Tafuta

2021.07.28: Nchini China, kuwekwa wakfu wa askofu Li Hui 2021.07.28: Nchini China, kuwekwa wakfu wa askofu Li Hui 

China:amewekwa wakfu Askofu mwandamizi wa Pingliang

Mchungaji wa tano kutangazwa baada ya kuanza kwa mkataba wa makubaliano ya muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China kuhusiana na kuteuliwa kwa maaskofu,amewekwa wakfu tarehe 28 Julai.

VATICAN NEWS

Askofu mpya wa tano baada ya saini ya Mkutaba wa makubaliano ya  muda kati ya Vatican na Jamhuri ya Watu wa China kuhusiana na suala la kuteuliwa kwa maaskofu  amewekwa wakfu tarehe 28 Julai 2021 chini China. Huyo ni Askofu Antonio Li Hui, mwandamizi wa Pingliang, katika Wilaya ya Gansu.

Sherehe za kuwekwa wakfu, kwa mujibu wa habari kutoka ka Wavuti wa Kanisa Katoliki nchini China ziliongozwa na Askofu Giuseppe Ma Yinglin wa Kunming,Wilaya ya Yunnan. Askofu Li Hui alizaliwa mnamo mwaka 1972 katika kata ya Mei, Wilaya ya Shaanxi, na kujiunga na Seminari ya Jimbo la Pingliang kunako 1990 na akapata digrii  katika Seminari ya kitaifa ya Kanisa Katoliki nchini China. Alipata daraja la upadre mnamo mwaka 1996.

Kuteuliwa kwake kwa upande wa Baba Mtakatifu, umethibitishwa na msemaji wa vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni kamba ulitokea mnamo tarehe 11 Januari 2021.

29 July 2021, 14:48