Tafuta

Askofu Eduardo Hiiboro Kussalawakati wa kutembelea watu wake Askofu Eduardo Hiiboro Kussalawakati wa kutembelea watu wake 

Sudan Kusini:dini zimeungana kwa ajili ya amani ya Nchi

Hivi karibuni viongozi wa kidini Sudan Kusini wamehitimisha utume katika vijiji na miji ya viongozi wa kidini wa Baraza la madhehebu ya kidini na mashirika ya kimataifa.Askofu Edward Hiiboro Kussala,wa Tombura-Yambio na mjumbe wa uwakilishi akihojiwa na Vatican News amesema kwamba wamepeleka ujumbe wa upendo na maridhiano ambayo yamegusa mioyo ya watu.Linaendelea kusaidia kimaadili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ulikuwa ni utume wa Mungu. Ni katika kijiji cha amani mahali ambamo viongozi wa kidini wa Sudan Kusini wametimisha katika mji na vijiji vya nchi hiyo, utume uliohitimishwa tarehe 10 Agosti 2021, ambapo kwa mujibu wa Askofu wa Jimbo katoliki la Tombura-Yambio na mjumbe mwakilishi amebanisha kuwa umeleta matokeo mazuri.

Akihojiwa na Vatican News, Askofu Askofu Edward Hiiboro Kussala, wajimbo katoliki la  Tombura-Yambio amesema “ tumegusa mioyo ya watu ambao wameteseka kwa sababu ya vurugu na tumeonesha ukaribu na huruma”. Utume huo ulikuwa unawahusisha wawakilishi wa dini mbali mbali na baadhi ya mashirika ya kimataifa, kwa ajili ya lengo la kukutana na watu na viongozi wakuu wa kisiasa, ili kutafuta kuisha kwa mapigano ya kikabila ambayo kwa miaka sasa yanazalisha vifo na nchi nzima kuwa na majeraha makubwa ya  umaskini wa kudumu na mgogoro mkubwa wa kikatiba.  “Ujumbe wetu wa upendo na mapatano, na watu wameridhishwa na matembezi haya kwa kutusikiliza” amehakikisha Askofu Hiiboro Kussala.

Vile vile  ujumbe wao, umesikilizwa hata  na makundi ambayo yapo katika mapigano. Askofu amesisitiza kuwa kama inavyotokea mara nyingi, kwamba si watu wote lakini wana utashi wa kuelewa. Hii ni kutokana na kwamba kuna watu wengi ambao wanasikiliza na wengine hawataki waona amani inakuwapo kwa sababu ya kutafuta faida kubwa kupitia migogoro hiyo. Askofu ameongeza kusema kuwa “ ninaweza kusema kwamba zaidi ya asilimia 75 ya watu ambao tumekutana nao wameelewa ujumbe wetu;  hawa lakini ni wanawake, watoto na wazee wenye mapenzi mema. Pamoja nao pia tumeweza kusali sana”.

Akifafanua juu ya hali halisi ya Nchi kwa sasa Askofu Hiiboro  amethibitisha kuwa tatizo kuu zaidi ni ukosefu wa uongozi. Bila hili, bila seikali ya nguvu na inayoweza kuratibu, ni kuunda hali halisi ya kuchanganyikiwa. Kwa sasa kuna makundi mengi ya kisiasa ambayo hayataki kuelewa kwa ajili ya wema wa Nchi. Baadaye kuna ukosefu wa haki. Kwa mfano, watu wenye makosa ya uhalifu wajinai wanakwenda gerezani kwa siku moja tu na kisha wanaachiwa uhuru. Na zaidi, hakuna nguvu za polisi ambao wanaweza kuheshimu na kulinda usalama, na vile vile kuna umaskini wa kutisha, kwani watu hawana chakula, madawa, na vitu msingi vya maisha. Kwa maana hiyo walio wengi wanakimbilia vurugu ili kupata chochote. Raia wanateseka sana na mara nyingi wanasema: “maaskofu hatuna chakula, hatua madawa, tusaidieni” lakini umaskini wa Kanisa letu unaweza kufanya nini? Je fedha zinaweza kupatikana wapi?

Kwa kuhitimisha hata hivyo Kanisa nalo nchini Sudan Kusini liko katika shida kwa maana Askofu anasema, Kanisa lina mamlaka ya kimaadili halina jambo jingine. “nimejaribu kuomba msaada kwa mashirika mengi ya kimataifa, lakini kwa sababu ya janga la uviko wanasema hatuwezi kufanya lolote. Wananiambia: Padre Hiiboro, hatuna fedha, lazima kufikiria watu wetu

13 August 2021, 15:53