Tafuta

Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Gambia, Liberia na  Sierra Leone, katika picha ya pamoja na Papa  walipokuwa katika ziara yao ya kitume jijini Vatican. Maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Gambia, Liberia na Sierra Leone, katika picha ya pamoja na Papa walipokuwa katika ziara yao ya kitume jijini Vatican. 

Liberia:Jengo la Sekretarieti katoliki limeungua Moto

Hivi karibuni,Jengo la Sekretarieti ya Baraza la Maaskofu nchini Liberia liliungua moto.Mkurugenzi wa Shughuli za Kimisionari za Kipapa Kitaifa (PMS)ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Liberia ameomba kusali kwa ajili yao wote.

Na Sr. Angella. Rwezaula – Vatican.

Hivi karibuni mnamo tarehe 19 Oktoba 2021, majira ya saa 4.30 asubuhi, motou katika Jengo la Sekretarieti  Katoliki kitaifa ya Baraza la Maaskofu nchini Liberia(CABICOL). Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Baraza , Padre Dennis Cephas Nimene, aliliambia shirika la habari za kimisionari Fides kuwa moto uliunguza paa la chumba chake wakati ambamo walikuwa wote wanafanya kazi katika ofisi zao. Walifanya kila njia kutaka  kuuzima moto kwa upande wa wafanyakazi wao lakini, walishindwa hadi  kusubiri wazima moto  (LNFS), lisaa limoja baadaye, ameeleza Padre huyo ambaye pia ni Mkurugenzi kitaifa wa shughuli za Kipapa za kimisionari PMS nchini Liberia.

Ndani ya jengo hilo, ambalo pia ni makao ya PMS hawakuweza kukomboa chochote kama vile Hati mbali mbali, ( darija na ripoti, vimeharibiwa na moto) vikiwemo pamoja na vitu  binafsi, kama vile vitabu na nguo za Padre huyo. Kwa sasa wanasubiri taarifa kutoka katika kitengo dharura cha Kitaifa cha Wazima Moto ili kujua sababu iliyopelekea moto huo na Katibu Mkuu wa Baraza la maaskofu kwa sasa amekaribishwa kwa Watawa wa Ndugu wa Mtakatifu Yohane wa Mungu ambao  wanatoa huduma zao katika Hospitali katoliki na yeye kushirikishana nafasi ya kazi katika Ofisi ya Caritas ya Liberia.

Hata hivyo siku iliyofuata, baada ya moto kwa mujibu wa maelezo yake walifika watu wengi na miongoni mwake: Balozi wa Kitume nchini Liberia, Askofu Mkuu Dagoberto Campos Salas, na Askofu Mkuu mstaafu Lewis Zeigler wa Forontoniana na msimamizi wa jimbo, Gabriel Blamoh Jubwe, ili kutathimini, uharibifu  huo na kuonesha ukaribuna mshikamano  kwa watu wote wanaofanya kazi katika Sekretarieti kuu.  Aidha watu wengi waliwapigia simu kuonesha ukaribu na miongoni mwao ni Askofu Anthony Fallah Borwah wa Gbarnga, Askofu Andrew Jagaye Karnley wa Cape Palmas, na amehitimisha maelezo yake akiomba wawaombee katika janga hili lililowapata.

25 October 2021, 15:24