Tafuta

Mfuko wa Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji linaomba mchango wa kutengeneza Biblia kwa lugha ya Kalanga kwa ajili ya watoto. Mfuko wa Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji linaomba mchango wa kutengeneza Biblia kwa lugha ya Kalanga kwa ajili ya watoto. 

Zimbabwe:Biblia ya watoto yatafsiriwa kwa lugha ya kalanga

Imetafsiriwa Biblia kwa lugha ya kalanga,ambalo ni kabila mojawapo la Zimbawe kwa ajili ya watoto, na lugha ambayo inazungumzwa karibu na shule 188. Kufuatana na hilo Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji linaomba na kutoa wito wa mchango kwa ajili ya kupata nakala ili kuzigawa kwa watoto 12,960.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji linaomba mchango wa kuweza kutengeneza nakala 12,960 za Biblia kwa lugha ya kalanga kwa ajili ya watoto ili kuweza kuzigawa nchini Zimbabwe kwa watoto hao wa kabila la Kalanga, lililoko Magharibi mwa Nchi.

Ni mfuko wenye sheria ya kipapa ambao umekuwa ukichapisha kwa miaka 42 sasa Biblia Takatifu katika matoleo mbali mbali kwa ajili ya watoto, yenye utajiri wa picha nzuri na historia mbali mbali za kibiblia. Hadi sasa zimetengenezwa nakala 191 za lugha ambali mbali kwa ujumla zenye nakala milioni 51.

Lugha ya kabila la Kalanga inajulikana kama moja ya lugha rasmi katika nchi na inazungumzwa na shule 188 mahalia na zaidi katika badhi ya vitabu vya shule hakuna vitabu vingine vya lugha ya kalanga.

Kufuatana na hali hiyo Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji limejikita kufanya tafsiri za Biblia kwa ajili ya watoto na kwa kila nakala ni euro moja, ikiwa na maana ya kwamba kuna ulazima wa kupatikana kwa euro 12,960.  Shirika la Kipapa la Kanisa hitaji linatoa wito kwa wote wenye mapenzi mema kuweza kuchangia kwa ajili ya Biblia ili hata watoto hao wa kabila hili la Zimbabwe liweze kuwa na biblia mpya kwa ajili ya watoto hao.

29 July 2021, 14:55