Tafuta

Askofu Mkuu  Stanislav Zvolenský, wa Jimbo Kuu Katoliki la  Bratislava nchini Slovakia Askofu Mkuu Stanislav Zvolenský, wa Jimbo Kuu Katoliki la Bratislava nchini Slovakia 

Askofu Mkuu wa Bratislava:umoja na matumaini,matunda la safari ya Papa

Askofu Mkuu Stanislav Zvolenský,rais wa Baraza la Maaskofu wa Slovakia,amerudia kuelezea hatua na maana kubwa ya ziara ya hivi karibuni ya Papa Francisko nchini mwao.

Na Sr. Angela rwezaula – Vatican.

Ziara ya kitume ya Papa Francisko nchini Slovakia imepelekea kuwatia moyo watu wa Mungu wote  na ujumbe mwingi wa kina, kwa mfano ni katika liturujia ya Mungu ya kibizantina ambayo ilikuwa ni katika siku kuu ya ‘Kukutuka kwa Msalaba’, na baadaye katika madhahabu ya kitaifa ya mama Maria wa mateso saba huko Šaštín, ambapo ilikuwa ni katika fursa ya siku kuu ya ‘Bikira Maria wa Mateso’.  Huu ni ujumbe kwa hakika wa matumaini katika mateso na ambapo unaweza kuthibitishwa katika kipindi maalum hiki ambacho ulimwengu unaishi. Kumekuwapo na mkutano wa vijana, wa maaskofu, waseminaristi, watawa, makatekista, lakini pia kila mkutano wameweze kuishi na baba Mtakatifu ambaye amewapelekea ujumbe wa matumaini kwa waamini na wasio waamini na kwa maana hiyo kwa jamii nzima ya Slovakia.

Amethibitisha hayo  kwa shukrani kubwa, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Slovakia Askofu Mkuu Stanislav Zvolenský wa jimbo kuu katoliki la Bratislava. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa Kanisa la Slovakia katika mahojiano na waandishi wa habari Vatican News amesema katika mkutano huo kwa dhati Papa umekuwa ni zawadi ya kiroho. Baba Mtakatifu kwa upendo mkuu na unyenyekezo alisema kuwa yeye yuko katikati yao kama mhudumu wa umoja. Kwa mana hiyo haya maaskofu wenyewe wenye ni watu ambao ni udhaifu, na dhambi zao na hata matatizo yao walikuwa na haja ya kuwa na Mchungaji mkuu katikati yao. Kwa maana hiyo katika misa kwenye Kanisa kuu kwenye madhahu ya Mama Maria, maaskofu 19 waliweza kusali a Papa Francisko kwa mama Maria wa Mateso saba. Kwa mujibu wa Askofu mkuu amethibitisha kuwa kila baraza kwa hakika alikuwa na sababu na umuhimu wa kusali kwa ajili ya umoja wa maaskofu. Wao waliweza kupata furaha hiyo, zawadi hiyo, na furaha ya kisali pamoja na Baba Mtakatifu kwa ajili ya muungano pia wa maaskofu kati yao, amebainisha Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Slovakia.

Baba Mtakatifu Francisko aliwa tia moyo ili kutembea na siyo kusimama na kwa maana hiyo ni zile nguvu ambazo zinawapa matumaini ya wakati ujao ambao ni vijana. Huko Košice kulikuwa na mkutano na vijana. Hapo waliweza kuishi tumaini la kuona vijana, kusikia ushuhuda wao; walisika hata majibu ya Baba Mtakatifu,kwa maswali yao. Tumaini hili linaweza kuthibitishwa hata na Baba Mtakatifu na aliona mustakabali wa jamii na Kanisa kutoka kwa vijana na watoto.

Mkutano huu uliwakilisha uwepo wa vijana ambao walielewa ujumbe wa Injili na wanataka kuishi. Katika ushuhuda, mwingine walisema kwamba walikuwa wameongoka. Baadaye kijana mmoja akasema jambo kubwa: “Nimeongoka, lakini maisha yangu yote sasa nataka kuishi kwa mujibu wa ujumbe wa Injili”. Ushuhuda ulikuwa wenye hisa kali kwa maana hii. Lakini hii ndiyo tumaini kwa Kanisa, alisistiza Askofu Mkuu wa Bratislava mara baada ya ziara ya Papa Francisko iliyotimishwa hivi karibuni.

17 September 2021, 14:43