Tafuta

Jinsi gani ya kudumisha Ikolojia fungamani? Jinsi gani ya kudumisha Ikolojia fungamani? 

Marekani:Siku ya utunzaji wa kazi ya uumbaji,inahitajika dhamiri ya ikolojia

Kiukweli kuna changamoto ambazo jamii inapaswa kukabilianaleo hii:janga la UVIKO-19,ulinzi wa maisha,vitisho kwa demokrasia na ulinzi wa kazi ya uumbaji.Ni ujumbe wa Baraza la Maaskofu Marekani katika Siku ya Dunia ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira sambamba na maadhimisho ya Kipindi cha Kazi ya Uumbaji Septemba 1 hadi 4 Oktoba.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kukuza dhamiri ya kiikolojia ambayo inatuwezesha kuona wazi, kuhukumu kwa usahihi na kutenda kwa maadili linapokuja suala la utunzaji wa, ndiyo onyo lililotolewa na Baraza la Maaskofu wa Marekani (Usscb), linalifungamana kwenye ujumbe wa Siku ya Dunia ya Kuombea Utunzaji Bora wa Mazingira sambamba na maadhimisho ya Kipindi cha Kazi ya Uumbaji kilichoanza tarehe 1 Septemba hadi tarehe 4 Oktoba ya kila mwaka katika siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi mpenda kazi ya uumbaji halisi. Katika hati hiyo, iliyosainiwa na Askofu Mkuu Paul S. Coakley, rais wa Kamati ya Haki za Ndani na Maendeleo ya Binadamu, na Askofu David J. Malloy, rais wa Kamati ya Haki na Amani ya Kimataifa, waamini wamehimizwa kuchukua njia ya kuelekea dhamiri ya ikolojia iliyokomaa, yenye huruma na inayowajibika ambayo inaweza kutathmini na kushughulikia shida za mazingira kwa njia ya kati badala ya pembezoni”.

Kwa hakika kuna changamoto ambazo jamii inapaswa kukabiliana leo hii kama vile: janga la UVIKO-19, ulinzi wa maisha, vitisho kwa demokrasia na kwa dhati, ulinzi wa kazi ya uumbaji, maaskofu wa Marekani wanaelezea.  “Ole wetu, ikiwa tutatenganisha kilio cha maskini na kilio cha dunia”, wanaonya. Kwa hivyo, mwaliko wao ni wa kutafakari kwa uangalifu na kwa mtazamo wa imani juu ya Ripoti ya sita ya hivi karibuni ya Kamati ya Serikali ya Umoja wa Mataifa ya Mabadiliko ya Tabianchi, ili kufungamanisha sayansi bora inayopatikana na ukweli wa imani Katoliki, ili kuimarisha dhamiri kiikolojia.

Katika suala hili, maaskofu wa Marekani walisisitizia mambo muhimu ambayo yalitoka kwenye Ripoti hiyo: la kwanza wanasema kwamba hali ya hewa inaathiriwa na shughuli za kibinadamu na kwamba hatujafanya vya kutosha kubadili mwelekeo. Kwa hakika tuko bado tuko nje ya njia, ili kufikia malengo yaliyowekwa na Mkataba wa Paris, ambao unapaswa kuweka joto la joto chini ya digrii 2 za Celsius. Kwa maana hiyo, lazima tuchukue hatua kwa ujasiri na haraka, pia kwa mtazamo wa mkutano ujao wa Umoja wa Mataifa juu ya hali ya hewa (COP 26) utakaofanyika huko Glasgow nchini Scotland, Novemba ijayo. Mkutano huu unawakilisha fursa kwa nchi kuwa na ujasiri zaidi katika ahadi zao za kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kwa hivyo kuweza kutazama siku zijazo kwa matumaini. Pia kwa sababu na huu ni ukweli mwingine ulioibuka kutoka kwa Ripoti hiyo ambao matukio yanayowezekana zaidi yanaonesha hali ya tabianchi thabiti, hata ikiwa ni ya joto.

Kwa kutambua, kwamba wanaume na wanawake wameitwa kuwa wasimamizi, na sio wamiliki, wa kazi ya Uumbaji waliokabidhiwa na Mungu, Baraza la Maaskofu Marekani (Usccb) linawaalika waamini kusali kwa ajili ya wanasayansi wote wa masuala ya hali ya hewa, wataalam na wale walio mstari wa mbele katika masuala hayo kupunguza na kurekebisha. Katika Bunge la Marekani, hasa, maaskofu wanao, na kufanya kazi kwa kushirikiana na kwa ujasiri ili kushughulikia shida za mazingira kwa msisitizo juu ya uwekezaji katika miundombinu na kutekeleza wa sera kabambe za tabianchi, kuchochea ugwiji na maendeleo ya uchumi wa kitaifa na kimataifa. Maombi zaidi yanatolewa hasa kwa mkutano wa COP26, kwa ajili ya viumbe vyote na watu walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi na kwa maskini zaidi na wahitaji zaidi, lakini mambo zaidi kila wakati yakiambatana na utekelezaji wa dhamiri ya kiikolojia ya dhati, wanasisitiza Maaskofu hao.

03 September 2021, 15:40