Tafuta

Maaskofu nchini Argentina wanawaalika Bunge kusikiliza madai halali ya watu wa asilia, wakiomba kuongezwa kwa sheria yao ya umiliki na mahali wanapoishi. Maaskofu nchini Argentina wanawaalika Bunge kusikiliza madai halali ya watu wa asilia, wakiomba kuongezwa kwa sheria yao ya umiliki na mahali wanapoishi. 

Maaskofu Argentina wameomba wanasiasa wasikilize watu wa Asilia!

Katika barua iliyotumwa kwenye Bunge,Timu ya Kitaifa ya Kichungaji kwa ajili ya watu Asilia inaomba kuongezwa muda kwa sheria ya sensa ya jamii asilia na kusimamishwa suala la unyakuzi wa ardhi yao.Asilimia 58 ya jumuiya za asilia zilizopo kwenye eneo la taifa bado hazijasajiliwa,katika makundi mengi ya Argentina ya tamaduni nyingi,kama Katiba inavyosema, kwa mujibu wa maaskofu.

Na Sr. Angella Rwezaula- Vatican.

Maaskofu nchini Argentina wanaunganisha sauti zao na zile za watu wa kiasilia, wakiunga mkono madai halali ya jumuiya hizi asilia katika barua iliyoelekezwa kwa rais wa Baraza la wabunge, Bwana  Sergio Massa. Timu ya Kitaifa ya Kichungaji kwa  ajili ya Watu wa Asilia(Endepa) nchini Argentina inayoongozwa na Askofu Luis Antonio Scozzina, inaelezea wasiwasi wake kwa kucheleweshwa dhahiri ambapo wanasiasa waliidhinisha upanuzi wa sheria 26.160 (sasa 27.400). Sheria hii inaanzisha sensa ya jumuiya zote za kiasili za nchi na kusimamisha vitendo vya utawala na mahakama vya unyakuzi kupitia uchunguzi wa kiufundi, kisheria na wa kikatili wa ardhi wanazoishi.

Katika barua hiyo aidha inathibitisha dharura na ulazima, kulingana na umiliki wa ardhi zinazokaliwa kimila na jumuiya asilia nchini, zenye hadhi ya kisheria iliyosajiliwa katika orodha ya Kitaifa iliyo elekezwa kwao. Iliidhinishwa mwishoni mwa 2006, hata hivyo sheria hii ilitekelezwa sehemu ndogo tu, wanaandika Maaskofu katika barua yao, kiasi kwamba wanasema kuwa "asilimia 58 ya jumuiya za asilia zilizopo kwenye eneo la taifa bado hazijasajiliwa, katika makundi mengi ya  Argentina ya tamaduni nyingi, kama Katiba inavyosema. Lakini hali hii ya kutochukua hatua lazima isilipwe na watu wa kiasilia", inasisitiza timu ya taifa hivyo kuwataka manaibu wabunge  kuongeza muda wa sheria kabla haijakamilika.

Katika hali ya sasa kwa mujibu wa barua kutoka kwa maaskofu, kwa kuzingatia kwamba Baraza la Wabunge linadai kutambua, kudhamini na kutetea haki za binadamu kama nguzo ya kuishi pamoja kijamii, bila kumtenga mtu yeyote, wanawaalika kusikiliza madai halali ya watu wa asilia, wakiomba kuongezwa kwa sheria hii . Tayari mwezi Machi, mwishoni mwa Bunge lake la 16, Endepa ilikuwa imesema kwamba: “ikiwa katika mshikamano na upinzani usio wa kuchoka kwa watu wa kiasilia, kwa sababu mapambano yao ya kulinda maliasili ni mapambano ya maisha ambayo lazima yashughulikie kila mtu kwa jina la ulinzi wa kazi ya Uumbaji.

Katika suala hilo suala hilo na Umoja wa Mataifa pia uliingilia. Mwanzoni mwa Novemba, kupitia kwa mratibu mkazi wa Argentina, Roberto Valent, na mwakilishi wa kikanda wa Amerika Kusini wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Jan Jarab, chombo cha kimataifaalikuwa ameomba upanuzi wa sheria, huku akielezea wasiwasi wake kwa mitazamo ya kibaguzi, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni ambao watu wa kiasili nchini Argentina, kwa namna ya pekee Wamapuche, ni waathirika. Hata hivyo wito wa Kanisa Katoliki umesikilizwa katika saa chache zilizopita, serikali imeamua kuongeza muda wa sheria kwa njia ya Amri ya ulazima na uharaka”.

Ikumbukwe kwamba Katiba ya Kitaifa ya Argentina ya 1994 inatambua, katika kifungu cha 75, uwepo wa kabila na kiutamaduni wa watu wa kiasilia na inathibitisha umiliki wa jumuiya na umiliki wa ardhi wanayokaa. Nchi hiyo pia imeidhinisha sheria kadhaa za kimataifa kuhusu watu wa kiasilia, kama vile Mkataba wa 169 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), kuanzia 1989, na kupitisha Azimio la Umoja wa Mataifa la 2007 kuhusu Haki za Watu wa Kiasilia.

24 November 2021, 13:45