Tafuta

Askofu Mkuu Philip Naameh, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Ghana. Askofu Mkuu Philip Naameh, Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki nchini Ghana. 

Ghana:Mpango wa ujenzi wa Kanisa Kuu la Kidini waleta manung'uniko

Mpango wa ujenzi wa Kanisa kuu la kitaifa la kidini,umeleta mashaka kwa maaskofu wa Ghana kuhusu ufadhili uliopendekezwa na serikali,kwa maana Kanisa alikuhusishwa ushauri kuhusiana na kuchangia michango kwa upande watu wa Mungu wa Ghana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kila mzalendo nchini Ghana anapaswa atoe angalau cedi 100 yenye thmani ya dola 6 kwa mwezi ili kujenga Kanisa Kuu la Kitaifa la Kidini. Ndilo pendekezo la Serikali ya Accra iliyozinduliwa kwa watu, lakini ambayo imeibua manung’uniko kwa upande wa maaskofu wa Kanisa. Kwa dhati Baraza la Maaskofu kitaifa wa Ghana (Gcbc), wanalalamikia suala la ukosefu wa kushauriana nao hata kidogo, kati ya watendaji na viongozi wa kikristo katika Nchi hiyo.

Rais wa Baraza la Maaskofu Ghana (Gcbc) na Askofu Mkuu Philip Naameh wa Jimbo Kuu Katoliki la Tamale amefafanua kuwa “ hata kama wakristo ndiyo wanaonufaika zaidi  kwa eneo  jipya la ibada, lakini haiwezekani kudai wao wato mchango ili kulijenga Kanisa hilo.  Njia za kufadhili mradi lazima ziwe tofauti. Kwa  maana hiyo, ndipo, yamoneshwa masikitiko kwamba viongozi wa Kikristo wa nchi hiyo hawajawahi kushauriana na serikali kuhusu jinsi gani ya kuweza kufadhili ujenzi huo.

Hata hivyo hayo yametokea mnamo Julai, ambapo Waziri wa Fedha wa Ghana, Ken Ofori-Atta, alitangaza, kuwa  mnamo tarehe 12 Agosti, uzinduzi wa Klabu ya cedi  100 kwa mwezi, itafanyika ili  kuwaruhusu watu wa Mungu nchini humo kuchangia ujenzi wa Kanisa kuu na kwamba linapaswa kuzinduliwa mnamo 2024 na liwe na uwezo wa viti vya kukaa elfu 5.  Suala hili liliwasilishwa mnamo 2017 kama sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 60 ya uhuru wa nchi hiyo, iliyoadhimishwa mnamo mwezi Machi 6 mwaka huo, kwamba  mahali pa ibada baadaye kutajengwa karibu na Jengo la Bunge katikati mwa mji mkuu, Accra. Ukusanyaji wa fedha za ujenzi zilianza hata hivyo mnamo 2018.

08 August 2021, 13:33