Tafuta

classroom-1866519.jpg

Porto Rico:14Agosti ni maandamano dhidi ya ukoloni wa kiitikadi shuleni!

Kutokana na mjadala unaoendelea kutaka kuanzisha mtaala wa shule wa mafunzo juu ya ukoloni wa kiitikadi,Baraza la Maaskofu wa Porto Rico wameandaa maandamano ya kupinga itikadi hiyo tarehe 14 Agosti.Kulingana na Katekisimu ya Kanisa Katoliki,wazazi wana haki na wajibu wa kuwasomesha watoto wao wakifuata mafundisho ya Injili na raia wote lazima wafurahie uhuru kamili na huduma zinazotolewa na Serikali.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Mjadala mkali huko Puerto Rico juu ya kuanzishwa, katika mitaala ya shule, wa kozi juu ya “ukoloni wa kiitikadi na mipango mingine inahamasishwa ili kuwezesha utekelezaji wake na tayari imetangazwa kuwa itaanza kutumika mwaka ujao. Kwa sababu hiyo Baraza la Maaskofu Kitaifa (Cep) imetoa taarifa ambayo inasema kuwa na  wasiwasi juu ya uamuzi huu na inawaalika raia wote wanaopinga mpango huu kushiriki katika maandamano yatakayofanyika tarehe 14 Agosti 2021 kuanzia manispaa ya jiji. Wakikumbusha kuwa, kulingana na Katekisimu ya Kanisa Katoliki, wazazi wana haki na wajibu wa kuwasomesha watoto wao wakifuata mafundisho ya Injili, viongozi hao wanasema kwamba “raia wote lazima wafurahie uhuru kamili   na huduma zinazotolewa na Serikali, kwa sababu kuwa Wakristo haiwafanyi kuwa tofauti au duni kuliko idadi yote ya watu”.

Kufuatia na hili ndipo wanatoa wito “kwa mamlaka ya serikali ili kutopunguza haki za wazazi Wakatoliki kuishi na kutenda kulingana na imani na dhamiri zao, kwa sababu wana haki halali ya kutaka watoto wao wasomeshwe bila kuwekewa hadharani kwa itikadi zinazoshambulia moja kwa moja imani zao”.  Kiukweli, maaskofu wanaendelea kusema kiwa wakitumia haki yao ya asili, wazazi na waamini wa kawaida wana uhuru wa kuelezea wasiwasi wao na maombi yao kuhusu kuwekwa kwa njia thabiti na yenye amani kila wakati”. Hasa kwa kuwa hali hii ni ya kiitikadi zaidi kuliko kisayansi”, wanasisitiza Baraza la Maaskofu (CEP).

Hatimaye, wanawahimiza washiriki wote wa kufanya maandamano hayo ili wafanye kwa amani, bila kujiruhusu kukasirishwa au kutumiwa na wale ambao, hata katika nyanja ya dini, wanaweza kuwa na malengo mengine ambayo yanaweza kusababisha kutomheshimu kila mtu katika hali yake, kwa maana hiyo maaskofu wa Porto Rico waanatumaini kuwa hakuna mtu, kwa sababu ya hali yake ya kibinafsi, ulemavu, asili, dini, mielekeo inayoweza kuwa kitu cha kunyanyaswa, vurugu, matusi na ubaguzi usio wa haki”.

Hata hivyo katika moja ya hotuba za Baba Mtakatifu Francisko amekuwa akielezea juu ya hali hizi ambazo zinazidi kuibka ulimwenguni kwa mfano alisema kuwa "ukoloni mkongwe umepita, ukaingia ukoloni mamboleo, lakini kwa sasa kuna ukoloni wa kiitikadi". Alisema hayo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari  ambapo alizungumzia kuhusu familia, vijana na dhamana ya Serikali; amani, upatanisho na msamaha wa kweli; umuhimu wa kutangaza na kushuhudia kweli za maisha ya binadamu; madhara ya ukoloni wa kiitikadi sanjari na utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote; cheche za mpasuko wa Kanisa na umuhimu wa unyenyekevu katika maisha na utume wa Kanisa. Ni wakati anarudi kutoka hija ya kitume Barani Afrika kuanzia tarehe 4 hadi 10 Septemba 2019.

03 August 2021, 15:36