Tafuta

Lazaima kulinda maisha tangu kutungwa kwake hadi kifo cha kawaida Lazaima kulinda maisha tangu kutungwa kwake hadi kifo cha kawaida 

Maaskofu wa Marekani watoa wito mpya wa sheria ya kulinda maisha

Katika barua iliyotiwa saini na Kardinali Timothy M.Dolan,rais wa Kamati ya uhuru wa dini na Monsinyo Joseph F. Naumann,Mwenyekiti wa Kamati ya Shughuli za Pro-Life, inasema: “Bunge lilipiga kura kwa njia ambayo haiendani kabisa na mapenzi ya watu wa Marekani,ambao wanapinga sana utoaji mimba unaofadhiliwa na walipa kodi”. Pendekezo la sheria katika suala hili linapatikana katika kifungu cha 4502.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Pamoja na kura 219 kuunga mkono na 208 kupinga mnamo tarehe 29 Julai 2021, Bunge la Marekani liliidhinisha muswada huo wa kifungu 4502 cha mgao wa kiuchumi unaohusiana na kazi, afya, huduma za kibinadamu na elimu. Mswada wa sheria inayohusika haijumuishi, hata hivyo, marekebisho mawili ya muda mrefu kwa pande mbili, zote zinazohusiana na ufadhili wa umma kwa utoaji mimba: marekebisho ya Hyde ya miaka 46 iliyopita ambayo inakataza matumizi ya pesa za walipa kodi kufadhili utoaji mimba isipokuwa katika kesi ya  visa vya ubakaji, uchumba au wakati maisha ya mama yako hatarini; na Marekebisho ya Weldon ambayo yanakataza mashirika ya shirikisho na serikali za majimbo na za mitaa, wapokeaji wa fedha za umma, kubagua mtu yeyote, pamoja na watu binafsi na taasisi, ambayo inakataa kutoa, kulipa au kulipia gharama za utoaji mimba. Kuondolewa kwa vifungu hivi viwili, kwa hivyo, kutalazimisha walipa ushuru wa Marekani kulipia utoaji mimba kwa hiari na kusababisha wataalamu wa afya kutelekeleza mimba, hata dhidi ya imani zao. Kwa kuongezea, waajiri na bima watalazimika kulipia hatua za utoaji mimba.

Hatari zilizooneshwa na maaskofu

Mwitikio wa Mkutano wa Kitaifa wa Baraza la Maaskofu (Usccb), ambao hapo zamani ulikuwa tayari umejielezea kwa haraka wa kupinga sheria hiyo ya (ddl) 4502. Katika barua iliyotiwa saini na Kardinali Timothy M. Dolan, rais wa Kamati ya uhuru wa dini, na Monsinyo Joseph F. Naumann, Mwenyekiti wa Kamati ya Shughuli za Pro-Life, inasema: “Bunge lilipiga kura kwa njia ambayo haiendani kabisa na mapenzi ya watu wa Marekani, ambao wanapinga sana utoaji mimba unaofadhiliwa na walipa kodi”. “Marekebisho ya Hyde yameokoa watu wasiopungua milioni 2.4 tangu kutungwa kwa sheria hiyo”, wanakumbuka maaskofu na kwamba “Sasa, bila hiyo, mamilioni ya wanawake maskini, katika mazingira magumu, watafanya uamuzi usiobadilika kukubali ombi la serikali hadi mwisho wa maisha ya mtoto wao”.

Ukosefu wa haki wa sheria inayohusika

Maaskofu wanasema pamoja na kukiri kwamba sheria inayopendekezwa inajumuisha vifungu vinavyosaidia watu walio katika mazingira magumu, pamoja na wanawake wajawazito, hata hivyo Baraza lao linasisitiza kwamba "licha ya hiyo, ni chaguo lisilo sahihi la kushambulia moja kwa moja, kupitia utoaji wa mimba,ambapo ni maisha ya binadamu yasiyo na hatia. Hii ni kwa sababu kutokuwa na uwezo wa kulinda na kutetea uhai katika sehemu zake zilizo hatarini zaidi kunatoa madai yoyote kwa haki ya vifungu vingine vinavyohusu maskini na dhaifu kabisa ndani ya mtuhumiwa wa jumuiya”.

Sio hivyo tu, Kardinali Dolan na Monsinyo Naumann wanaangazia kwamba “ukosefu wa haki wa sheria inayohusika pia inaendelea kufutwa kwa kukataa dhamiri na kutolewa kwa wataalam wa afya ambao wanaamini kuwa utoaji mimba ni kosa au imani yao inawasukuma kutumikia na kuponya maisha, badala ya kuikandamiza”. Kwa sababu hiyo, “kufadhili uharibifu wa maisha ya watu wasio na hatia ambao hawajazaliwa na kulazimisha watu kuua, kwa kukiuka dhamiri zao, kumbuka maaskofu wanawakilisha unyanyasaji mkubwa wa haki za binadamu”. Kwa hivyo, ombi la wazi la Usccb kwa Seneti ni kumaliza muswada 4502, wakati maaskofu katika Bunge wanaomba kupitisha sheria ambazo zinasaidia kikamilifu na kulinda utu wa binadamu na walio katika mazingira magumu zaidi ndani ya jamii.

02 August 2021, 15:37