Tafuta

2021.10.11:Nembo ya Juma la 49 la Kijamii katoliki,Italia 2021. 2021.10.11:Nembo ya Juma la 49 la Kijamii katoliki,Italia 2021. 

Juma la 49 la Kijamii katoliki,Italia 21-24 Oktoba huko Taranto

Katika Juma la 49 la kijamii katoliki, Italia kuanzisha 21 -24 Oktoba huko Taranto linaongozwa na mada 'Sayari tunayotegemea.Mazingira,kazi na wakati ujao.#vyotevimeunganika”.Katika Juma hilo watazungumzia hata hali halisi ya fadhila iliyotolewa kwenye waraka wa Laudato si’ wa Papa Francisko,kuwa na matarajio ya ikolojia fungamani katika nyanja ya ujasiriamali,usimamizi,jumuiya na wafanyakazi.

Na Sr. Angella Rwezaula- Vatican.

Kwa mtazamo ambao unathibitisha hali halisi kama zawadi na siyo jambo la kurarua, hadi mfupa na baadaye kuharibiwa. Askofu Mkuu Filippo Santoro, wa jimbo Kuu katoliki la Taranto, Italia ameeleza mtazamo  wake kuhusu tafakari ya Mtakatifu Francis wa Assisi ambaye naonekana sana katika Waraka wa Laudato si kama kituo cha kuunzia kwenye fursa ya  Wiki ya 49 ya Jamii ya Wakatoliki nchini Italia ambayo pia itazungukia ndani ya mwongozo wa Waraka mwingine wa Fratellii tutti.  Wiki hiyo inatarajiwa kuanza tarehe 21 hadi 24 Oktoba 2021 ambapo zaidi ya maaskofo 140, wawakilishi 670 wa majimbo 218, wataalam, wajumbe wa ulimwengu wa kisiasa, raia, na utamaduni wazungmzia mada kuhusu “sayari ambayo tunatajaria. Mazingira, kazi, wakati ujao. # vyote vinaunganika” kwa lengo la kutafakari kwa kina juu ya mtindo mpya wa maendeleo na juu ya kuanzisha mpito wenye maono ya matarajio ya ikolojia fungamani.

Rais wa kamati ya kisayans ya kuandaa Wiki ya Kijamii, walikutana hivi karibuni huko Bari katika fursa ya jukwaa la mafunzo katoliki kwa ajili ya kulinda Kazi ya uumbaji, iliyoandaliwa na  Greenaccord, ambapo amekumbusha jinsi ambavyyo toleo la Wiki ya kijamii iliyofanyika kabla ya janga la mnamo  2017  huko Cagliari, Italia  ilikuwa inaongozwa na mada “ kazi ambayo tunataka”. Kwa upande wake anasema, kazi na mazingira, ni mada ambazo zinaunganika pamoja, ni mada kuu ambazo tunaishai kwa namna ya pekee katika hali halisi inayofanya kuteseka kwa Taranto, katika masuala kwa mfano wa kiwanda cha zamani cha ILVA cha Taranto kilochokuwa katikati ya mitaa ya Tamburi na katika uchafuzi wa mazingira ambayo yamesababisha vifo vingi sana  vya watoto  na watu wazima na kusababaisha matokeo ya matatizo hata katika kazi.  Amesisitiza kwamba umefikia wakati sasa  wa kuonesha zaidi jinsi ambavyo ni lazima  uwe mwisho na kusema inatosha kuharibu mazingira. Kuna mambo mengi ambayo yanaungana hasa kwa ubunifu wa kiteknolojia  wa kubadilisha mzunguko wa makaa ya mawe na vyanzo mbadala, kama vile gesi, na hidrojeni. Na kwa pesa za Mpango wa Kufufua haya yote yanawezekana ni muhimu kwa huduma ya afya, ambayo ni nzuri kwanza na kwa utunzaji wa kazi, ambayo inahitajika kudumisha maisha.

Katika tukio la huko Taranto, ambalo linataka kuwa safari ya watu kama inavyoelekeza kitendea kazi , kuna masuala ambay yamekabiliwa na jumuiya ya kanisa ya italia. Askofu Mkuu Santoro amezungumza kwa kazi kubwa ya kisinodi ambayo inaandaliwa kwa kushirikiana na vijana wa Economy of Francesco, semina na mikutano ambayo wameweza kukabiliana pamoja na mengine udhaifu ulioo katika eneo, masuala ya sheria na mambo ya uhalifu wa kimafia, mantiki ya mpito wa kiikolojia , mchango  wa viwanda na kazi , kwa lengo la wema wa pamoja. Aidha wameweza kutoa tathmini ya idadi kubwa ya mazoezi mazuri ya wajasiliamari, waratibu, jumuiya na watu. Biashara nyingi, usimamizi, jamii na 'mazoea mazuri' pia yamechunguzwa na kupangwa ramani, ili kupiga picha  ya dhamira thabiti ambayo tayari inaendelea. Baadhi ya hayo ya karibu zaidi na mji mkuu wa Ionio, watautembelewa", kwa mujibu wa maelezo ya Padre Antonio Panico, makamu askofu Mkuu  wa Jimbo kuu la Taranto kwa ajili ya  jamii na ulinzi wa kazi ya uumbaji, na ambaye ni mmoja wa wasimamizi wa Juma la 49 la  Kijamii.

Ni ukweli mzuri ambao  unawakilishwa na utajiri wa sasa kutoka katika  mtazamo wa bioanuwai, wa kupona kwa uzuri katika eneo hilo, labda wakati mwingine hata na uzuri wa kuona watu wengi wameajiriwa katika eneo ambalo bado linakabiliwa na uhaba wa kazi: Takwimu za  Italia (Istat) za mwaka 2020 zinazungumzia juu ya kiwango cha ukosefu wa ajira cha asilimia 14% huko Puglia, Italia. Huo ni ukweli ambao unaonesha jinsi uendelevu katika aina zote umetoa ajira na hata utajiri kidogo. Zinatakiwa kwenda kwenye uendelezaji wa Mar Piccolo ya Taranto ambayo ni wilaya ndoyo iliyotengenezwa kwa nguvu zaidi na  Martina Franca, kutoka kampuni ya Ginosa ambayo inazalisha mbolea kwa njia ya asili hadi kufikia safari ya kilomita 12 za uchungu wa bonde la Laterza. Na sio tu hilo. Miongoni mwa ziara zilizopangwa, pia ni ile ya Masseria Fruttirossi huko Castellaneta. Katika Juma la Kijamii, Padre Panico amesisitiza, kwamba wanataka kuwa na  wafuasi wa mazoea mazuri pia. Kwa kampuni ya Castellaneta ya De Lisi inaendelea mbele, uendelevu huo unaweza kuunganishwa katika mazingira, kiuchumi na kwa hivyo pia kijamii, ikionesha jinsi ya kufanya kazi katika eneo, hasa eneo la Taranto, ambalo tasnia kubwa, hata nzito,  daima imekuwa bwana kidogo: kwa maana  hiyo wanapozungumza juu ya uchumi wa kijani, wanaweza kuonesha kilimo chenye afya na endelevu kinachoweza kutengeneza mapato na ajira, amebainisha.

19 October 2021, 15:54