Tafuta

Msaada kwa wasiojiweza Msaada kwa wasiojiweza 

Malawi:“Catholic Girls Arise” wajitolea kusaidia jirani

Wasichana wa kikundi kiitwacho“Catholic Girls Arise”,kilichoanzishwa mnamo Novemba 2020 jimboni Mangochi kimejitahidi kuishi upendo wa kikristo kwa kutoa mchango wa kununua zana mbali mbali kuwasaidia maskini na walemavu wa kimwili katika Parokia ya Ulongwe,jimbo la Mangochi Malawi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kikundi cha wasichana karibia 200 kutoka Malawi wamechagua njia ya kuishi maisha yao kwa ukaribu na upendo kuulekeza kwa jirani,hasa kwa mujibu kuishi mafundisho ya Injili na mawazo ya kuhamasisha, kuanzia wao binafsi ili kuleta mabadiliko katika ulimwengu. Hawa ni wasichana wa kikundi kiitwacho “Catholic Girls Arise”, kilichoanzishwa mnamo Novemba 2020 jimboni Mangochi.  Shukrani kwa jitihada zao, wasichana hao kwa ajili ya kusaidia walemavu kimwili katika Parokia ya Ulongwe, jimbo la Mangochi, ba  kwa kujitolea wamewezesha kununua na kukabidhi viti vya walemavu, mashuka na vitu mbali kama vyakula na vifaa vya usafi binafsi kwa ajili ya watu wenye kuhitaji masaada zaidi.

Padre Chris Sichinga, msimamizi wa kikundi hicho cha wasichana "Catholic Girls Arise", amethibitishwa kufurahishwa na kushangazwa na ukarimu wa wasichana hao ambao wamechangia katika mpango huo, kwa kuonesha upendo wa urahisi wa matendo ambayo yanabadili maisha ya wengi. Hawa wanajikita katika matendo ya dhati, mafundisho msingi wa imani yao. Ni ishara ambayo wameweza kushirikisha na wakiishi kile ambacho Bwana Yesu Kristo anafundisha kwa Kanisa lake.

Naye Sister Theresa Mulenga, mmoja wa mjumbe wa kikundi na kama mshauri wa uratibu wa watu wa kujitolea amebainisha kupendezwa kwa msaada ambao wamewezesha kuutoa japokuwa kwa zana ndogo walizokuwa nazo. Hawa wameelewa kwa kina kazi hii ya ufadhili kwa ngazi mahalia kwa njia ya michango midogo midogo ya wajumbe wa kikundi na wadau wengine, amesisitiza. Vile vile,Mtawa huyo ameandika kwamba Mungu anapobariki, kwa neema zake ni vema kumshukuru kwa kushirikisha na wale ambao ni wadhaifu zaidi au maskini. Hazikukosa shukrani kubwa kutoka  upande waliopokea ufadhili huo na wote wameelezea furaha na shukrani kwa watu wa kujitolea wa kikundi cha “Catholic Girls Arise”  kwa uwezekano wao wa kushirikisha kidogo walichonacho na ndugu wenye kuhitaji.

26 May 2021, 15:47