba na ambapo Rais Joe Biden, mkuu wa pili wa Ikulu ambaye ni Mkatoliki katika historia ya Marekani. Lakini katika hati iliyopitishwa na kura 222 za ndiyo, nane hapana na tatu hakuna mrejesho wa wazi kuhusu mwanasiasa yeyote, wala kuchunguza ushauri wa kukataa komunyo kwa watu mashuhuri wa umma wanaotetea misimamo ambayo haiendani na mafundisho ya maadili ya Kanisa. Hata hivyo, waraka huo unasema kuwa Wakatoliki walio na nyadhifa za mamlaka wana wajibu wa pekee katika kufuata sheria za Kanisa. Na wanasisitiza kwamba wale wanaopokea komunyo licha ya kuwa wamekataa mafundisho ya Kanisa katika maisha yao ya hadharani huzua kashfa na kudhoofisha azimio la Wakatoliki wengine kuwa waaminifu kwa matakwa ya Injili.

Hata hivyo wakati wa mkutano wa kwanza wa mashauriano ya kibinafsi ndani ya miaka miwili, Baraza la Maaskofu wa Marekani lilikubali mialiko ya Vatican ya kuepuka shutuma zinazoweza kuwa chanzo cha mafarakano, kama vile Kadinali Luis Ladaria, Rais wa Baraza la Kipapa la Mafundisho tanzu ya kanisa alikuwa ameonya katika barua maaskofu wa Marekani. Hofu pia ilitawala, ambayo iliyooneeshwa na baadhi ya maaskofu kama vile Robert McElroy wa Mtakatifu Diego, kwamba Ekaristi inaweza kutumika kama silaha katika vita vya kisiasa. Siku ya tatu ya kikao cha mkutano mkuu huko Baltimore, ambacho pia kilikuwa wazi kwa waandishi wa habari, hata hivyo, ilifichua kwamba maoni tofauti juu ya suala hilo yanabakia ndani ya Mkutano huo. Andiko hilo, kwa hakika, linawakabidhi maaskofu binafsi kazi maalum ya kurekebisha hali zinazohusisha matendo ya umma tofauti na ushirika unaoonekana wa Kanisa na sheria ya maadili" Na ikiwa baadhi ya maaskofu wametafsiri kifungu hicho kuwa mwaliko wa mazungumzo, wengine wameona kuwa ni uwazi unaowezekana wa kuwanyima Ekaristi wanasiasa wa wakatoliki wanaokubali msimamo wa kutoa mimba.

Kamati ya mafundisho jamii ya Kanisa iliandika kurasa 30 za “Fumbo la Ekaristi katika maisha ya Kanisa” pia ilikubali katika dakika ya mwisho ombi la askofu mkuu Salvatore Cordileone wa Mtakatifu Francisco,  la kujumuisha wajibu wa watu katika nafasi hiyo wa mamlaka ya kuendeleza maisha ya mtoto ambao hawajazaliwa. “Kushindwa kutambua aina ya binadamu wahanga wa maangamizo makubwa zaidi ya maisha ya binadamu katika wakati wetu itakuwa ni jambo lisiloeleweka ambalo, kwa baadhi yetu, lingegeuza waraka huu kuwa tatizo badala ya kuwa msaada,” alisema Askofu Mkuu. Maaskofu hao wa Marekani walikubaliana kwa kauli moja kueleza kwamba waraka huo unaenda mbali zaidi ya suala la wanasiasa wakatoliki na zaidi ya yote unaangazia nafasi ya sakramenti katika maisha ya Kanisa. Kurasa 30 kwa hakika zinaweka msisitizo mpya juu ya katekesi juu ya maana ya Ekaristi, kwa kuitikia kupungua, huko Marekani, kwa imani katika uwepo halisi wa mwili na damu ya Yesu Kristo katika kumunio.

18 November 2021, 16:33