Tafuta

Vatican News
Kanisa Kuu la Rabat nchini Morocco Kanisa Kuu la Rabat nchini Morocco  (Vatican Media)

Morocco:Jimbo kuu la Rabat linajiandaa kufanya Sinodi ya Pili

Kwa jina la Yesu na Injili:ni Kanisa lipi la Morocco?Ndiyo mada ya Sinodi ambapo watachambua changamoto mpya za uinjilishaji katika nchi ya Afrika Kaskazini kulingana na mabadiliko ambayo yametokea katika siku za mwisho kwa miongo miwili wakati wa Sinodi ya kichungaji 2021-2022.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mwanzoni mwa mwaka ujao wa kichungaji 2021-2022 Jimbo Kuu katoliki la Rabat nchini Morocco, litafanya Sinodi yake ya pili kijimbo kwa zaidi ya miaka 25 kati ya sinodi ya kwanza ambayo ilifanyika tangu 1993 hadi 1995. Aliyetangaza hilo siku ya Jumapili ya Siku Kuu ya Pentekoste ni Kardinali Cristóbal López Romero, (Sdb), anayeongoza jimbo kuu hilo tangu 2018. “Kwa jina la Yesu na Injili: ni Kanisa lipi la Morocco?” Hii ndiyo kauli mbiu ya mkutano ambao utachambua changamoto mpya za uinjilishaji katika nchi ya Afrika Kaskazini kulingana na mabadiliko ambayo yametokea katika siku za mwisho kwa miongo miwili.

“Miaka ishirini na mitano baada ya Sinodi ya kwanza, ambayo ilizaa matunda mazuri, tunafahamu kwamba Kanisa limebadilika na bado linabadilika, likijumuisha kila kitu ambacho kimemwilishwa tangu wakati huo”, amesema kardinali wa Uhispania wa shirika la wasalesian katika ujumbe wake. “Sinodi ni mchakato wa safari, lakini pia hali ya akili na kiroho ambayo inahitaji sisi kutembea pamoja, kufanya safari pamoja. Ikiwa tunataka kuwa Kanisa ambalo ni ishara ya Morocco, ni muhimu kuruhusu kuhojiwa na kuguswa na tamaduni tofauti za Kanisa letu na pia kuwa na mizizi katika utamaduni na ukweli wa nchi hii” amesisitiza. Kwa maana hiyo “tutaweza kutoa utamaduni wa kiinjili, na sio kupitia kugeuza watu imani, lakini kwa njia ya kuvutia kwa njia  njia yetu ya kuwa katika huduma zetu”.

Kulingana na Kardinali López Romero, ni kuwa Kanisa ambalo ni ishara, Jimbo kuu linahitaji kutathmini historia yake, ili kujua utofauti wake, utajiri na changamoto ambazo zinajumuisha, kusoma na kutafakari juu ya Neno la Mungu, kusikiliza matarajio ya watu wa Morocco, kuwa wazi kwa ajili ya uongofu ambao Roho anawaita, kutambua chaguzi za kichungaji ambazo zinapewa kipaumbele na kuwa waaminifu katika Roho wa Yesu. “Ni suala la kujiweka katika hali ya uwazi kwa Roho, kutoka sisi wenyewe, kutembea kuelekea Ufalme, kutafuta pamoja mapenzi ya Mungu na kukutana na wengine, kardinali amefafanua”. Kutokana na hili ndipo mwaliko kwa waamini wote wa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa safari ya sinodi kwamba: “Tunapaswa kuomba na kutafakari pamoja, kukaribiana, kujuana vizuri na kutafuta njia bora za Kanisa letu. Hii inamaanisha kuwa Sinodi inajali sisi sote Wakatoliki, wa Jimbo kuu la Rabat” na kwamba hakuna mtu anayeweza kuhisi ametengwa, amethibitisha Kardinali López, akibainisha kuwa Sinodi pia itakuwa wazi kwa ushiriki wa Wakristo wa madhehebu mengine na pia kwa Waislamu.

Kwa habari ya kupangwa kwa mkutano wa sinodi, askofu mkuu wa Rabat ametaja kwamba itagawanywa katika makanisa ya jimbo na maparokia ambamo watashiriki harakati za kikanisa zilizopo katika jimbo kuu. Maelezo ya uandaaji yatafafanuliwa kwa kina katika barua ya kichungaji itakayochapishwa Septemba ijayo. Ujumbe wa Kardinali López kwa hiyo umemalizika kwa mwaliko kwa waamini kuiombea Sinodi, na kukabidhi tmafanikio yake kwa “Mashahidi Watakatifu wa Marocco na kwa ulinzi wa Maria, Mama yetu wa Morocco. Kanisa Katoliki la Morocco leo lina waamini wapatao 23elfu sawa na 0.07% ya idadi ya watu karibu Waislamu wote, jumuiya inayoundwa na wageni wengi wao ni Wazungu (ambao wanaongezwa na  vijana kutoka Afrika chini ya jangwa  Jangwa la Sahara ambao walikuja Morocco kwa sababu masomo ), wamegawanyika  kati ya Jimbo kuu la Rabat na lile la  Tangier. Maeneo ya shughuli ya utume wa Kanisa mahalia, ambalo lina hadhi ya kisheria inayotambuliwa kwa sababu ya fadhila  na Barua ya hati miliki ya 1984 ya Mfalme Hassan II wa wakati huo, ni pamoja na kazi za hisani, elimu na mazungumzo.

Hasa, ni kuhamasisha mazungumzo ya kidini na kuelewana kati ya Waislamu na Wakristo ina nafasi kubwa, pia shukrani kwa msaada wa Mfalme Muhammad VI ambaye alikuza mipango mbali mbali katika eneo hili. Na mazungumzo halisi kati ya dini yalikuwa katikati ya safari mbili zilizofanywa nchini na Mtakatifu Yoahane Paulo II mnamo 1985 na na Papa Francisko mnamo 2019, ambapo Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba mshikamano kati ya waamini unaitwa kujiweka katika huduma ya familia nzima ya wanadamu, kutoa michango asili ya ushughulikia dharura za ulimwengu kama vile dharura za ekolojia na uhamiaji.

26 May 2021, 15:58