Tafuta

2019.09.07  Rais Andry Rajoelina wa Madagascar akisalimiana na Papa Francisko wakati wa Zaira yake ya kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius mnamo Septemba 2019. 2019.09.07 Rais Andry Rajoelina wa Madagascar akisalimiana na Papa Francisko wakati wa Zaira yake ya kitume nchini Msumbiji, Madagascar na Mauritius mnamo Septemba 2019. 

Madagascar:Maaskofu kwa Rais Rajoelina,Kanisa linahitaji amani

Katika mkutano wa Maaskofu wa Madgascar na Rais wa nchi hiyo Rajoelina,wamethibitisha kuwa Kanisa linataka amani na msimamo wa nchi na kwamba Kanisa Katoliki halifanyi siasa,badala yake linatoa msaada wa kiroho na ushauri kwa wajumbe wote wa kijamii kwa ajili ya wema wa Nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Baraza la Maaskofu wa Madagascar wamethibitisha kuwa Kanisa Katoliki halifanyi siasa, badala yake linajikita kutoa msaada wa kiroho na ushauri kwa wajumbe wote wa Kanisa na kwa wote kwa ajili ya wema wa Nchi. Wamesema hayo wiki iliyopita walipokutana na Rais Adry Rajoelina ambaye hivi karibuni amenusurika kwenye shambulio lililolengwa kwake. Ilikuwa tarehe 21 Julai ambapo watu sita pamoja na raia wawili wa Ufaransa, walikamatwa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Madagascar kwa madai ya kuhusika katika na njama hiyo. Mkutano wa maaskofu na Rajoelina kwa mujibu wa Shirika la habari katoliki Afrika, ulifanyika kufuatia na wito wa wachunguzi wa Askofu Mkuu Odon Marie Arsène Razanakolona, ​​wa mji mkuu Antananarivo. Kiongozi aliulizwa juu ya uhusiano wake na mratibu anayedaiwa na njama hiyo, Paul Maillot Rafanoharana, askari wa kifaransa na kimadagascar ambaye anadai askofu Mkuu kuwa ni mshauri wake.

Ujumbe ulioongozwa na Kardinali Désiré Tsarahazana, Rais wa Baraza la Maaskofu Madagascar (Cem), ulieleza kwamba, kinyume na inavyoripotiwa na mitandao ya kijamii, Kanisa haliungi mkono mgombea yeyote na wala kufanya siasa. Jukumu lake la Kanisa ni kutoa msaada wa kiroho na ushauri kwa viongozi juu ya tabia na mwenendo wa kuchukua ili kuhakikisha kuwa na amani ya kijamii na utulivu nchini vinatekelezwa. Wakati wa mkutano huo, maaskofu pia walizungumza juu ya dharura za kijamii na kiuchumi zilizopo nchini, wakimhimiza Rais kuendelea na utume wake mgumu. Miongoni mwa shida zilizoripotiwa, janga la Uviko-19, mfumko wa bei ya mahitaji ya msingi, ukosefu wa usalama na ufisadi ulioenea.

Madagascar inakabiliwa na shida kubwa ya chakula, hasa kusini mwa nchi iliyokumbwa na njaa kutokana na ukame. Kulingana na Unicef ​​na Mpango wa Chakula Ulimwenguni (WFP), zaidi ya watu milioni moja wako katika hali ya ukosefu wa chakula na watoto nusu milioni chini ya umri wa miaka 5 wataathiriwa na utapiamlo mkali, pamoja na 110,000 katika hali mbaya na uharibifu usiowezekana kwa ukuaji wao na maendeleo. Hali mbaya ambayo, bila kuingiliwa kwa wakati unaofaa na jumiya ya kimataifa, inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo. Ikumbukwe kwamba Rais Andry Rajoelina, ambaye alikuwa tayari ni meya wa zamani wa mji mkuu wa Antananarivo, yuko katika muhula wake wa pili kama Rais wa Madagascar. Mnamo tarehe 17 Machi 2009 aliwekwa kwenye uongozi wa serikali ya mpito baada ya mapinduzi ya kijeshi kufuatia mapigano makali ya uwanja dhidi ya Rais wa wakati huo Marc Ravalomanana. Alishika nafasi huo hadi 25 Januari 2014, na alichaguliwa tena katika uchaguzi wa urais wa 2018.

04 August 2021, 14:46