Tafuta

Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu Kardinali Peter Turkson Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu 

Ghana:Kard.Turkson atuzwa kwa jitihada ya haki,amani na mshikamano

Mfuko wa Milenia ya Ubora,nchini Ghana,imetunukia tuzo kwa kuheshimu kazi ya Kardinali Peter Appiah Turkson,Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu.Tuzo za Ubora wa Milenia hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitano kwa taasisi au watu binafsi ambao wanachangia maendeleo ya kitaifa.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican.

Tuzo maalum kwa ajili ya jitihada maalum, inayotekelezwa kila wakati kwenye masuala msingi kama vile kulinda haki na amani, utatuzi wa ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kuhamasisha mshikamano wa ulimwengu, ndivyo iliyofafanuliwa na Mfuko wa Milenia ya Ubora, nchini Ghana, kwa kuheshimu kazi ya Kardinali Peter Appiah Turkson, ambaye ni mzaliwa wa nchi hiyo na  Rais wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo  Fungamani ya binadamu.  Tuzo hiyo ametunukiwa Kardinali wakati wa sherehe rasmi iliyofanyika mnamo tarehe 26 Agosti jijini Accra, katika Chuo cha Sayansi na Sanaa.

Katika afla hiyo, Kardinali Turkson alitoa mhadhara, ambao ulianza na maneno mawili muhimu: uhuru na haki, ambayo sio kwa bahati upo katika kauli mbiu ya kitaifa ya nchi ya Ghana. Ili kuelewa dhana hizi alisema kardinali – kuwa nchi lazima ihakikishe kuhamaisha hadhi ya  binadamu kwa raia wake wote. Uhuru, kwa hakika huruhusu watu kuishi maisha yenye hadhi, wakati haki inakaribisha kila mtu kuishi katika ufahamu kwamba sisi ni viumbe wenye  uhusiano. Mahitaji ya wengine, kwa maana hiyo, alielezea Kardinali lazima yaheshimiwe, kwani hii inamfanya mtu kuwa

Wakati huo huo, Kardinal Turkson aliwasihi Waghana wasipoteze mtazamo wa wema na ustawi wa wote wa nchi: “Ikiwa baba waanzilishi wa Ghana walichagua 'Uhuru na haki' kama kauli mbiu yao ya kitaifa  ina maana ​​walijua wanachokizungumza , yaani, walitaka kuturuhusu kukuza na kuishi hadhi yetu”. Njia ya juu zaidi ya haki, kwa hakika ni ile ambayo inaona uhamasishaji na kukusa uhuru kwa kuunga mkono wengine, kwa heshima kamili ya mahitaji yao. Hatimaye kutoka kwa Kardinali Turkson alitoa woto wake kwa wote wote, ili kuepuka maradhi kama vile ufisadi na ulaghai, ili kuleta haki kati yao.

Mfuko wa Milenia ya ubora ni shirika lisilo kiserikali lililoanzishwa mnamo 1998 na Ashim Morton: mjasiriamali na mbunifu kwa taaluma, mtu huyo aliishi kwa miaka kadhaa huko Marekani na aliporudi Ghana akachangia maendeleo ya nchi. Kama shahidi wa kila wakati wa shida na kesi za utawala mbaya hazipo tu nchini Ghana, lakini katika bara lote la Afrika, Morton ameamua kubadilisha dira hasa  akitoa mwangaza, kutokana na biashara zilizofanikiwa na kuwapa nafasi watu ambao, kwa kujitolea, zinaleta mabadiliko mazuri katika eneo lote. Tuzo za Ubora wa Milenia hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitano kwa taasisi au watu binafsi ambao wanachangia maendeleo ya kitaifa.

03 September 2021, 16:31