Tafuta

Baraza tendaji la Baraza la Makanisa Ulaya(KEK). Baraza tendaji la Baraza la Makanisa Ulaya(KEK). 

Ulaya:Shule ya kiangazi ya Kek:kusaidia uhuru wa kidini

Siku za hivi karibuni imefanyika shule ya kiangazi ya VIII iliyoandaliwa na Baraza la Makanisa Ulaya(Kek)kwa lengo la kuhamasisha haki za binadamu katika muktadha wa kujenga na kusaidia kuhamasisha uhuru wa kidini.Shule ya kiangazi iliongozwa na kaulimbiu:“Kuhakikisha Usalama wa Maeneo ya Ibada na Jumuiya za Dini” hasa uhamasishaji wa kile ambacho Wakristo wanapaswa kwa usalama wa maeneo ya ibada.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Kujenga na kusaidia kuhamasisha uhuru wa kidini ni katika nia hiyo msingi wa Shule ya kiangazi ya VIII kuhusiana na haki za binadamu, iliyoandaliwa na Baraza la Makanisa Ulaya (Kek) ambayo imefanyika siku zilizopita kwa njia ya mtadando kwa sababu ya janga la Covid. Tukio lililokuwa likaribishwe jijini Berlin, ni sehemu ya mchakato wa mafunzo na utafiti juu ya hali ya jumuiya za kidini Ulaya ambazo zilibuniwa na Kek kwa kushirikiana na Tume ya Ulaya ili kusaidia kuondolewa kwa aina zote za ubaguzi.

Shule ya kiangazi iliongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuhakikisha Usalama wa Maeneo ya Ibada na Jumuiya za Dini” hasa kukuza uhamasishaji wa kile ambacho Wakristo wanapaswa kufanya kwa usalama wa maeneo ya ibada kuanzia tafakari ya kitaalimungu juu ya umuhimu wao kwa maisha ya Makanisa na ya kijamii barani Ulaya. Tukio la Baraza la Makanisa Ulaya (Kek) lilifunguliwa na utafiti wa kina juu ya thamani ya maeneo ya ibada kwa sasa kwani kama ilivyosemwa, barani Ulaya, kwa karne nyingi, wameshuhudia kukutana kati ya wanaume na wanawake na Mungu.

Hasa kulingana na kumbukumbu hii, mahali pa ibada ni sehemu msingi ya kukuza ukarimu na kushirikisha, mbali na tamaduni za dini binafsi, kama sehemu muhimu ya mapambano kwa ajili ya haki za binadamu. Ni tafakari ya kitaalimungu iliyojikita katika Maandiko Matakatifu ambayo yanapaswa kusaidia kusoma tena yaliyopita na kujenga sasa ambapo Wakristo lazima waombe na kuunga mkono hatua za kimataifa ili kutetea maeneo ya ibada, kama ilivyotokea katika miaka ya hivi karibuni, katika upeo wa macho ambayo huenda zaidi ya ile ya Jumuiya za Ulaya na zaidi katika mifano hali halisi kutoka Kosovo hadi Armenia

Wakati wa Shule ya kiangazi kuhusu Haki za Binadamu, zimewasilisha hatua za hivi karibuni za Jumuiya ya Ulaya katika kufafanua kanuni za utetezi wa maeneo ya ibada zikionesha hitaji la kanuni hizi kutekelezwa katika ngazi ya eneo, pia na uanzishaji wa njia ya kuunda ili kusasisha jumuiya juu ya kile kinachofanyika katika Bara la Kale, na tema hii. Kazi hizo zilifahamishwa na uwasilishaji wa ripoti juu ya visa vya unyanyasaji dhidi ya maeneo ya ibada vya mwaka jana. Kwa kuongezea, kulikuwa na mazungumzo ya hali hii ambapo, hata Ulaya, haki ya uhuru wa kidini na maeneo ya ibada yana mashaka, ikionesha jinsi mashambulio ya haki hii yanavyosababisha kutovumiliana na vurugu ambazo zinahusishwa na dini.

Wakati kinyume chake sababu nyingine kiukweli ni juu ya jambo hili kwamba Wakristo wameitwa kuingilia kati kwa sababu dini haiwezi kamwe kutumiwa kuhalalisha kuondolewa kwa haki ya uhuru wa dini. Pamoja na Shule hii ya kiangaza, Baraza la Makanisa Ulaya (Kek) lilitaka kuimarisha kujitoa kwake katika kukuza na kulinda uhuru wa kidini,na  sio Ulaya tu, bali wakithibitisha kwamba ahadi hii ni kiini cha safari ya kiekumene katika fursa ya Mkutano huo, na kama alivyokumbuka, siku chache kabla ya kufungua  kazi za Shule ya kiangazi Jørgen Skov Sørensen, katibu wa Kek, huku akihimiza ushiriki mkubwa zaidi wa jumuiya, kwa kupatikana tena kwa urithi wa kawaida ambao tayari unaunganisha Wakristo katika kutetea haki za binadamu kwa jina la neno la Mungu.

30 July 2021, 15:28