Tafuta

Papa wakati wa Ziara ya kitume katika Jumuiya ya  Qaraqosh kwenye Kanisa la Bikira Mkingiwa dhambi Papa wakati wa Ziara ya kitume katika Jumuiya ya Qaraqosh kwenye Kanisa la Bikira Mkingiwa dhambi 

Iraq:Sinodi ya Kanisa la Wakaldayo ni kutembea pamoja na kusoma ishara za nyakati!

Upyaishwaji wa Kanisa,mapinduzi ya mchakato wa liturujia na Katekisimu,mafunzo ya wakleri,hali halisi ya wakristo wa Iraq.Ndiyo mambo msingi ayaliyo katika ratiba ya sinodi ya Kanisa la Kikalifayo iliyoanza tarehe 9 Agosti na itamalizaka tarehe 14 huko Baghdad nchi Iraq.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Aliyefungua kazi ya Sinodi na ambayo itahimitishwa katika mkesha wa siku kuu ya Mpalizwa, Jumamosi tarehe 14 Agosti ni Kardinali Raphael Sako Patriaki wa Babilonia wa wakaldayo, iliyoanza Jumatatu na ambapo alielezea mada ambazo zipo katika sehemu mbili ambazo ni hitaji la kutembea kwa pamoja na roho ya kweli ya kisinodi na dharura ya kupyaisha ili kuweza kuleta mabadiliko ya utumaduni na jamii ya kisasa, na kujibu mahitaji mapya ya waamini.

Kard.Sako:Inahitajika kutembea kwa umoja  kamili

Katika hatua ya sasa ya kutokuwa na uhakika na utulivu wa kijamii na kisiasa nchini Iraq na katika nchi nyingine ni muhimu kutembea pamoja kwa ushirikiano kikamilifu na kutoa majibu ambayo sio ya zamani na yaliyo tayarishwa mapema kwa ajili ya maombi  na mahitaji ya watu”, amesisitiza Kardinali Sako katika hotuba yake. Aidha amesema: “Kama maaskofu, tumeitwa kusoma ishara za nyakati”.

Kuhusu mageuzi ya kiliturujia

Marekebisho ya kiliturujia yaliyoanzishwa na Kanisa la Wakaldayo kwa msukumo wa Patriaki mwenyewe ili kuyafanya yaweze kupatikana kwa waamini imezingatiwa katika mtazamo huu wa mktano wao. Katika suala hili, Kardinali Sako ameona jinsi ambayo yaliyomo,kama  lugha na mtindo wa tamaduni  zaidi ya miaka elfu moja na kuzaliwa katika muktadha tofauti kabisa,  wakati mwingine amesema hutenganishwa na unyeti na hali za ulimwengu wa kisasa. Na ndio sababu, amesisitiza, kwamba “ni jambo lisilo na mantiki kushikilia na maneno ya tamaduni hiyo. Lazima kuwe na 'kubadilishana' kiutamaduni na Kanisa linaitwa kujipyaisha ili kuwalisha waamini wake katika maisha yao ya kila siku, kuanzia na dhana kwamba tamaduni  hufanyika kwao, na ni njia na sio kufika mwisho ". Aidha amesema: ”Lazima tufikirie  juu ya Wakaldayo hasa vijana na wale waliozaliwa katika nchi za Magharibi ambao wanajua kidogo au hawajui chochote juu ya tamaduni hii na kwa maan hiyo hawapendi kusali, kwa sababu hakuna mawasiliano yanayowagusa hasa katika lugha yao, mantiki na utamaduni wao”. Kwanjia hiyo hitaji lililooneshwa na Patriaki pia kusasisha katekisimu na njia za kielimu kulingana na muktadha wa kiutamaduni na kijamii uliobadilishwa katika Kanisa hili la kikaldayo.

Wakristo wa Iraq waangaziwe dhamiri ya masuala ya amani, haki, uraia na uhamiaji

Hali ya Wakristo nchini Iraq ni miongoni mwa masuala mengine yaliyozungumzwa katika hotuba yake kardinali sako. Katika suala hili, Kardinali Sako amesisitiza kwamba "katika mazingira magumu kama vile Iraq, Kanisa halipaswi kuchukua jukumu la kisiasa, lakini badala yake linafanya kazi, pamoja na ujasiri wa kitume na uwajibikaji, kuangazia dhamiri juu ya masuala kama ya amani, haki  kijamii, uraia na uhamiaji. Dhamira ya Makanisa pia ni ile ya kuwa sauti inayopanda mbegu za udugu, upendo, amani, usalama, mshikamano, ushirikiano kwa furaha na kuomba haki", na kusisitiza huku akihitimisha "umuhimu wa Kuimarisha uwepo wa Kanisa la Wakaldayo nchini Iraq".

 

12 August 2021, 19:57