Tafuta

2021.07.21 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini  Slovakia: Na Maria na Yosefu katika njia ya kuelekea kwa Yesu 12-15 Septemba 2021.07.21 Nembo ya Ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Slovakia: Na Maria na Yosefu katika njia ya kuelekea kwa Yesu 12-15 Septemba 

Slovakia:Maandalizi ya hija ya Papa nchini Slovakia yapamba moto!

Tangu Jumatatu tarehe 6 Septemba 2021 watu wa Slovakia wanapaswa kujiorodhesha kwa njia ya mtandao katika vitengo ambavyo vitakuwa vimetengenezwa kwa ajili ya wale walio na chanjo ili kuudhuria mikutano na Papa Francisko katika ziara yake ya Kitume. Hayo yalitangazwa mnamo tarehe 4 Septemba na timu ya maandalizi ya ziara nchi humo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika maandalizi ya ziara ya Papa Francisko nchini Slovakia yamepanda moto ambayo yanaongozwa na kauli mbiu: Na Maria na Yosefu katika njia ya kuelekea kwa Yesu” , tarehe 12-15 Septemba, lakini kitu cha kwanza ni kufuata itifaki ya kuzuia maambukizi na kwa maana hiyo itakuwa ni watu walio na ‘Kadi ya kijani’(Green card) ambao wataweza kuingia kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwa mikutano na Papa. Tangu Jumatatu tarehe 6 Septemba 2021. watu wanapaswa kujiorodhesha kwa njia ya mtandao katika vitengo ambavyo vitakuwa vimetengenzwa kwa ajili ya wale walio na chanjo. Hayo yalitangazwa mnamo tarehe 4 Septemba na timu ya maandalizi ya ziara ya Papa nchini humo.

Uthibitisho wa waandishi wa habari ulifanyika mnamo tarehe 31Agosti unabainisha kuwa: Waandishi wa habari 580 wamedhibitishwa, kati yao 80 watakuwa katika ndege ya Papa. Kutoka Slovakia karibu waandishi wa habari ni 400 na kutakuwa na watu 3 wa Slovakia kwenye ndege hiyo ya Papa, wanaowakilisha ofisi mbili za wahariri jijini Vatican. Kati ya wapiga picha 110 walioidhinishwa, wapiga picha wapatao mia, kwa mujibu wa Habari zilitolewa na mkurugenzi wa Ofisi ya Wanahabari wa Baraza la Maaskofu wa Slovakia, Padre Martin Kramara alisema kuwa  watu wa kujitolea wapatao 3,000 walijiandikisha kwa tukio hilo  kubwa.

Hata hivyo tangu Agosti 30 kulikuwa na washiriki 46,000 waliokuwa wamesajiliwa kati yao 30,000 kuwa katika  misa kwenye uwanja wa Šaštín, na bado wanaendelea kujiorodhesha. Vile vile kuna Mpango wa kiroho baada ya ziara ya Papa  ya kwenda huko Šaštín tangu siku ya ziara ya Papa tarehe  15 Septemba watakuwa na siku tisa za sala  na kufunga kwa ajili ya makuhani ambao ni mpango wa harakati ya ‘Modlitby kňazov’  inayhusi 'Maombi ya mapadre', ambao utafungwa mnamo tarehe 23 Oktoba kwa Hija ya Kitaifa ya makuhani kwenda Šaštín.

Kwenye Uwanja wa Mpira wa  Košice-Lokomotíva wataiba  wimbo wa mkutano wa Papa na vijana, utakaongozwa na kauli mbiu “Tuinue Ulimwengu” na waimbaji Sima Magušinová na Martin Husovský na Zbor wa kwanya ya Mtakatifu Cecilia na bandi nzima Mji wa Košice utakaotembelewa na Papa mnamo tarehe 14 Septemba 2021 huko tayari umeandaa mpango wa kiutamaduni kwa raia katika eneo la kituo cha kihistoria cha jiji la Hlavnà ulica kuanzia Jumapili tarehe 12 Septemba. Tamasha katika roho ya sanaa takatifu, na ukumbi wa michezo wa Rom Haliganda, maonesho ya bandi  ambao ni waimbaji kutoka vikundi mbali mbali vya wasanii. Siku ya ziara ya Papa kutakuwa na skrini kubwa katikati mwa jiji, kwa maana ya ufikiaji hautakuwa na masharti  kadi  ya kijani ya Uviko-19  ili kutoa  uwezekano wa kufuatilia ziara ya Papa pamoja kwa watu ambao kwa sababu tofauti hawajapata chanjo na shirika la Reli ya Slovakia litaongeza treni 95 zaidi katika siku za ziara ya Papa.

06 September 2021, 16:08