Tafuta

12 Agosti utafanyika uchaguzi mkuu nchini Zambia 12 Agosti utafanyika uchaguzi mkuu nchini Zambia 

Zambia:Wito wa maaskofu nchini kuepuka vurugu 12 Agosti katika uchaguzi mkuu

Maaskofu nchini Zambia wanatoa wito kwa raia wote kupiga kura kwa amani na kuepuka vurugu ili kufikia malengo ya kisiasa.Ni katika matazamio ya uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 12 Agosti 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 12 Agosti 2021, ni siku muhimu nchini Zambia ambapo raia wake wanakaribishwa kupiga kura ili kumchagua Kiongozi wa Nchi yao na wabunge wa kitaifa. Hata hivyo katika matazamio ya uchaguzi huo mkuu, Jumapili tarehe 1 Agosti 2021, katika Kanisa Kuu la kianglikani la Msalaba Mtakatifu, huko Lusaka, kulikuwa na wakati wa maombi ya kiekumene ya amani, ambapo wito wa nguvu wa kutotumia nguvu na vurugu ili kufikia malengo thabiti ya kisiasa umezinduliwa na Askofu Mkuu Ignatius Chama, wa Jimbo la  Kasama na Mwenyikiti wa Baraza la Maaskofu nchini Zambia  (Zccb).

Katika hotuba yake amesema, “Kama Kanisa tunaamini kabisa kwamba pande zote zinazohusika katika mchakato wa uchaguzi lazima zioneshe kujitoa kwao kwa ajili ya amani kwa kujiepusha na vurugu, vitisho na matumizi ya nguvu kama njia ya kufikia malengo yao. Vurugu ​​ni ya siasa za enzi za mawe, na vitisho havitoi washindi, lakini ni shida zaidi”. Ili kuwa na uchaguzi huru, wa haki na amani Askofu Mkuu wa Kasama alisema kwamba wanaitwa kuwa na roho ya unyenyekevu wa kweli huku akihimiza kuwa wasione fadhila hii kama ishara ya udhaifu, bali ni kipengele cha ukuu. “Ni hasa kwa sababu ya maono haya yaliyopotoka, wakati mwingine viongozi wa kisiasa wako tayari kuwadhalilisha wapinzani wao na kulinda maslahi yao tu, kwa hasara ya wanyonge na maskini zaidi”, kwa mtazamo kama huo, kiongozi huyo alisisitiza kwamba  hiyo sio zaidi ya kichocheo cha mzozo.

Katika matazamio hayo ndipo wito kutoka kwa rais wa ZCCB kwa raia wote ili kufanya wema, ambao inamaanisha ustadi mzuri, na sio udhaifu. Kwa dhati alisema “ni fadhila ya wajenzi wa amani na inamaanisha kuwa na nguvu ya ndani ya kutochukua hatua mbele ya uchochezi”. Ni matumaini ya kiongozi huyo kwamba wanasiasa wa Zambia, pamoja na wale wasio na msimamo, pamoja na wafuasi wao, watakuwa wenye fadhili kwa kila mmoja kabla, wakati na baada ya uchaguzi, wakati washindi watakapotangazwa. Fadhila nyingine iliyokumbukwa na Askofu Mkuu Chama ilikuwa ile ya uvumilivu ambayo inamaanisha kuchukuliana kwa upendo.

Askofu Mkuu alisema kuwa “Subira inamaanisha kutokuwa mwepesi wa hasira  au kutolipuka mbele ya uchochezi unaofanywa na mtu mwingine”. Kwa kuzingatia hilo, rais wa Baraza la maaskofu amesisitiza kwamba “Wakati umefika wa kuelewa kwamba amani sio tu kutokuwepo kwa vita au kudumishwa kwa nguvu kati ya maadui. Badala yake, ni tunda la haki na upendo ambalo sisi sote tunapaswa kutekeleza, kama watoto wa Mungu”. Hatimaye, Askofu Mkuu Chama alimalizia hotuba yake kwa kutoa wito kwa wazambia kwamba “Wambiani, popote mlipo, ninawaomba mchague kufanya kazi kwa amani na kuishi au kuchagua kufanya kazi dhidi ya vurugu za kisiasa na kufa.

Chama cha Patriotic Front (Pf), kinachoongozwa na Rais Edgar Chagwa Lungu, anayetaka kuchaguliwa tena kwa hawamu ya pili ya miaka mitano, na wapinzani wengine, miongoni mwake ni chama cha United cha maendeleo ya kitaifa (Upnd), kinachoongozwa na Hakainde Hichilema  watakao kuwa pamoja  katika kinyang’anyiro cha kura tarehe 12 Agosti 2021. Lakini mashauriano yanatarajiwa kuwa magumu kwa sababu katika  wiki za hivi karibuni, kiukweli, mivutano kati ya pande hizo mbili imekua, na visa vya vurugu vilifanywa na pande zote mbili kwa mapanga na shoka. Tayari mnamo mwezi Juni Tume ya Uchaguzi ilikuwa imesimamisha vyama hivyo viwili kutoka katika  kampeni ya uchaguzi katika mji mkuu na katika wilaya nyingine tatu, kwa sababu ya mapigano. Kupigwa marufuku zaidi yanahusiana na kampeni za uchaguzi wa nyumba kwa nyumba ambazo haziwezi kufanywa na vikundi vya zaidi ya watu watatu, wakati serikali imepeleka jeshi na jeshi la anga ili kusaidia polisi kudumisha utulivu.

Ikumbukwe, Zambia sio jambo jipya la vipindi muhimu vya uchaguzi. Mnamo 2016, kiukweli, kura za urais ziliwekwa alama na mapigano, vurugu na udhibiti wa uhuru wa vyombo vya habari, licha ya ukweli kwamba walikuwa watu wa tatu baada ya kuanzishwa kwa vyama vingi nchini humu, ambapo ilifanyika mnamo 1991 tu, mwishoni mwa kipinid cha urais wa  muda mrefu wa Kaunda. Kwa kuongezea, 2020 ilishuhudia mjadala mkali kati ya Chamama cha 'Patriotic Front' na vikosi vya upinzani ambavyo vinashiriki matukio ya rushwa na shughuli nyingine haramu kwa watendaji, kama biashara haramu ya mbao, mikataba iliyotolewa na vigezo visivyojulikana, utoaji wa idhini mpya ya madini kwa kampuni za kigeni na usimamizi usio wazi wa fedha za serikali.

03 August 2021, 16:33