Tafuta

Umuhimu wa utunzaji bora wa Mazingira katika kuenzi Waraka wa Laudato si Umuhimu wa utunzaji bora wa Mazingira katika kuenzi Waraka wa Laudato si 

Mwongozo wa maadhimisho ya utunzaji wa mazingira kutafsiri kwa lugha ya kiarabu

Lengo lake ni kuruhusu wale wote wanaotaka kushiriki kwa uhai wote katika Nchi za Mashariki ya Kati,katika mpango ambao utaanzia Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba sambamba na siku kuu ya Mt. Francis wa Assisi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baraza la Makanisa ya Mashariki ya Kati (Mecc) limechapisha kwa lugha ya kiarabu “mwongzo wa maadhimisho” katika Kipindi cha Kazi ya Uuumbaji 2021 au cha utunzaji bora wa mazingira, ambacho kitaanza tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba sambamba na siku kuu ya Mtakatifu Francis wa Assis. Lengo lake ni kuruhusu wote wanaotaka kujiunga na kwa Wakristo wa Mashariki ya Kanisa katika ushiriki ulio hai wa utunzaji bora wa mazingira. Mwaka huu, mada ya mpango huo ulioanzishwa mnamo 1989, kama familia kikristo kusheherekea zawadi nzuri ya kazi ya uumbaji: Ni Nyumba kwa ajili ya wote? Kupyaisha Oikos ya Mungu.

Cecilia Dall’Oglio: katika kipindi cha uumbaji, ni mtazamo wa dira kuelekea udugu

“Familia ya Kikristo inaunganika katika sherehe hii ya sala ya Ulimwengu na hatua inayolenga kulinda nyumba yetu ya pamoja, kwa mujibu wa Cecilia Dall’Oglio wa Kamati ya Uendeshaji ya kipindi cha kazi ya Uumbaji, ambayo pia inajumuisha Baraza la Kipapa la Maendeleo ya fungamani ya Binadamu.  Cecilia amesema “Kama wafuasi wa Kristo kutoka ulimwenguni kote, tunashiriki jukumu la pamoja la kuwa walinzi wa mazingira,  kazi ya uumbaji ya  Mungu na mtazamo wa dira kuekeza udugu wa kweli.

Kazi ya pamoja kwa njia mpya ya kujifunza Maandiko

Viongozi wa kidini wa Kamati ya Ushauri ya Kipindi cha utunzaji wa mazingira wanaelezea kuwa kazi ya pamoja inaweza kukuza njia mpya ya kuona Maandiko, au maisha na Dunia katika Oikos ya Mungu na kupata hekima kutoka kwa kaka na dada wote ambao husaidia kila mtu kupyaisha uliwengu wetu kama jumuiya pendwa ya ulimwengu ambayo imeunganishwa na inayotegemeana. Lakini hata hivyo wanaonya kuwa oikos, nyumba ya wote, kwa sasa iko hatarini kwa sababu ya uchoyo, unyonyaji, ukosefu wa heshima, kukatwa kwa miti hovyo na uharibifu wa kimfumo, na kwamba viumbe vyote bado vinapiga kelele,  kwamba leo hii ni vipande vya fahamu za kibinadamu zinazomtambua Mungu anayetenda ili kurejesha na kuiponya Dunia.

Mwongozo ni msaada kwa ajili ya kujifunza mipango ya kiekumene

Ushirikiano wao  kwa hakika wanasema umekuwa, bora japokuwa, umesahaulika na mbaya zaidi, umekataliwa kwa makusudi, viongozi wa dini wamebainisha.Kwa maana hiyo ni matumaini yao na maombi kwamba wanaweza tena kuwa jumuiya hii pendwa ya utume wa kukusudia. Katika kuwasilisha mwongozo kwa lugha ya Kiarabu kwa ajili ya Kipindi cha  Utunzaji bora wa Mazingira Baraza la Makanisa La Mashariki ya Kati (Mecc) linabainisha kuwa maandishi ya mwongozo ni msaada wa kujifunza zaidi juu ya mpango wa kiekumene na kupanga maadhimisho yake na kwamba nyenzo za kujua mambo mengine zaidi ya sala, mikutano na mengine, zinapatikana moja kwa moja kupitia mtandaoni na tovuti ya yao.

18 August 2021, 14:10