Tafuta

Kongamano la Ekaristi kimataifa huko Budapest Kongamano la Ekaristi kimataifa huko Budapest 

Budapest:Kard Yeom Soo-jung,kuwa makini na mapinduzi ya anthropolojia

Katika katekesi ya Kongamano la Ekaristi kimataifa,Budapest,Kardinali Yeom Soo-jung wa jimbo la Seuol amebainisha juu ya mapinduzi ya anthropolojia ambayo hutuzingira na ambayo maadili yake ni kinyume na ya Kikristo.Kardinali Dominik Duka,Askofu Mkuu wa Praga alisema kilio kinachohitaji msaada kinatoka jamii tajiri,lakini ambacho kinakaribia hali ya jamii maskini.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Amani na upatanisho kati ya Kaskazini na Kusini, mashambulio ya maadili ya utamaduni na kwa familia, nguvu kubwa ya mtandao ndiyo mambo muhimu aliyojikita nayo Kardinali Andrea Yeom Soo-jung, Askofu Mkuu wa Seoul na Msimamizi wa Kitume wa Pyongyang, wakati wa kutoa katekesi yake katika Kongamano la Ekaristi huko Budapest nchini Hungaria, ambalo limehitimishwa na Baba Mtakatifu Francisko Dominika tarehe 12 Septemba 2021 kwa adhimisho la Misa Takatifu.  Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Soom –Jung alisema “ Dhana ya mtu, umuhimu  wake na utakatifu  unabadilika, pamoja na maana ya maisha na familia. Ni mapinduzi ya anthropolojia ambayo hutuzingira ambayo maadili yake ni kinyume na yale ya Kikristo”.  Kwa kuongezea kwa kutoa mifano halisi amesema “Ishara za mabadiliko haya ya anthropolojia ni ongezeko kubwa la talaka na utoaji mimba, euthanasia na, hivi karibuni, nafasi nyingine iliyopewa katika maisha ya umma na pia ile iitwayo itikadi ya ‘jinsia’. Hali hii inaleta mkanganyiko mkubwa kwa vijana, kwa sababu inawasilisha jinsia ya kijinsia ya kiume na ya kike, sio kama ukweli wa kibaolojia, lakini kama jukumu la kijamii linaloweza kubadilishwa kwa uhuru. Kiukweli mambyo haya ni ambayo kwa miaka 30 iliyopita vingeonekana kuwa vya kipuuzi, na leo vinaunda maisha yetu kiajabu”, ambainisha Kardinali.

Naye Kardinali Dominik Duka, Askofu Mkuu wa Praga katika katekesi nyingine pia alisema kilio kinachohitaji msaada kinatoka katika jamii tajiri, lakini ambacho kinakaribia hali ya jamii maskini kama vile: “Kongamano letu la Ekaristi linafanyika katika hali ambayo sisi ni mashuhuda wa mapambano ya kinyama ya kutovumilia katika mabadiliko ya ustaarabu wetu. Kanuni msingi zilizozaliwa katika utoto wa utamaduni wa wanadamu, kwenye makutano ya Afrika, Asia na Ulaya, katika nchi ya asili ya Yesu Kristo, zinakataliwa na kubadilishwa na maadili, ambayo ni kificho tu cha maoni ya Umaksi, Ummao, wapinga dini”.  Kwa maana hiyo hizi ni itikadi zinazokataa ukweli wowote, kwa maana hiyo hata Ukweli hubadilishwa na itikadi mbaya, iliyolazimishwa nao”. Hawa hutumia mara nyingi kwa madhumuni haya njia za kizamani  na kupigana na silaha, njia za ahadi za uongo kwa lengo la kisiasa au kutaka kufikia upendeleo binafsi, lakini pia silaha za kisasa, pamoja na habari za mbaya  kupitia vyombo vya habari. Silaha hizi ni silaha mbaya na wengi wana wasiwasi kuwa hazishindwi.

Tunajua, hata hivyo, kwamba maneno ya Ukweli wa milele hayashindwi, alisema, kwa sababu ukweli kila wakati hugundua wahusika, wanaoiga”. Kwa maana hiyo kusudi la Kongamano la Ekaristi liko wazi: Tafakari yetu juu ya Ekaristi katika Kongamano la Ekaristi la Kimataifa ni sehemu ya liturujia ya Kanisa. Kanisa sio taasisi tu, au, kama tunavyofikiria, shirika la kisiasa, kiitikadi, au labda kiuchumi. Ekaristi haifikiriwi bila Mungano wa wa Kanisa, wa mashahuda wa Yesu. Ekaristi ina mwelekeo wa ulimwengu wote, hatua yake inapita zaidi ya Kanisa, ubinadamu, wote walio hai na waliokufa, inajumuisha viumbe vyote. Kanisa ambalo linaweza kuvutia kwa mwanadamu leo ​​ni Kanisa la Ekaristi”.

Jambo muhimu katika suala hili ni dhana kwamba katika Kongamano la Ekaristi jijini Budapest la mnamo 1938, Askofu Mkuu wa Zagreb wakati huo, leo hii ni Shuhuda  mwenyeheri Alojzije Stepinac, alifanya mbele ya hatari ya vita iliyokuwa ikiandaliwa, iliyopendekezwa tena na Kardinali Bozanic. Yeye alisema: “katika siku hizi za kutisha, ambazo jamii ya wanadamu inaishi, tunaamini kabisa, kwa uthabiti zaidi kuliko hapo awali, kwamba kuna Upendo wa nguvu zote, ambao una uwezo wa kuunganisha watu wote katika familia kubwa na yenye furaha. Huu ndio upendo wa Kristo katika Ekaristi Takatifu Zaidi. Imani hii katika Upendo wa mwenyezi Mungu inatuleta pamoja leo hii kutoka sehemu zote za ulimwengu ....

Ekaristi Takatifu ni kifungo cha dhahabu cha upendo, kinachomuunganisha mtu na Mungu na mataifa .... Sisi Wakatoliki tunaamini katika hili. Tunaamini na kwa sababu hii tunarudia kwa maneno kamili ya imani ya Mtakatifu Yohane Mtume: 'Nos credidimus caritati, quam Deus habet in nobis'(A. Stepinac, Mahubiri katika Kongamano la Ekaristi huko Budapest mnamo 27 Mei 1938). Ushuhuda wa Rais wa Jamhuri ya Hungaria ulimalizika na kusadikika kwamba kumtafuta na kumkubali Mungu kunahitaji shughuli halisi, haiwezi kuwa hatua tu. “Sisi sote tunapokea ishara zetu, na ni juu yetu kuzichukua kama historia rahisi au fumbo. Ni juu yetu kuiona kama bahati mbaya au kitendo cha Mungu”.

13 September 2021, 15:02