Tafuta

Mtakatifu Edith Stein mfano wa kukumbatia msalaba wa Yesu

Mtakatifu Theresa Benedeta wa Msalaba(Edith Stein) ni mfano wa mazungumzo na matumaini ya wakati wote.Edith Stein alikabiliana na kifo dini katika vyumba vya gesi vya Auschwitz Birkenau mnamo Agosti 1942.Ni kilele cha safari ndefu ya maisha ya ndani kama mtawa mkarmeli iliyomwongoza kutoka katika masomo ya falsafa,hadi kufikia kujitoa kwa kuhamasisha ubinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kila tarehe 9 Agosti ya kila mwaka, Mama Kanisa anaadhimisha kumbu kumbu ya Mtakatifu Theresa Benedeta wa Msalaba, ambaye jina lake ni Edith Stein, mtawa na mfiadini wa shirika la wakarmeli, ambaye ni mmoja kati ya watakatifu wasimamizi wa Bara la Ulaya. "Ave Crux, Spes Unica, salamu Msalaba wa pekee wa matumaini ya ulimwengu.  Ni kwa mtazamo wake ambao ukitazama mikono ya Kristo msalabani, tumaini lake pekee, ambalo Edith Stein alikabiliana na kifo dini katika vyumba vya gesi vya Auschwitz Birkenau mnamo Agosti 1942. Ni kilele cha safari ndefu ya maisha ya ndani iliyomwongoza kutoka katika masomo ya falsafa, hadi kufikia kujitoa kwa kuhamasisha ubinadamu na mtawa katika maisha ya ndani. Edith alizaliwa wa Breslau huko Silesia nchini Ujerumani mnamo 1891, binti wa kumi na moja wa wanandoa wa dini ya Kiyahudi, ambapo Edith mara moja alitambuliwa kuwa na akili yake nzuri ambayo ingeweza kupendeza maono ya busara na kikosi cha vijana ambao hawakuwa na dini. Alikatisha masomo yake wakati wa Vita vya Kwanza vya Ulimwengu ili kusaidia askari kama muuguzi wa Msalaba Mwekundu. Hiyo itakuwa ni fursa ya kukutana na mwanafalsafa Husserl, ambayo baadaye akawa msaidizi wake katika Chuo Kikuu cha Fribourg, akiongezea mada ya uelewa na mwanafalsafa Max Scheler, pamoja na usomaji wa maisha ya Mtakatifu Ignatius na maisha ya Mtakatifu Theresa wa Avila, ambayo yalimwongoza kufikia uongofu wa Ukristo.

EDITH STEIN
EDITH STEIN

Imani na Unazi

Edith akiwa na hamu ya kupata ukweli kupitia maarifa na masomo, alishindwa na Ukweli wa Kristo kwa kuyakaribia maandiko ya Mtakatifu Thomas na Agostino. Alipokea Ubatizo na Kipaimara mnamo 1922, dhidi ya mapenzi ya wazazi wake, lakini hakuwahi kukataa asili yake ya Kiyahudi. Wakati wa miaka ya mateso, alikuwa mwalimu na mtawa wa wakarmeli huko Kolon mnamo 1934 kwa jina la Theresa Benadetta wa Msalaba na alikumbatia mateso ya watu wake, yakianzia katika sadaka ya Kristo. Baadaye alihamishiwa huko Holland, nchi isiyo na upande wowote na akiwa katika  utawa wa Ukarmeli wa Uholanzi huko Echt aliandika juu ya "shauku ya kujitoa kama sadaka ya upatanisho kwa ajili ya amani ya kweli na kushindwa kwa ufalme wa mpinga Kristo”.

Shuhuda huko Auschwitz

Miaka miwili baada ya uvamizi wa Kinazi nchini Uholanzi mnamo 1940, alichukuliwa pamoja na Wayahudi wengine 244 Wakatoliki kama kitendo cha kulipiza kisasi dhidi ya maaskofu wa Uholanzi ambao walikuwa wamepinga mateso hadharani na kupelekwa Auschwitz. Akiwa huko yeye alitunza watoto gerezani, huku akiwasindikiza kwa huruma kuelekea kifo na kufundisha Injili kwa wafungwa. Pamoja naye alikuwa na dada yake Rosa, aliyebadilika pia kuwa Mkatoliki na ambaye kwa wakati mgumu sana wa kuuawa alisema: “Njoo, twende kwa watu wetu”. Hapo zamani alikuwa ameandika naye kuwa: “Ulimwengu umewashwa moto: vita kati ya Kristo na mpinga Kristo vimekuwa vikiendelea waziwazi, kwa hivyo ukiamua kuwa wa Kristo unaweza kuombwa kwa kutoa sadaka ya  uzima”.

Mfano wa uvumilivu na kukubalika kwa Ulaya

Mawazo na imani ya Edith Stein yako katika kazi zake, kwa namna ya pekee katika “Kiumbe kuwa wa mwisho na Kuwa wa  Milele” ambayo ni ufupisho wa muundo wa kifalsafa na fumbo ambalo hisia ya mwanadamu huibuka na  upekee wake upo katika uhusiano na Muumba. Binti mashuhuri sana wa Israeli na binti mwaminifu wa Kanisa, ndivyo  alimweleza Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo   1998 wakati wa kutangazwa kuwa Mtakatifu. Hata hivyo Mtakatifu Benedetta ( Edith Stein), tendo la kuwa mtakatifu na msimamizi mwenza wa Ulaya kunamaanisha  kuweka kwenye upeo wa wa juu wa Bara la Kale ile bendera ya heshima, uvumilivu, na kukubalika, lakini pia  ni muhimu kuinua maadili halisi, ambayo msingi wake ni sheria ulimwenguni. Yeye alikuwa mtu wa mazungumzi na matumaini kwa wengi alisema Mtakatifu Yohane Paulo II na kuongeza “Ulaya ambayo ilibadilisha thamani ya uvumilivu na heshima na kutokujali kimaadili juu ya maadili yasiyoweza kujitenga ingejifunua kwa vitisho vyenye hatari zaidi na mapema au baadaye inaweza kujitokeza katika aina mpya chini ya mifumo mipya ya kutisha ya historia yake”.

09 August 2021, 09:19