Tafuta

Vatican News
Mwahamiaji kutoka Haiti kwenda Marekani Mwahamiaji kutoka Haiti kwenda Marekani 

Marekani:Maaskofu wanapongeza hadhi ya ulinzi wa muda kwa wahamiaji wa Haiti

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa,Haiti,mojawapo ya mataifa maskini zaidi ulimwenguni,imekuwa katika hali ya ukosefu wa usalama mkubwa,uliowekwa na wimbi kubwa la vurugu na utekaji nyara,katika hali ya mzozo mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.Maaskofu wa Marekani wanafurahishwa na uamuzi wa Rais Biden kutoa hati ya muda ya kulinda kwa miezi 18 kwa wahamiaji wa Haiti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maaskofu nchini Marekani wamekaribisha uamuzi wa Utawala wa Biden kutoa Hati ya Muda ya Kulinda (TPS) ya miezi 18 kwa wahamiaji wa Haiti. Hatua hiyo, ambayo inaruhusu raia wa kigeni wa mataifa fulani kukaa na kufanya kazi nchini Marekani katika kipindi ambamo kurudi kwao nchini kwao kunachukuliwa kuwa hatari. Ni taarifa iliyotolewa Jumamosi iliyopita. Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, Haiti, mojawapo ya mataifa masikini zaidi ulimwenguni, imekuwa katika hali ya ukosefu wa usalama mkubwa, uliowekwa na wimbi kubwa la vurugu na utekaji nyara, katika hali ya mzozo mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Vurugu nchini humo zinathibitisha kuongezeka kwa ushawishi wa magenge yenye silaha nchini, wakati idadi ya watu bado inasubiri kuanza kwa kampeni ya chanjo dhidi ya Covid-19.

Katika muktadha huu, Askofu Mario E. Dorsonville na Askofu David J. Malloy, marais, wawili mmoja wa Kamati ya Uhamiaji na mwingine wa Kamati ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Marekani (Usccb), kwa maandishi wamekaribisha na kuridhika kwa kutambuliwa hatua hiyo (TPS) kwa raia wa Haiti, wakati wanaelezea mshikamano na waathiriwa wa vurugu  na maaskofu wa Haiti ambao wamelaani mara kwa mara uasi unaojitokeza  nchini humo. Vurugu ambayo pia imeathiri Kanisa la Haiti moja kwa moja kutokana na utekaji nyara uliolengwa makuhani, watawa na walei wamekumbusha maaskofu.

Maaskofu wa Merekani pia wanamemuomba Rais Jovenel Moïse achukue hatua kwa ajili ya masilahi bora ya watu wa Haiti kwa kuheshimu na kudumisha haki na utu wao na hatimaye wanaomba Utawala wa Biden kushughulikia hali ya kukata tamaa ambayo inatesa nchi kupitia hatua za kidiplomasia na kibinadamu. Licha ya kumalizika kwa muda wake wa urais Moïse, uliopingwa sana na asasi za kiraia na upinzani kwa sababu ya  ufisadi na mageuzi yenye utata kikatiba, lakini hadi sasa amekataa kuacha uongozi wa serikali akisubiri uchaguzi ujao wa rais uliopangwa kufanyika Septemba, wakati Bunge lilimaliza  muda wake mnamo Januari 2020. Kukwama kwa taasisi ni sehemu ya shida kubwa ya kiuchumi na kijamii ambayo vimbunga, matetemeko ya ardhi na magonjwa ya milipuko yamechangia katika miaka 15 iliyopita, kuanzia na mtetemeko wa ardhi mbaya ambao ulipiga nchi magoti mnamo 2010.

Maaskofu wa Haiti wameingilia kati mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni juu ya mgogoro na ukosefu wa usalama katika kisiwa hicho, pamoja na mipango ya kupendeza ya maandamano, kama vile migomo miwili ya taasisi za Katoliki zilizoitwa baada ya utekaji nyara wa makuhani 5, watawa 2 na walei watatu waliotekwa nyara manmp Aprili,11 na baadaye kuachiliwa huru. Kwa kuongezea, wamewaalika waamini kushiriki katika mipango mbali mbali ya maombi, pamoja na Novena kwa Mama yetu wa Msaada wa Daima, msimamizi wa Haiti, iliopangwa kuanzia tarehe 18 hadi 26 Juni 2021.

26 May 2021, 16:13