Tafuta

Vatican News
Mkutano kuhusu uwekezaji wa Uchumi Afrika uliofanyika Paris  Mkutano kuhusu uwekezaji wa Uchumi Afrika uliofanyika Paris   (AFP or licensors)

Nigeria:Mawakiri katoliki waomba kufanya Mkutano na rais wa nchi

Katika barua iliyoandikwa na chama cha kitaifa cha Mawakiri katoliki (NACL) wanamwomba rais wa nchi ya Nigeria Bwana Muhammadu Buhari aitishe kwa haraka mkutano juu ya usalama wa nchi. Katika uthibitisho wao uliosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wake kitaifa,Mwakiri Chukwuma Ezeala na Angela Odunukwe, wanalaani vurugu za kihalifuzinazotendeka bila kuthibitiwa na wanaomba vyombo vya usalama kudhibiti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Chama cha kitaifa cha Mawakiri katoliki (NACL) wanamwomba  rais wa nchi ili kukubaliana na matendo mengi ya vurugu dhidi ya raia wasio na hatia, wakiwemo mauaji na kuteka nyara kwa lengo la kupata fidia. Hayo yameandikwa katika hati yao ambapo wamemsihi Rais Muhammadu Buhari aitishwe kwa haraka mkutano juu ya usalama. Katika uthibitisho wao uliosainiwa na Mwenyekiti na Katibu wake kitaifa, Mwakiri Chukwuma Ezeala na Angela Odunukwe, wanalaani kwa dhati vurugu za kihalifu ambazo zinafanywa bila kuthibitiwa na wanaomba nguvu za vyombo vya usalama kama Polis ina majeshi kuongeza maradufu jitihada zake  za kuhakikisha usalama wa  maisha na mali watu wa Nigeria. Katiba ya shirikisho, wanakumbusha mawakiri katoliki kuwa inasisitiza  usalama wa wazalendo ni moja ya kipaumbele cha serikali.

Mkutano ambao umeombwa na mawakiki Katoliki (NACL) unapaswa uwe na lengo la kutafuta suluhisho la ukosefu wa usalama ambao umeenea kwa muda mrefu, na ambao unatesa Shirikisho la nchi hiyo kubwa barani Afrika. Tendo la vurugu ambazo pia zimekumba Kanisa Katoliki na ambao hivi karibuni katika Parokia ya Mtakatifu Vincent Ferrer, Malunfashi, kwenye  Serikali ya Katsina kaskazini mwa nchi ya Nigeria, na utekaji nyara, pia suala la  Padre mwingine Alphonsus Bello aliyekutwa ameuawa, mwingine pia mwenye  umri karibu miaka 50 Padre Joe Keke. Kutoka vyanzo vya magazeti, inasemekana kuwa Polisi wamewaweka mbaroni huko Katsina watu wawili, miongoni mwao, hata mlinda usalama wa parokia kushiriki shambulizi.

26 May 2021, 15:15