Tafuta

2021.09.02 Monsinyo Julius Agbortoko Agbor, Msimamizi wa Jimbo la Mamfe ameachiwa huru nchini Cameroon. 2021.09.02 Monsinyo Julius Agbortoko Agbor, Msimamizi wa Jimbo la Mamfe ameachiwa huru nchini Cameroon. 

Cameroon:Monsinyo Julius Agbortoko Agbor ameachiwa huru

Dominika 31 Agosti ameachiliwa huru Mosinyo Agbor wa jimbo la Mamfe nchini Cameroon aliyekuwa ametekwa nyara jana yake.Taarifa zimethibitishwa na Kansela wa Jimbo hilo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Padri wa jimbo katoliki la Mamfe, kusini magharibi mwa Camroon  aliachiliwa bila kulipa fidia na alikuwa ametekwa nyara siku ya Jumapili tarehe 29 Agosti. Taaifa hii imetangazwa tarehe 31 Agosti 2021  na Kansela wa Jimbo huko Cameroon, Padre Sébastien Sinju.

“Tunamshukuru Aliye Juu Zaidi aliyemweka Monsinyo Julius Agbortoko Agbor kuwa salama wakati wa kifungo chake na kumrudisha kwetu salama salimini”, inasema taarifa hiyo  iliyosainiwa na Padri Sinju, ambaye alinukuliwa na Shirika la Habari za kimisionari Fides. Kansela ameshukuru jumuiya za Kikristo na wale wote ambao, wakiwa nyumbani na nje ya nchi, walikuwa nao bega kwa bega wakati wanaunganika katika maombi. Na kwamba Mungu wabariki.

Kwa kuachiliwa kuhani huyo, watekaji nyara walikuwa wameomba fidia ya faranga milioni CFAi 20 (kama euro 30,489). Inavyoonekana hata hivyo jumla isingeweza kulipwa. Monsinyo Agbortoko Agbor alikamatwa na kutekwa nyara Jumapili tarehe 29 Agosti 2021 na baadhi ya vijana wenye silaha, ambao walikuwa wamehitimu kama watenganishaji, na  ambao walikuwa wameshambulia seminari kuu ya Mamfe. Kusudi lao, kwanza lilikuwa kumnasa Askofu Francis Teke Lysinge, Askofu Mstaafu wa jimbo la  Manfe. Lakini kutokana na uzee wa Askofu huyo, wahalifu hao walipendelea kumuondoa msimamizi wa jimbo hilo Monsinyo Agbor.

02 September 2021, 15:16