Tafuta

Vatican News
Mtazamo wa Msikiti huko Yerusalemu Mtazamo wa Msikiti huko Yerusalemu 

Wcc yaomba kuheshimu maeneo matakatifu ya Yerusalemu!

Katibu Mkuu wa Mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni,Wcc,mchungaji Ioan Sauca,ameomba mamlaka ya Israeli kuheshimu Maeneo matakatifu katika Mji wa kizamani wa Yerusalemu,kwa ajili ya amani na mshikamano. Wamombwa wote waache kabisa vurugu na matendo ya uchochezi ili wawe msimamo thabiti.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Baraza la Makanisa Ulimwenguni (Wcc) linalaani vikali vurugu zilizotokea usiku wa kuamkia tarehe 7 Mei 2021 karibu na Msikiti wa Yerusalemu mahali ambapo maelfu ya wapalestina wakiwa katika sala yao ya mwisho wa siku kabla ya kuisha mwezi wa mfungo wa Ramadhani, ambapo kwa upya wamepigana kati ya polisi na waisraeli. Takwimu inahesbabu ni zaidi ya majeruhi miambili. Katibu Mkuu wa Mpito wa Baraza la Makanisa Ulimwenguni, (Wcc), mchungaji Ioan Sauca, ameomba mamlaka ya Israeli kuheshimu Maeneo matakatifu katika Mji wa kizamani wa Yerusalemu, kwa ajili ya amani na mshikamano. Wameombwa watu wote waache kabisa vurugu na matendo ya uchochezi ili wawe msimamo thabiti.

Hata hivyo Jumapili tarehe 9 Mei  mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu, katimiito mbali mbali na salamu, Papa Francisko ameonesha masikitiko ya kile kichotokea katika nchi Takatifu. Amewaomba kwa dhati kutafutamuafaka wa mazungumzo na maelewano. Mapigano hayo, ni moja wapo ya mapigano makali huko Mashariki ya Yerusalem katika miaka ya hivi karibuni, ni sehemu ya picha ya mvutano mkali wa kisiasa na kijamii uliosababishwa na uwezekano wa kufukuzwa kwa familia za Wapalestina kutoka kitongoji cha Sheikh Jarrah, karibu na Jiji la Kale, kwa faida ya wakoloni  wa Israeli. Tahadhari ya mamlaka iko juu zaidi kwa kutarajia sikukuu ya Eid-al-Fitr mnamo tarehe 12 Mei ambayo inaashiria kumalizika kwa Ramadhani, na kuvutia makumi ya maelfu ya Waislamu kwenye Mlima wa Hekalu.

Kuongezeka kwa vurugu huzo pia kunatia wasiwasi katika Baraza la Makanisa Ulimwenguni, ambalo tangu 2008 limesaidia jumuiya ya Wapalestina wa Sheikh Jarrah kupitia Mpango wake wa Kusindikiza Kiekumene huko Israeli na Palestina (Eappi) na inasaidia familia zilizotishiwa kufukuzwa. “Kwa niaba ya jumuiya ya kiekumene ya Baraza la Makanisa, ninaelezea masikitiko makubwa kwa hali  ya familia za Wapalestina za Sheikh Jarrah na machafuko na vurugu zilizofuata”, amesema mchungaji Sauca.

Jibu, halipaswi kuwa vurugu tena, lakini huruma na haki kwa watu wa Palestina walioathiriwa na hali hii isiyo ya haki. Mzozo wa muda mrefu wa kisheria uliosababisha maandamano hayo unahusu nyumba nne zinazokaliwa na familia za Wapalestina, ambazo zipo kwenye ardhi inayodaiwa na Wayahudi. Mahakama Kuu ya Israeli ilikuwa imealika vyama hivyo kutafuta maelewano, lakini bila mafanikio. Kwa maana hiyo ndipo  waliona  uamuzi wa kujadili mzozo katika chumba cha mahakama ili kumaliza hukumu hiyo. Usikilizaji umefanyika Jumatatu tarehe 10 Mei 2021 wakiwa pia na wasiwasi wa  hatari ya kusababisha vurugu zaidi. Kwa Wapalestina wa Sheikh Jarrah, unyakuzi wa ardhi unawakilisha hatua zaidi katika lengo la miaka kumi la ukoloni wa Kiyahudi kuwafukuza Waarabu kutoka Yerusalem Mashariki.

10 May 2021, 19:42