Tafuta

Assisi:Ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika kinaonekana kikanisa kidogo 'Porziuncola'. Assisi:Ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika kinaonekana kikanisa kidogo 'Porziuncola'. 

Papa Francisko na maskini Assisi:Ndugu wadogo wanasema ni ishara ya udugu wa dhati

Hakuna aliye tajiri ambaye hana uhitaji wa mwingine na hakuna hata maskini hasiyeweza kutokuwa na lolote la kutoa.Kwa upande wa Mkuu wa Provinsi ya Umbria na Sardegna anasema hiyo ndiyo thamani ya ziara ya Papa Francisko kwa mara nyingine tena katika mji wa Umbria mahali ambapo atakutana na kikundi cha watu wenye kuhitaji kutoka Ulaya nzima katika matarajio ya siku ya maskini ulimwenguni tarehe 14 Novemba lakini Papa atakwenda Novemba 12.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Ni furaha kubwa katika mji wa Assisi walipotangaziwa kuhusu Ziara ya Papa Francisko katika Kikanisa Kidogo Porziuncola kilichomo ndani ya Kanisa Kuu la Bikira Maria wa Malaika, mnamo tarehe 12 Novemba 2021.  Mkuu wa Provinsi ya Umbria na Sardegna  Padre Francesco Piloni amesema ni kwa jinsi gani wanayo furaha kubwa na kusisistiza hasa shauku ya Papa ya kuonesha hatua hiyo ya kukutana na ndugu maskini. Ziara hiyo itakuwa ishara ya urahisi kwa mujibu wa padre huyo akikumbusha tabia ya kifaragha ambayo imeandaliwa na Baraza la Kipapa la kuhamasisha Uinjilishaji mpya, inayongozwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella.

Tayari katika eneno hilo, hivi karibuni katika kanisa kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika umesheeni utashi wa kutafsiri haraka shauku ya Papa katika tukio muhimu. Kiini chote hicho kuna uhusiano wa kila mtu, ambao unaalikwa hata umakini kwa mambo madogo na kwa namna ya pekee zawadi ndogo ambaye itatolewa na ndugu maskini katika ishara ya utambuzi, utunzaji na upole wa baba Mtakatifu.

Bado hazijatolewa taarifa rasmi jinsi siku itakavyokuwa, lakini Padre Piloni (OMF) ametafakari juu ya mada ya udugu ambayo ilichaguliwa mara moja na Baba Mtakatifu. “Hakuna tajiri hata mmoja  kwa namna ya kukosa mahitaji ya mwingine na hakuna maskini kwa namna ya kukosa chochote cha kutoa". Ni katika ujumbe ambao unatazama kila mmoja wetu kutokana na dharura ya kurudisha uhusiano wa kweli ambao katika nyakati zetu umepotea. Ikiwa hatuweze kuhusiana na shauku hiyo ya Mungu ya kidugu na mahusiano ya kweli , kuna hatari ya kuingia daima katika muundo wa dhambi ambao unaitwa ubinafsi na huo kiukweli ndiyo virusi vya ajabu leo hii amefafanua Padre Piloni.

Kwa upande wa Padre Piloni, vile vile amesema Papa Francisko ana moyo wa tasaufi ya Mtakatifu wa Assisi kwa namna maalum  katika Sura  ya Tisa ya Kanuni  ya Kifransiskani. Katika sura hiyo inasomeka kuwa:  “ndugu wanapaswa kufurahia wanapoishi na watu wengine ambao hawahesabiwi na kudharauliwa”. Lakini  ameongeza kusema si katika kufurahia  kutembea nao kama ambavyo itakuwa na maana ya ziara yake hiyo.  Badala yake padre anasema kwa upande wa familia ya Ndugu wadogo  kuna hata sehemu ile ndogo sana iitwayo Porziuncola ambayo inakumbusha maisha aliyoishi mtakatifu wa Assisi hadi miisho ya dunia.

Maono ambayo yanarudishwa nyuma mnamo Oktoba 2013 wakati Papa Francisko alipokwenda kwa mara ya kwanza huko Assisi na wakati alipotoka kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria wa Malaika aliwambia umati wa watu kwamba alihisi neno moja tu wakati wa sala katika kikanisa kidogo sana kiitwacho Porziuncola: "Injili, Injili, Injili!" Ameongeza kusema Padre Piloni hayo ni maono ambayo yabatabaki tena zaidi katika moyo wake hata mara baada ya ziara yake ijayo kwa sababu ni moja ya Injili ya nguvu zaidi ambayo inatazama walio wadogo, maskini, wale wasiojiamini kama ni watu, lakini wanaofanya maisha yao kuwa na uwezekano wa kukutana nao. 

19 October 2021, 16:09