Tafuta

Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mula wa Jimbo Kuu Katoliki la Juba nchini Sudan Kusini. Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mula wa Jimbo Kuu Katoliki la Juba nchini Sudan Kusini. 

Sudan Kusini:Wawakilishi maaskofu waomba Rais Kiir kujumuishwa

Hivi karibuni wawakilishi wa maaskofu wamekutana na Rais Kiir wakiomba kujumuishwa katika mchaakato wa utekelezaji wa Mkataba katika kumaliza migogogoro nchini humo.Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini viliibuka mnamo 2013,miaka miwili tu baada ya uhuru wake kutoka Sudanna kusababisha vifo vya watu 400,000 na milioni nne wakakimbia makazi yao kwenda nchi nyingine.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Kujumuisha pia viongozi wa kidini wa Sudan Kusini katika utekelezaji wa Mkataba uliofufuliwa juu ya Utatuzi wa Migogoro huko Sudan Kusini (R-Arcss), ndivyo ujumbe wa maaskofu wa Sudan Kusini ulivyo muomba Rais Salva Kiir wa nchi hiyo ambaye tarehe 27 Julai 2021 alikutana na wawakilishi wa viongozi wa dini ili kutamaza kwa pamoja mchakato wa amani ulioanza na makubaliano yaliyotiwa saini huko Addis Ababa mnamo tarehe 12 Septemba 2018. Katika uwakilishi huo alishiriki Askofu  Stephen Nyodho Ador Majwok, wa Malakale,  Askofu mstaafu  Paride Taban, wa Torit na Askofu Mkuu Stephen Ameyu Martin Mulla wa Juba. Mkutano huo ulifanyika zaidi ya wiki moja mara baada ya mazungumzo mapya ya amani yaliyoandaliwa na kufanyika kuanzia tarehe 15 hadi 18 Julai na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, kati ya serikali ya mpito iliyofufuliwa ya umoja wa kitaifa (R-TGoNU) na Muungano wa Upinzani wa Sudan Kusini- Sudan Kusini/ Jeshi (Ssoma/ Ssuf), Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Ssoma-Real Sudan (Ssoma/ Rsplm), na vikundi viwili ambavyo havijasaini mkataba R-Arcss.

Wakuu hao dini kwa mujibu wa Askofu Ameyu katika mahojiano kwenye blogi ya Amecea, walisisitiza kuunga kwao mkono kwa mchakato unaoendelea. Wakati huo huo, walielezea hitaji la kujumuisha viongozi wengine wa kidini katika mazungumzo ambayo hakuna kiongozi yeyote wa dini aliyeitwa hadi sasa. Umuhimu wa kuwashirikisha viongozi wa dini wenyewe katika mchakato wa upatanisho, haki na amani kati ya wahusika kwenye mzozo kwa maana hiyo ulitiliwa mkazo. Wajumbe hao walisisitiza jinsi amani ilivyo muhimu kwa watu wa Sudan Kusini, pia wakikumbuka majukumu ya upinzani hasa kwa faida ya wote.

Hata hivyo mchakato huu utakuwa mzuri wamesisistiza  walisisitiza wakuu hao watatu ambao na ambao walionesha kuridhika na uhusiano mzuri kati ya Serikali na Kanisa. Kwa upande wake, Rais Kiir alikaribisha ombi hilo na aliahidi kuwasilisha katika duru ijayo ya mazungumzo yaliyopangwa kufanyika mwezi Septemba, Oktoba na Novemba. Duru mpya ya mazungumzo itawakilisha kipande zaidi cha kile kinachoitwa “Mpango wa Roma”, mchakato wa amani sambamba uliozinduliwa mnamo 2020 na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuleta kwenye meza ya mazungumzo pia harakati za upinzani ambazo hazikusaini upya Mkataba wa 2018. Hatua hii inaongeza matokeo muhimu yaliyopatikana na mazungumzo katikati ya Julai ambayo vyama vilitia saini ramani ya ujumuishaji wa Real Splm na SSUF/A katika utaratibu wa uthibitisho wa kusitisha mapigano (Ctsamvm) na ya mchakato wa mazungumzo itawakilisha sehemu ya kile kinachoitwa 'Mpango wa Roma', ambao ni mchakato wa amani sambamba  na uliozinduliwa mnamo 2020 na Jumuiya ya mtakatifu Egidio ili kuleta pamoja kwenye meza ya mazungumzo pia harakati za upinzani ambazo hazikusaini kwa upya Mkataba wa 2018. Hatua hii inaongeza matokeo muhimu yaliyopatikana na mazungumzo ya mwezi Julai ambayo vyama vilitia saini ramani ya ujumuishaji wa Real Splm na SSUF/ A katika utaratibu wa uthibitisho wa kusitisha mapigano (Ctsamvm) na ramani ya mazungumzo ya kisiasa juu ya sababu za mzozo, mwisho ambao washiriki walijitolea kusaini makubaliano ya jumla.

Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini viliibuka mnamo 2013, miaka miwili tu baada ya uhuru wake kutoka Sudan, na kusababisha vifo vya watu 400,000 na milioni nne wakakimbia makazi yao kwenda nchi nyingine na wengine kurundikana ndani. Kwa asili ya mgogoroni mzozo wa kisiasa kati ya Rais Salva Kiir, wa kabila la Dinka, na Makamu wa Rais wa zamani Riek Machar, wa kabila la Nuer, ambao tangu Februari 2020 wameunda serikali ya umoja wa kitaifa inayotokana na makubaliano yaliyotiwa saini mnamo 2018 baada ya makubaliano mengine kadhaa na kukomesha moto wa vita ambao umepuuzwa.

Mchakato wa amani umeungwa mkono kila wakati na Makanisa ya Kikristo na Baba Mtakatifu Francisko pia amefuata hali hiyo huko Sudan Kusini kwa wasiwasi mkubwa. Jambo muhimu zaidi ni mafungo ya kiroho yaliyofanyika jijini Vatican mnamo Aprili2019 na viongozi hao wawili wapinzani. Mkutano ambao unaonesha kwa dhati picha ya Papa Francikso akibusu miguu yao na ambayo inabaki kwenye kumbukumbu ya ulimwengu. Mnamo Desemba 24 mwaka jana Baba Mtakatifu Francisko na Mkuu wa kianglikana Askofu Mkuu Justin Welby, pamoja na Msimamizi wa Mkutano Mkuu wa Kanisa la Scotland Martin Fair, walikuwa wameandika ujumbe wa pamoja kwa watawala wa Sudan Kusini, wakionesha kufurahishwa na maendeleo yaliyofanywa na wakati huo huo wakisisitiza kwamba ni muhimu kufanya hata zaidi ili watu wahisi kabisa hali za amani. Ujumbe huo pia ulithibitisha nia yao ya kutembelea nchini humo mara tu hali itakaporuhusu.

02 August 2021, 15:47