Tafuta

2021.11.19 Kanisa Kuu la  Rabat linafikisha miaka 100 tangu kuzinduliwa kwake. 2021.11.19 Kanisa Kuu la Rabat linafikisha miaka 100 tangu kuzinduliwa kwake. 

Kanisa Kuu la Rabat linaadhimisha jubilei ya miaka 100

Katika mji mkuu wa Morocco,tarehe 20 Novemba 2021,uzinduzi rasmi wa Jubilei ya Kanisa Kuu lake ambalo linaitwa Mtakatifu Petro.Lilizinduliwa mnamo tarehe 17 Novemba 1921 na lilikuwa halijakamilika.Mara baada ya kukamilika likawa kituo kikuu cha wakatoliki wa nchi na kuwa Makao makuu ya Kitume yaliyozinduliwa na Papa Pio XI mnamo 1923 na baadaye kuwa Jimbo Kuu la Rabat mnamo 1955.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Tukiyatazama yaliyopita kwa shukrani na utambuzi wa kushukuru kuyaishi maisha ya sasa kwa shauku na kukumbatia yajayo kwa matumaini, huo ndiyo mwelekeo wa  Kikristo ambao Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Rabat, Kardinali Cristόbal Lόpez Romero, amewaalika kuuendeleza wakati wa maadhimisho ya miaka mia moja ya uzinduzi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro huko Rabat.  Kardinali ameandika kuwa wanapenda kuchukua fursa ya maadhimisho ya miaka mia moja kuwaenzi watangulizi wao, kushukuru yote waliyofanya na ambayo sasa wanafurahia amesisitiza hayo katika barua kwa waamini, huku akiwashuria na kuwahimiza kujenga ushirikiano kati ya wote kuanzia utofauti na kujitolea wenyewe kuishi katika udugu pia na Wakristo wa madhehbu mengine, pamoja na Waislamu na mtu yeyote mwenye mapenzi mema.

Kanisa kuu la Rabat liliwekwa wakfu mwaka wa 1933. Lilizinduliwa bado halijakamilika mnamo tarehe 17 Novemba1921. Ili kusherehekea ukumbusho wake wa miaka 100, mipango mbalimbali umepangwa hadi Juni 29 mwaka ujao, kuanzia katika sikukuu ya Watakatifu Petro na Paulo. Na kwa maana hiyo tarehe  20 Novemba 2021,  saa 4.30, itafanyika Misa ya uzinduzi wa Jubilei hiyo na kufuatiwa afla ya kukaa pamoja na saa 2 usiku litafanyika tamasha la Kwaya ya Bunge la Morocco. Mipango mingine ni pamoja na marathon ya maombi tarehe 4 na 5 Desemba 2021, matamasha ya Orchestra ya Philharmonic ya Morocco tarehe 9 na 10 Desemba na tamasha la Kuzaliwa kwa Bwana kutoka  kundi la Kroatia la Klapa Armorin tarehe 17 Desemba. Kwa mwaka 2022, matukio yameandaliwa kwa ajili ya Juma la maombi  kwa ajili ya Umoja wa Wakristo ;  tarehe 22 Februari 2022, katika Sikukuu ya UKULU wa Mtakatifu Petro vile vile na Mwezi Machi kuadhimisha kumbu kumbu ya  ziara ya Papa Francisko nchini Morocco iliyofanyika mnamo mwaka 2019, pamoja na matukio ya mengine ya kijamii.  Mipango mingine ya kiutamaduni na kisanii itafanyika.

Kanisa kuu la Rabat
Kanisa kuu la Rabat

Maonesho ya picha  mbali mbali zikiwemo picha za zamani yameanzishwa katika Ukumbi wa Kanisa kuu la Mtakatifu Pietro, Rabat wakati, kwa mwaka mzima, katika taasisi ya kiekumene ya Kitaalimungu Al Mowafaqa, mahali pa malezi na mikutano ambayo inahamasisha mazungumzo ya kiutamaduni na kidini, makongamano yatafanyika. Iyanayojitika juu ya sanaa, historia na umuhimu wa Kanisa kuu. “Kuadhimisha miaka 100 ya Kanisa kuu lazima iwe ni tukio kwetu, la ajabu sana, kugundua tena kwamba sisi ni wa Kanisa zima, amesisitiza Kardinali Lόpez Romero katika barua yake kwa Jimbo kuu la Rabat, akiongeza kuwa mali ya Kanisa imeoneshwa kupitia ujuzi wa historia na watu, kwa kuhudhuria na kushiriki katika sakramenti na shughuli nyingine, kujitoa kwa huduma ya jumuiya za parokia, ushirikiano wa kiuchumi na kwa njia ya upendo”.

Kardinali Lόpez Romero anapendekeza hasa kufanya hija kwenye Kanisa kuu. Kwa kardinali, safari ya kweli ya kiroho kufanywa katika ngazi ya parokia, pamoja na familia yake, katika vikundi vidogo au mmoja mmoja. Askofu mkuu wa Rabat anapendekeza kuanza kwa wakati wa sala na kutafakari, ambayo inaweza kuendelea wakati wa safari, kusimama katika Kanisa kuu kwa safari ya kuongozwa na kumalizia safari katika Jumba la Upatanisho kwa sala ya pamoja na, kwa wale matakwa, kwa nasadiki. Kardinali  Lopez pia anatarajia, kujumuishwa katika hija, adhimisho la Ekaristi, kutia saini katika kitabu cha wageni na sadaka kwa ajili ya Kanisa kuu, na kuhitimisha anapendekeza kushiriki mlo na nyakati za kuishi kwa furaha pamoja.

Hatimaye, Kardinali Lόpez Romero anapendekeza  jambo la muhimu zaidi katika hija ni kukutana na Kristo, aliyepo katika Sakramenti Takatifu, lakini pia katika Neno la Mungu, katika upatanisho, hekaluni, katika mwanga wa mshumaa wa Pasaka; katika alama mbalimbali na zaidi ya yote katika makuhani na katika kila kaka na dada wakutana. Mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu walikuwa wamefungua hata Sinodi ya pili ya kijimbo iliyoongozwa na mada ya “Kwa sababu ya Yesu na Injili ni kanisa lipi la Morocco”. Hiyo ndiyo  moja ya mada ya jubilei na ambayo inapendekezwa kuendelezwa katika sinodi ya kijimbo ambayo inaendelea kwenye mchakato wa Sonodi ya miaka mtatu ambayo inatarajiwa kufanyika Sinodi ya Maaskofu Roma mnamo 2023.

19 November 2021, 17:31