Tafuta

Hakuna aliye mgeni Hakuna aliye mgeni 

Mons.Vitillio:Tume ya Uhamiaji Katoliki inaongeza mshikamano wake ulimwenguni

Tume ya Uhamiaji Katoliki ya Kimataifa (ICMC)inaadhimisha miaka 70 katika utume wake ili kulinda na kuhudumia watu waliotokomezwa,wakiwa ni wakimbizi,wanaotafuta hifadhi,wakimbizi wa ndani,wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu na wahamiaji,bila kujali imani,rangi, kabila au taifa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika wiki iliyopita ripoti za vyombo vya habari zimeongezeka juu ya mikasa kuhusu wahamiaji na wakimbizi wanaokimbia nchi zao katika boti mbovu ambazo hazistahili wakijaribu kufika Ulaya. Moja ya hivi karibuni iliingia Jumamosi wakati boti hiyo iliripotiwa kupinduka kwenye pwani ya Dakhla, Maroccoo, katika mkoa wa Sahara Magharibi, ambapo makumi kadhaa yanaaminika kutoweka na kuhofiwa kufa. Shirika la Kimataifa la Uhamiaji linakadiria kuwa zaidi ya watu 1,140 wamekufa mwaka huu pekee kwa kujaribu kutafuta kuhamia Ulaya kutoka nchi kama Libya na Tunisia. Wakati hali ya Ulaya kuhusu uhamiaji wa kupata chanjo kwa kiasi kikubwa, ukweli ni wa kiulimwengu. Mashirika mengi Katoliki yanasaidia kwa kutoa msaada wa dharura na huduma za makazi ya muda mrefu kwa wahamiaji na wakimbizi. Shirika kubwa katoliki linalofanya kazi katika uwanja huu ni Tume ya Kimataifa ya Uhamiaji Katoliki au ICMC iliyoko jijini Geneva Uswis ambayo inaleta pamoja ufikiaji wa mashirika ya kitaifa ya mabaraza ya maaskofu ulimwenguni kote. ICMC inalinda na kuhudumia watu walioondolewa, pamoja na wakimbizi, wanaotafuta hifadhi, wakimbizi wa ndani, wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu, na wahamiaji, bila kujali imani, rangi, kabila au taifa.

Monsinyo Robert Vitillo ni Katibu Mkuu wa Tume hii ya ICMC na alifanya mahojiano na  Vatican News juu ya ufikiaji wa huduma hii. Katika siku za hivi karibuniamesema zaidi ya wahamiaji 800 wameokolewa katika bahari ya Tyrrhenian, lakini Waokoaji wa shirika lisilo la kiserikali (NGO) haliwezi kuwaleta pwani. Na kwa kuelezea ukweli huu na mwenendo wa kuongezeka kwa watu wanaosonga, iwe Ulaya au katika sehemu zingine za ulimwengu, amesema kuwa  awali ya yote kabisa, ni kweli kwamba hii inatokea Ulaya. Pia hufanyika ulimwenguni kote, na wahamiaji na wakimbizi wanapoteza maisha yao baharini, jangwani, na katika maeneo ya baridi na milima. Cha kusikitisha, amesema hawajui ukweli huu kila wakati ikiwa wanafuata tu habari huku Ulaya au katika nchi zenye kipato cha juu. Kwa maana  hiyo, vifo hivi vya kutisha ni jambo la ulimwengu na hupuuzwa na watu wengi sana. Monsinyo Vitillo amependa vile vile kusema kwamba kwanza lazima tukumbuke kwamba uhamiaji ni sehemu ya hali ya kibinadamu na hii imekuwa ikitokea tangu nyakati za kihistoria.

Watu wanalazimika kukimbia mateso hatari na ya kutishia maisha na vurugu wakiwa na matumaini ya kujipatia uhuru na kujenga mustakabali mpya wa familia zao. Kutambuliwa kama “mkimbizi,” kulingana na Mkataba wa Geneva wa 1951, hupewa wale watu ambao wako nje ya nchi zao na wana “hofu  msingi ya mateso kwa sababu ya rangi yake, dini, utaifa, uanachama wa kikundi fulani cha kijamii au maoni ya kisiasa ”. Wanapewa ulinzi maalum ambao wanasimamiwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Wakimbizi wa Umoja wa Mataifa(UNHCR). Lakini pia kuna watu wengine wengi ambao wamezuiliwa katika majaribio yao ya kufikiriwa katika hali ya wakimbizi, au ambao ndani ya mipaka ya nchi zao wamelazimika kukimbia kwa sababu kubwa, pamoja na ghasia za genge, ukosefu wa sheria, hali mbaya ya tabianchi, ukosefu kamili wa lishe ya kutosha na maji safi, usafirishaji haramu wa binadamu, na kutoweza kupata kazi nzuri na kulipwa kwa haki. Mara nyingi, wanataka kukaa nyumbani, lakini wanajua kuwa kuishi katika familia nzima huwalazimisha kuhamia. Nyakati zingine, wazazi wanahisi kulazimika kulipa wasafirishaji na wafanyabiashara haramu ili kuwaleta watoto wao kwa kile wanachotarajia itakuwa usalama, uhuru, na fursa mpya za maisha yenye hadhi.

Katika kujibu swali la ni nini ICMC inafanya ili  kusaidia ikiwa katika hali za dharura au hata kwa makazi ya muda mrefu na ujumuishaji wa wanaowasili katika nchi zinazowakaribisha amethibitisha kuwa ICMC ilianzishwa miaka 70 iliyopita mnamo 1951 na Papa Pio XII na aliamuru kuunda mtandao kwa mabaraza ya Maaskofu yote, mashirika na taasisi nyingine zinaoongozwa na ukatoliki na ambazo zinajibu mahitaji ya wahamiaji na wakimbizi ulimwenguni kote. Kwa maana hiyo, wengi wanajishughulisha na mtandao huu wa kimataifa wa ICMC hambao utumika kama wajibu wa kwanza katika dharura zinazohusiana na uhamiaji katika ngazi ya kitaifa, na hata katika ngazi za kijimbo na parokia. Kwa maana hiyo Sekretarieti ya ICMC huko Geneva inajaribu kusaidia wanachama wake kwa kutoa sasisho na habari juu ya hali na mwenendo wa uhamiaji ulimwengu na wa kanda, na kwa kuwahimiza kushiriki uzoefu wao mzuri na mafunzo waliyo yapata, pamoja na changamoto, kwa kujifunza pamoja na kujenga uwezo, kupitia wavuti wao na kupitia majukwaa yao ya vyombo vya habari  na mitandao ya kijamii.

Monsinyo Vitillo katika mahojiano hayo ikwa anataka kutoa wito wake, ni kitu gani anaomba leo hii, mkuu wa ICMC amependa kurudia maneno yaPapa  Francisko kwa sababu amesema kuwa amefanya miito mingi tangu mwanzo wa upapa wake na ni vizuri hali hii ambayo imo ndani ya taalimungu na tamaduni za Kanisa letu kwa miaka elfu mbili iliyopita kuendelezwa. Amenukuu kwa mara nyingine tena vitenzi vinne muhimu ambavyo Papa alivisisitizia juu ya uhamiaji na ukimbizi kuwa ni:kukaribisha, kulinda, kuhamasisha, na kujumuisha. Wakati mwingine watu husema kwamba vitenzi hivi vinatumiwa kupita kiasi, lakini anafikiria kuwa vinafaa sana hasa katika hali ya kutokuwa na uhakika na kukataliwa kwa hali halisi ambayo inakabiliwa na wahamiaji na wakimbizi katika ulimwengu wa leo, hasa kwa sababu ya kuongezeka kwa dalili za utaifa ambao tunaona katika jamii ulimwenguni kote. Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kwa urahisi lakini kwa nguvu ya kumtendea mgeni na kumwona kama zawadi ya Mungu, ambayo tumefundishwa katika Agano la Kale na Agano Jipya na katika utamaduni mkuu ya imani. Ikiwa tuko wazi kufanya hivyo, basi tunaweza kuifanya dunia hii kuwa mahali pazuri zaidi, mahali salama kwa wale ambao wamelazimika kukimbia, iwe ni kwa mateso au sababu za kisiasa au sababu za kiuchumi na kuwapa nafasi ya kufurahi utu kwamba waliupokea kutoka kwa Mungu mwenyewe. Pili, hata sisi pia kama tunajifungulia ili kunufaika na wakimbizi na wahamiaji ulimwenguni leo na sio tu kama wanavyolazimika kujibu mahitaji yao na mahitaji yaw engine. Kwa maan hiyo wito wake sio wa asili lakini unaegemea katika uongozi wa Baba Mtakatifu Francisko kwa kutanguliza jukumu la kukutana na Yesu kwa kila wahamiaji na mkimbizi na watu wote walio pembezoni au kupuuzwa na kukataliwa na jamii inayoitwa tawala.

Kwa kuwatia moyo wakatoliki ili washiriki kikamilifu katika kusaida na kuongeza uelewa wa hali hii  ya uhamiaji Monsinyo Vitillo amesema kuwa kwanza kabisa, ni  kuelewa, na kujumuisha katika maisha yao ya imani, mafundisho ya Kanisa letu kuhusiana na wahamiaji na wakimbizi. Wakatoliki wengi hawaonekani kufahamu mafundisho kama hayo au hatua hizi  kwa niaba ya wahamiaji kama hao kwa zaidi ya milenia mbili. Pia, amemewahimiza Wakatoliki wengi, ambao wanatokana kwa wahamiaji au wakimbizi kukumbuka jinsi mababu zao wenyewe, hata babu na bibi na wazazi, walihamia mahali pengine, labda kwa sababu ya mateso, au kwa sababu ya machafuko ya kisiasa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, au kwa sababu ya uwezekano bora wa kiuchumi. Mara nyingi, watu wale ambao leo hii hukataa wahamiaji na wakimbizi, wao wenyewe walitoka katika nchi nyingine au mkoa wa ulimwengu na walipokelewa na kukaribishwa katika nchi zao mpya za nyumbani. Vile vile anadhani kuwa ni muhimu sana kwetu kuwajua wakimbizi na wahamiaji. Ni rahisi kuwaita kuwa ni shida au sababu au mafuriko ya watu wanaofika. Lakini, mara tu utakapowajua watu hawa, na kushiriki nao, na kuelewa kuwa wana mahitaji na mahitaji sawa kama tuliyo nayo, kwamba wana zawadi zile zile ambazo tunazo, basi upinzani na kukataliwa vitatoweka, na kukubalika zaidi na kupendana kama kaka na dada katika Mungu mmoja vvile vile udugu utakua.

09 August 2021, 15:55