Tafuta

Vatican News
2021.01.24 Papa Francisko akikabidhi zawadi ya Toleo jipya la Biblia:Kueneza Neno hadi miisho ya dunia 2021.01.24 Papa Francisko akikabidhi zawadi ya Toleo jipya la Biblia:Kueneza Neno hadi miisho ya dunia  

Uingereza:“Antiquum ministerium” itasaidia kuboresha imani!

Maaskofu wa Uingerza na Walles wanakaribisha kwa furaha Barua ya Papa Antiquum ministerium na ili waboreshe namna ya kuwasilisha imani yao

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika taarifa iliyotolewa kwenye Tovuti ya Baraza la Maaskofu katoliki wa Uingereza na Galles na Askofu David Evans, Rais wa Kamati kwa ajili ya Katekesi kwa niaba ya Maaskofu, wamekaribishwa kwa shangwe kuu, barua binafsi ya Papa Francisko Antiquum ministerium, yaani mambo ya kale ambayo inatambua huduma ya katekisita.

Askofu Evans amesema “tunataka kujua ni kitu gani tupendekeze kwa Kanisa la Ulimwengu na lile la Uingereza na Walles kutoka katika Barua ya motu proprio”. Na tunataka kupongeza kazi ya ukaribu kwa kina kwa makatekisita wote katika mchakato wa historia ya miaka ya Kanisa. Tunaweza kufikiria kwa namna nyingi kwa jinsi ambavyo makatekisita wameweza kuwasindikiza wengine katika safari ya imani na si tu kama walimu, lakini wamekuwa zaidi kama mashuhuda, wakitembea na watu wanaotafuta kumjua Bwana na Kanisa lake.

Katika taarifa hiyo hiyo kwa waandishi wa habari, Baraza la Maaskofu wa Uingereza na Wales unathibitisha kwamba, katika kujibu maneno ya hati mpya ya Baba Mtakatifu Francisko, itaifanya huduma  ya katekista kuamua mchakato muhimu wa malezi na vigezo vya kuanza kutumika. “Katika kufundisha wanaume na wanawake wa huduma ya katekista tutazingatia pia shida ambazo zinaweza  kujitokeza kutokana na shida ya janga”, wameandika maaskofu wa Uingereza, tena  “na jinsi ya kukabiliana na changamoto ya kuzifanya jamuiya zetu kuwa na nguvu na kuboresha njia tunayowasilisha imani yetu”.

15 May 2021, 14:33